Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UHAKIKA - kwa aliyewahi kuwa BIKIRA!

>> Thursday, November 12, 2009

Maswala ya kuwa na uhakika NA KUJUA alikuwa na BIKIRA,...
....kuna ambaye UHAKIKA ni mpaka astukie MAUMIVU kwakuwa alisimuliwa atasikia MAUMIVU au atatokwa damu wakati anatolewa BIKIRA ndio awe na UHAKIKA.:-(



Kwa bahati MBAYA uhakika LABDA unahitaji UHISI KITU KWANZA kwa kuwa hata sasa hivi kama hujui KUNA KITU labda huwezi kustukia kuna kitu na ukistukia unaweza usiwe na UHAKIKA.:-(

Na hata KATIKA SWALA LA kuwa kila hewa avutayo mtu KWA KAWAIDA inavijidudu na VIPATIKO a.k.a chembechembe maridhawa, UNAWEZA usistukie mpaka upate swine flu kuwa - kama tu wakati wowote ulivyo kuwa ni wakati wa CHAI,- basi na kila wakati KUNA KITU hata kama tu ni JINSI ya KUBANA PUA KWA MARA YA KWANZA BILA KUMUUDHI MPENZI kwa sababu KWA MARA YA KWANZA umenusa kwa bahati mbaya chupi CHAFU ya mpenzi na INANUKA , - kwa hilo unatolewa BIKIRA ,....
.....na kwa kuwa vingi utolewavyo bikira kwako si muhimu NA HUVISTUKII , labda ndio maana huhitaji UHAKIKA.

NALIKATIZA WAZO HILI MSHENZI HAPA!
Swali:
  • Unauhakika hauna bikira ya KIPINDUPINDU?
  • Kwani unafikiri ni kweli KWA SIMULIZI kuna ajuae UBAGUZI kabla ya kwa vitendo MTU KUBAGULIWA na kustukia ANABAGULIWA na KWA hilo kwa maumivu ANAUHAKIKA?
  • Si unajua KUBAGULIWA ni mpaka ustukie UNABAGULIWA?

KUMBUKA ni wazo tu HILI na halina UTUKUFU na pia wala HALINA uhusiano na sehemu za siri MHESHIMIWA!

Basi ngojea twende Bongo Kilimanjaro Band walete-CHI NYAMANYAMA HICHO



Au tu MCHINGA SOUND wazungumzie-Kichwa cha PANZI

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Faith S Hilary 3:50 am  

Ngoja nikafikirie bikira nilizonazo then maybe nitarudi na bonge la list...au...nothing

Yasinta Ngonyani 12:45 pm  

nimefurahi kusikiliza kichwa cha panzi:-) halafu Tanzania nchi yangu nakupenda sana nchi niliyozaliwa nimekumbuka sana nyumbani usegwili bambu:-)

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! 12:50 pm  

Pole Yasinta. Karibu kwa njia ya tamaa...lol

Eti, Mt Somoni akina kaka nao wanakuwaga na bikira?...lol

Simon Kitururu 6:39 am  

@Candy1: :-)
@Da Yasinta: :-)
@Kadinali CHACHA aka Ng'wanambiti:

:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP