Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

SABABU KUBWA za kuona aibu kuvua NGUO MBELE ZA WATU labda wala sio HESHIMA!:-(

>> Thursday, November 12, 2009

Ukifuatilia unaweza kukuta kuwa ULIANZA KUINGIA AIBU ,...

.... za kuvua nguo kwa kuwa tu ulistukia WAKUTAZAMAO HATA WAZAZI WAKO wewe ukiwa mtoto , - HATA kwa wako utoto WAKAKUSTUA ni noma na si ujanja kuacha KIPENGELE NJE INGAWA HUJUI MATUMIZI YAKE KIKUBWA, kwa kuwa umekaa TU bila nguo.:-(



Na cha ajabu baada ya kuondokana na UTOTO wakubwa HASA WASIO WAZAZI WAKO wakikuhisi unavutia KWELI ukiwa uchi ingawa UNA AIBU,...
... wanaweza mpaka kuanzisha kipengele kwenye MISS TANZANIA cha kukukalisha uchi - na KWA KUWA kama kikiitwa FASHENI MPYA na uwaaminio ni wajanja UWAZIMIAO wanaokushangilia tunaweza tusishangae ghafla UKITUHUBIRIA unaamini UMEPENDEZA na una BOMBA LA NGUO kwa kuwa hatuoni KITOBO TU katika vazi lako likukalishalo uchi wakati unadai umevaa NGUO.:-(

Swali:
  • Unauhakika kuvaa nguo KWAKO kama hutishiki na kuacha KITOVU na PAJA nje, maana yake sio tu kuficha VITOBO tu na hilo ni kwa sababu tu unaogopa kukalia miba na wala si kwa sababu Baba Mkwe YUPO?
  • Si unajua kuna waaminio kuwa wasiovaa BIKINI ni kwa kuwa TU wana mwili kama MNYOO?
  • Unauhakika unapendeza UCHI?
  • Unafikiri ni kweli tako la nyani linapendeza kwa FISI hata kama jekundu?

HIli ni WAZO TU na usitishike KINGUNGE ingawa hii sio BIBLIA, TORA, ITIKADI YA CHAMA CHA MAPINDUZI au wala KORANI!:-(

Hebu twende tena Kameruni Bebe MANGA alete- Mota Benamaa


Au tu ngojea MAFIKIZOLO warudie tu kitu -Nisixoshelani

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Faith S Hilary 4:08 am  

Kwanza KIDUDE...sasa KITOBO...

Simon Kitururu 6:34 am  

@Candy1: Kidude kwa kawaida kina KITOBO!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP