Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa WATANZANIA wamkumbukao Mwl. NYERERE ingawa katika KUMBUKUMBU husahau wake UFASHENISTA!

>> Tuesday, November 24, 2009

Mzee alikuwa anatoka ulimbwende na kama ulikuwa makini ungestukia:

Mzee katika VAZI alikuwa na mpaka KIFIMBO,...
.... asichotumia kuchapia.


Mzee alikuwa anavaa mpaka SUTI za MAO,...
.... ambaye itikadi zake kwa makini hakufuatilia.

Mzee alikuwa anaweza KUKUULIZA swali juu ya lako SWALI,...
....ingawa swali lako jibu kalichunia.

Mwalimu alikuwa anahusudu na kushuka Kiingereza,...
....na Kiswahili ndio alitaka WATANZANIA wengine wabobee na kufuatilia.





Na tukiachana na jambo la FASHENI ZA Mwl NYERERE ambazo wakereketwa hawazungumzii kwa kuwa hunogewa zaidi na SIASA zake zaidi :



Swali:
  • SI unakumbuka kitu chochote kama ni FASHENI huja na kama NYERERE hupitwa mpaka na wafuasi wake wakereketwa kama wanauziwa ulimbwende hata wajinsi ya kufikiri KIJINGA upya kama tu uuziwavyo FASHENI MPYA?

  • Kwani hukumbuki Nyerere TUKIACHILIA MBALI SIASA ZAKE alikuwa ni bonge la FASHENI TRENDI SETA kimavazi na labda kwa hilo ndio alikuwa anaeleweka zaidi kuliko sera zake za kujaribu kufanya maofisi ya serikali yasiwe sehemu za kujipatia ulaji kwa wajanja??

  • Wewe kama MTANZANIA unafikiri ulimuelewa NYERERE wakati sasa hivi HISTORIA inazidi kututhibitishia kuwa hata wafuasi wake wakereketwa aliowaachia madaraka walikuwa HAWAMUELEWI?
  • Unafikiri kwa kawaida unakumbuka mambo mangapi ya Mwl NYERERE ambayo unauhakika siyo ya Kawawa au Kingunge?



NI wazo tu hili kada wa chama na wala USIKONDE!:-(

Hebu tubadi mrengo wa mawazo na kwenda KENYA kwa Stella Mwangi aongelee-Biashara/biacara


Au tu Bob Marley asawazishe tena kiutu uzima kwa kitu-Dance Do The Reggae

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP