Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kuwa WASTAARABU na WANAOJIHESHIMU hawaongelei kirahisi NGONO na wakiiongelea waweza kuigeuza jina udhani wanaongelea CHAKULA CHA USIKU !:-(

>> Tuesday, November 17, 2009

Kutokana na waheshimiwa wajuzi wa SWALA NONIHINO wamekubuhu ububu katika swala,...
...labda NDIO MAANA:

  • Kunawaendeleao kujaribu ambayo labda wasingejaribu na kujikuta wanachezea MPAKA mavi katika jaribio.

  • Kuna waendeleao kupata MIMBA ambazo wasingezipata kwa kuwa tu walidhani aina ya staili ya chuma mboga ni bonge la mkao wa UZAZI WA MAJIRA/njia ya uzazi wa mpango wakati bado hutaki mtoto na unacheki tu chombo kama kikitiwa swichi gari linawaka kiutamu hata katika majaribio.

  • Na kuna wapatao MAGONJWA kwa kutostukia MHESHIMIWA si kweli anaheshima akiwa uchi na labda kwa kuendekeza vya gizani nawe labda anaviendekeza GESTI pia akienda kwenye semina na baameidi, Nyumbani mara mojamoja ili ndoa isiharibike kabisa, migombani kwa kua ndiko akikoanzia TAALUMA ,- na UKIMWI na KISONONO aliupata wakati NI mzoefu TU wa SWALA na kwa mtu waliyezoeana sana tu na mpaka siku hizo staili yao ilikuwa imerudia tu tena KIMISHENARI kwa kuwa wameshachoka majaribio.:-(
NALIKATIZIA HILI WAZO HAPA!:-(

Swali:
  • Wewe unauhakika sio MHESHIMIWA ndio maana kuongelea URODA unaona aibu na kisingizio ni kwamba sio UTAMADUNI na MILA zetu kuongelea au hata kuwafundisha taifa la kesho jinsi ya kula ngoma?
  • Hivi MHESHIMIWA MWENYE WATOTO si maana yake kasha hakikishia UMATI ashawahi KUNANIHII?
  • Hivi unauhakika ni kwanini KUNA WAONGEAO Kiswahili waitao NGONO chakula cha usiku au kulalamika MPAKA KWA BABA MKWE - eti BABA watoto sikuhizi hali nyumbani wakati walalamikiacho hata ukipambe vipi ni kilekile?
  • Hivi ni kweli unajiheshimu au tu wafanya uhisivyo hatuviheshimu KAMA NASI TUFANYAVYO kwa siri ili wote tuwe WAHESHIMIWA kinafiki?
  • Unafikiri ukimya wa MHESHIMIWA mwenye ujuzi awezaye kufunza ni HESHIMA hata kama unadhani kuna ustaarabu kwa hilo?


NAACHA na hili ni WAZO TU Mheshimiwa, USIKONDE!



Hebu FUNKSTAR DE LUXE wabadili kwa- SUN IS SHINING

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP