Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kawaida WANYONGE wakimshindwa MTEMI hubwengana WENYEWE kwa wenyewe!

>> Friday, November 27, 2009

Narudia tararila:

''Kwa kawaida JEMADARI ANDUNJE hugombana na ANDUNJE mwenziye ndio maana ni rahisi kwa WATANZANIA kugombana na WAKENYA kuliko kuzua ugomvi na UINGEREZA.
Au nikilainisha zaidi kachori naweza kusema:


''Katika TANZANIA ni rahisi kwa vyama vya upinzani kupigana vita vyenyewe kwa vyenyewe na kuiacha CCM shwari kwa kushindwa tu gia za kuivaragiza CCM au kwa kufikiri TU kuwa CCM ni maji mazito a.k.a katika maswala ya kung'ang'ania kidude ni MTEMI.'':-(


Au namaanisha:

'''Ndio maana SOUTH AFRICA ni rahisi kwa WASAUZI WEUSI kuwabwenga WAAFRIKA WENZAO KUTOKA NCHI NYINGINE kuliko kuwabwenga wasio waafrika ambao nao ni wageni South Africa kama ulivyoshuhudia walivyofanya tayari.''

Naweza pia kusema na maana:

''Ndio maana toto temi lililokuwa linakubwenga makonzi CHEKECHEA lilikuwa zaizi YAKO na hadi lile lililokuwa linakuonea HIGH SCHOOL ukifikiria utastukia lilikuwa halifuati wakubwa kuliko yeye''.:-(

Pia:

''Tukienda PAKISTANI utakuta vita imegeuka kuwa ni Wao (Wapakistani matalinbani] kwa WAO (Wapakistani -serikali]na MTEMI wanamuacha kakaa pembeni.''

Pia :
''Iraki Waislamu(SHIA] kwa Waislamu[SUNNI] wanabwengana na mtemi wamuachaye simtaji.'':-(


Swali:
  • Umenielewa MKUU kwa kusema kuwa TEMI huachwa na wanyonge hata majalalani ni rahisi kwao kubwengana wao kwa wao?



Kumbuka hili ni WAZO TU MKUU na kulibishia RUKSA !
Na nakutakia mafanikio MEMA hata kama nia yako ni kwenda kusaka DOGODOGO saizi yako !




Sasa ngojea tupate shule TISHATISHA-Genetic Link in Black Aids Epidemic?




Au tu BOB MARLEY apeleke reggea maeneo katika -Reggae on the Broadway

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP