Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kuna uwezekano ugumu wa MAISHA huongezeka kutokana na MIPANGO YAKO TU!:-(

>> Monday, November 23, 2009

Busara za mipango ya KUKU wa kienyeji kikubwa ni kukumbuka tu jioni kurudi BANDANI.

Binadamu na busara zake za kupanga MIPANGO mingi ya kurahisisha maisha aweza kujikuta mpaka kafanya MAISHA MAGUMU yazidi UGUMU ZAIDI kwa hata kufikia kufikiria anahitaji NYUMBA wakati yote yalio muhimu yake angeweza kuishinayo TU kwa raha KIBANDANI.:-(

Swali:
  • Hujawahi kukutana na atakaye gari wakati baiskeli yake inatosha kwendea kigengeni kumvizia muuza nyanya?
  • Unafikiri kimaisha Binadamu anamzidi Kuku busara?


NI WAZO TU HILI MKUU na usikonde!

Hebu Lenny Henry adai-BEcause I am Black


Alpha Blondy ngojea abadili kwa -I wish U were here

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 3:41 pm  

Natamani ningekuwa kuku:-)
Na ahsante kwa huu wimbo wa "I wish u were here"

nyahbingi worrior. 6:05 pm  

kama ilivosema unaweza kufanya yote kibandani lakini huoni bado wengi wakubatia ughaibuni?huoni wengi wanadai kibandani ni ugenini?

nufff nuff respect man.

Sellassi.

Fadhy Mtanga 6:38 pm  

Sana tu mkuu. Daima sichoki kusoma falsafa za Mtakatifu Simon.

Simon Kitururu 1:24 pm  

@Da Yasinta: :-)
@Nyahbingi Worrior: Kuna ukweli katika usemacho:-(

@Askofu Fadhy: Nashukuru Mkuu kwa kutonichoka hapa !

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP