Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Tukifikiria tena JINSI watu WASUBIRIAVYO mpaka MTU afe ili ndio WAMSIFIE!:-(

>> Friday, November 06, 2009

SIKATAI!

Labda ni kweli kuna watu ni mpaka WAFE a.k.a ZE KUKATA ROHO,....
..... ndio kuna watu hustukia UZURI au UMUHIMU wao katika yao wayaonayo ni ya muhimu.:-(

Lakini bado kwa marehemu aliyekata ROHO,...
.... KUNAUWEZEKANO MKUBWA hazina faida tena SIFA , na KWA aliye hai ASIFIAYE MFU kunauwezekano kwa hilo kuna utaahira AU NI SWALA LA UBINAFSI TU WA WALIO HAI kwa kusifia mfu ILI WAJISIKIE VIZURI kwa kuwa sifa nyingi asifiwazo marehemu UKICHUNGUZA, labda angekua hai labda ndio kwake zingekuwa MUHIMU.:-(


Swali kiduchu:
  • NI watu wangapi HAI SASA HIVI unaoweza kuwasifia NA huwasifii ingawa unauhakika wakifa utadai ''MAREHEMU ALIKUWA MTU MZURI KWELI!''!?
  • Unauhakika wasifiao wafu hawafanyi hivyo kujiridhisha na kujifariji wao WENYEWE au walio hai WENGINE wasikiao hizo sifa ambao MSIFIAJI MFU anajua ni wenye kumzimia MAREHEMU?

NI HILO TU Kingunge na ni WAZO TU!

Hebu tubadili hali ya hewa kwa kwenda Brazil kukutana na Kaoma waturudishie tena -Dançando Lambada


Au tu COCOA TEA atulize KIBARUTI kwa kuzungumzia tu ya jelajela katika -Riker's Island


Au tu Super Cat arudishe tu naye -Ghetto Red Hot

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP