Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MPENZI nahisi inabidi NIKUOE na nalazimika KUKUPENDA kwa kuwa nimpendaye kikweli SIWEZI KUMPATA!:-(

>> Friday, November 06, 2009

[Tahadhari: Kumbuka lijamaa LIFIKIRIALO hivi hili swala, kamwe halitamki kwa sauti MPENZI ASIKIE!:-(]

Katika haya MAISHA ambayo hakuna BREKI ya UMRI kwenda,...
.... siwezi kuendelea kusubiri KWA KUWA UMRI UNAKWENDA wakati NIAMINIYE ninampenda kikweli kubwa kuliko SIJAWAHI KUKUTANA NAYE na bado namuona tu kwenye MAGAZETI hata yale ya kiuchiuchi au tu kwenye mpaka KWENYE taarifa za HABARI hata za hali ya hewa kwenye TV a.k.a LUNINGA.:-(


Inabidi tu HISIA zangu za kukuzoea hata kwa ILE michezo yetu iwezayo mpa mimba mtu ZIGEUKE tu kuwa ni za kwa dhati nakupenda,...
.... kwa kuwa yule mwingine nimpendaye kuliko wewe niliyewahi mpaka kukutana naye , MIYE kanishinda na KWELI hata nikijaribu kumsabahi ANARINGA.:-(


Na wakati hata nikitakakujiaminisha sijazidiwa bahati mbaya, ETI wakati MAISHA YANGU yanaelekea CHINA kama tu yako POOZEO TOTOZ yanapokwenda,....

.... yule watatu nimpendaye zaidi kuliko wewe ,ingawa HUYU nimpendeacho tu ZAIDI hakina zaidi ya kwamba anatako TU zuri kuliko wewe, ETI naye wakati huu wakati KIMAISHA naelekea China, MAISHA YAKE nayo ndio kwanza yako Tanzania na ndio kabisaaa yanatoka mpaka DAR-es SALAAM nilikokuzoea na kuzidi kuelekea IRINGA.:-(


Lakini kama tu WENGINE WAFANYAVYO kihalihalisi ya MAHUSIANO ya WATU WAWILI ,sina ujanja zaidi tu ya wewe kukupenda,...

.....kwa kuwa kwa jinsi nionavyo WALIOKO KATIKA MAHUSIANO waliooa na KUOLEWA au tu wenye wapenzi tayari UCHOCHORONI watokwavyo na denda wakati wanatamani vya wengine hata kama DOGO DOGO ni saizi ya watoto wao, NAANZA KUAMINI LABDA ni FANTASI a.k.a NDOTO ZA ALINACHA ndio MPENZI wa kweli WA MTU duniani,....

.... na naahidi NTAJIFUNZA KUKUPENDA kwa dhati KIHIVYO,.....

.....kama tu HAO WENGINE wapendavyo kwa kuliambia wanalipenda JITU HILI wakati katika FANTASI hata za wakati wanashughulika na shughuli zijazazo UJAUZITO MTU walikuwa wanaendeleza penzi na JITU JINGINE KIFANTASI ndani ya tendo , kwa kuwa KIFANTASI HIZO a.k.a ALINACHA ZA aina ya TAMU ZAIDI IKO NYUMBA YA JIRANI NA SI KWAKO hunogewa zaidi ILE TAMU na KWA HILO wanajisikia vizuri hata kwa habari za kutoka REDIO ZA MBAO kuwa walipendalo KIFANTASI limeonekana sehemusehemu linaafya hiloo na limependezaa ingawa lilipoonekana , BONGE LA kamasi lilikuwa kwenye kadamnasi LINAPENGA.:-(
Swali:
  • Unauhakika HASA kama sasa hivi una-LIMTU, ungeweza kimapenzi au hata kimahusiano usingelibadili hilo LIMTU?

Namaanisha:

  • Kama uko kwenye UHUSIANO, unauhakika kama MATUMAINI YAKO tokea uanze KUWASHWA KIKUBWA yangetimia, ni huyo uliyenaye ungekuwa naye AU TU ume-SETTLE a.k.a IMEBIDI TU UWE NA HILO LIMTU kwa kuwa katika mazingira yaliyopo ndio -The best U can DO a.k.a ndilo LIMTU lidakikalo na kinamna unaweza KULIVUMILIA?
  • Una uhakika wewe ni chaguo la kwanza la wako mpenzi na kama sio kuna madhara?
  • Si inasemekana kwa kawaida wazuri wote wamfaao mtu ATAFUTAYE MPENZI huwa washaoa au kuolewa?

NIMEACHA!
Kumbuka hili ni WAZO TU MKUU wala USITISHIKE !
IJUMAA na WIKIENDI NJEMA MHESHIMIWA!

Hebu tupate sindimba kidogo..



Au hebu ENOMIZIZI wadai tena -Kiviringishe Tena


Basi bwana tuendeleze tu na SWAHILI NATION wakiwa na Chameleon wakileta-Chakacha

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mzee wa Changamoto 6:29 am  

Bado najitahidi kumulika kwa nguvu niuone mstari mwembamba kati ya KULIPIZA na KUSAWAZISHA (Revenge vs Make it even)
Maana kwa mawazo haya mazuri, nafikiria na huyo umuwazaye akiamua kukujibu kwa kuwaza bila kukwambia ili usisikie....Mmmmhhhh!!! Patanoga
Wacha niache mwachiko ili wajiachiao waachie yao
Blessings

Simon Kitururu 9:24 am  

@Mzee wa Changamoto: Afanyaye siri kwa mafanikio si mlengwa hatajua?

Halafu naamini asilimia kubwa ya binadamu hata kama nia si kuficha siri ila bado ni wachaguzi ni nini mtu mwingine wanamwambia.:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP