Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

TUKICHUNGUZA kwanini kanuni za UCHAGUZI WA CHUPI wa Mheshimiwa unafanana na wa CHANGUDOA

>> Wednesday, November 04, 2009

[Tahadhari: Wazo limepinda !:-(]

NI kweli MALENGO ya mchagua chupi sio yale yale,...
.....ndio maana kuna wenye chupi kama BICHIKOMA.


Ngojea nifafanue:

Tabia ya mtu unaweza kujifunza hata kwa kumuangalia chupi,...
.... na kwa bahati mbaya MHESHIMIWA na CHANGUDOA wote wanaendeshwa na WANACHO kilenga kufanikisha na kwa hilo WANAFANANA.

Na nikifafanua ZAIDI kipengele kwa kutumia chupi naweza kusema:


Uchaguzi wa chupi una sayansi zake kama tu uchaguzi wa Gari au Matunda.

Ndio maana ni vigumu kujua nia na MADHUMUNI ya mchagua chupi ,....
... na kama ingekuwa ni rahisi namna HIYO, tungekuwa na CHUPI za aina moja tu zenye mshono MMOJA na labda saizi tu ndio zingekuwa tofauti kutokana na UKWELI kuna watu wengine sehemu zao ZA kuvalishwa chupi ujazo ni SAIZI pipa wakati kamwili kenyewe debe.

UCHAGUZIII!
Ndio , binadamu ukimpa nafasi ya kuchagua atachagua kwa sababu binafsi, na UBINAFSI WA BINADAMU ndio vifanyavyo MHESHIMIWA na CHANGUDOA kufanana hata katika uchaguzi wa CHUPI!:-(


NIMEACHA!
Swali:
  • Kwani unauhakika ilikuwa lazima wanaume na wanawake wawe na chupi tofauti?

  • Si unakumbuka CHANGUDOA ni MHESHIMIWA kwenye eneo lake?
  • Si unajua tukidai dhumuni la kuwa na gari ni USAFIRI TU na kuna COROLLA, ina maana tunamaanisha wote wauzao COROLLA na kununua gari saizi ileile uthamani BENZI ni wajinga?



Hebu tu tubadili hali ya hewa kijiweni kwa kwenda tena South Africa kukutana na Soul Brothers




Au Yvonne Chaka Chaka audhi watu TENA kwa kusifia pombe katika - Umqombothi

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP