Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

NARUDIA ! - Kila MTU anatumia kichwa ingawa kuna ambao KICHWA kinawashauri ujanja kwao ILI WAKUZIDI wanahitaji pia tumizi la TAKO!

>> Friday, November 20, 2009

Matumizi ya kichwa yanaweza kukufanya UDHANI KUNA watumiao zaidi kichwa kuliko wengine.

Lakini kumbuka kuwa ni matumizi ya kichwa yafanyayo wengine wanatumia zaidi tako au KUREMBUA kama wamestukia BAADA YA KUTUMIA KICHWA kuwa katika SHUGHULI ni tako tu na KUREMBUA TU ndicho hata jichoni kwa BOSI na WAHUSIKA WALENGWA ndicho wawazidicho watumiao kichwa WENGINE.:-(

Tumizi la kichwa kama wajijua UNAMIAKILI hukupa mtazamo tofauti wa jinsi ya kutatua mambo kama ukilifanananisha na TUMIZI LA KICHWA LAMTU AMBAYE wakati kila akijichanganya hata katika mijadala ya ''HIVI JIRANI KALA NINI'' au tu kwa nini siku hizi JIRANI anatembea kama ANA BUSHA, anahisi NA KUSTUKIA hata kwa hilo KWA KAWAIDA wajuao kiundani kuwa ni kwa sababu JAMAA limetahiriwa hivi karibuni ukubwani kwa ombi la MCHUMBA ni WENGINE:-(

Swali:
  • Si unajua hata katika UMBEA kama TUMIZI LA KICHWA , kuna PROFESA WAKE mtaani?

KWA HIYO,....
.... labda ni MATUMIZI YA KICHWA ambayo ni bomba la tumizi la AKILI lifanyalo wengine KUONJWA KIDOGO NA BOSI ili kukuzidi mshahara kwa kuwa ni tumizi lao la kichwa lililowastua kustukia kuwa wakishindana nawe KWA KUJUA watatoka kapa kwa jinsi UJUAVYO MENGI -kitu kifanyacho unasifiwa KWA MIAKILI,- lakini wakitingisha tako na kwa adoado bosi akionja BILA KUSAA ile staili ya kukaa vibaya uone chupi ya maua ,....

....kwenye ziara za bosi au hata Rais Kikwete UGHAIBUNI watakuwepo, bonasi za semina za mambo yasiyo wahusu watazipata , kukuzidi cheo watakuzidi na usipoangalia wasipojua wafanyacho WANAUHAKIKA WAKIJA KUKUREMBULIA MACHO WEWE MWENYEWE bila kusahau na kuongezea CHACHANDU ya kukutingishia tako ukodolee VIBASTOLA a.k.a VIPISTO kama upendavyo hukuukifikiria ile chupi ya maua uliyoiona jana WAKATIA UNAANDALIWA KUINGIZWA MKENGE , utawafanyiakazi WASIZOZIJUA na juu yake utaofa mpaka LANCHI ingawa umezidiwa mshahara kwa angalau tu kuneemesha tumaini kuwa LABDA kunachazaidi utaonjeshwa,....
....
- NA AMINI USIAMINI hiyo ni aina ya kutumia KICHWA kwa wengine.:-(

Swali:

  • Si unajua si kila mtu mwenye akili uwezo wake wa kutumia kichwa ni lazima ajue SAYANSI?
  • Na siunajua KWA KUTUMIA KICHWA kuna ambao maana nzima ya maisha iwafanyayo wawena msukumo wa kuamka kila siku na kujisukuma kufanya kazi ni ili wajiwezeshe kutumia cha chini kichwa?
  • Unauhakika matumizi ya kichwa sio ndiye ibilisi mwenyewe a.k.a SHETANI ?
  • Katika matumizi ya kichwa si umeshawahi kushuhudia Profesa maskini ?

NIMEACHA wazo!

Hebu twende Kenya usikilize yaliyomkuta FRESHLY MWAMBURI aongelee matumizi ya kichwa ya Stella katika ndude iitwayo -STELLA WANGU

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 12:06 pm  

Mt. Simon nimefurahi kwa kurudi kwako maana ulipotea kidogo:-) nitarudi kwenye mada baadaye natafakari kwanza.

Simon Kitururu 8:43 am  

@Dada Yasinta: Asante sana kwa kutoacha kunitembelea!Nakupenda!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP