Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Tofauti ya tamaduni za Tanzania NA Finland kwa kutumia VIELELEZO vya zaidi ya akina nani zaidi wana MAGOVI!

>> Wednesday, November 04, 2009

[Tahadhari: Nia na madhumuni ya taralira hii ni kugusia kidogo vijambozi kwa staili ya kukuna TAMADUNI kinamna katika MFANANISHO wa BONGO na FINLAND!]





Ukitoka TANZANIA ukajikuta uko FINLAND ambako govi ni TUKUFU, unaweza kushangaa ukichekwa kisa mtu kastukia dume zima UMETAHIRIWA hasa ikiwa wewe ndiye ulikuwa bingwa wakucheka wenye MAGOVI !


Samahani NAANZA UPYA hii TARALIRA na safari hii kiheshima......


Utamaduni ni kitu cha ajabu sana!
Na moja ya njia NZURI ya mtu kujifunza kuhusu utamaduni wako ni kuishi katika utamaduni wa watu WENGINE.

Kuna mambo ambayo katika utamaduni wako AMBAYO yanakuumiza kichwa, yanaweza kukusumbua mpaka ustukie watu wengine waishivyo bila kuhitaji uaminicho NI MUHIMU kwenye utamaduni wako ndipo utakapo gundua kuna mengi ni muhimu kwako kutokana tu na staili yako ya KUFIKIRIA na wala LABDA si kweli hata MAMA MKWE akikuvulia lichupi kwa hasira UTALAANIKA kwa kuwa unashuhudia JAMII ambayo watoto hawapofuki kwa kuona vipengele vya wakubwa na HAWANA KIITWACHO KULAANI katika tamaduni na staili ya kufikiria.

Na haki ya nani ni mtazamo tu NA JINSI YA KUFIKIRIA usababishao GUINEA PAPUA kibuyu kwenye kikojoleo cha mwanaume IWE ni chupi tosha, na kwa akinadada BICHI BRAZIL iwe ni vikamba tu vimefunika kidude huku tako liko nje ionekane KIMWANA KATOKA, wakati wewe chupi lako BONGE na linafanyakazi kwa ufanisi utafikiri lina iga NEPI, halafu wajanja wanakucheka na mpenzi anakuona wakuja.:-(

Tupumzike kwa kuangalia jinsi ufikiriavyo kwa utamaduni wako wa asili na mpaka wa kuiga uwezavyo mpaka kukuchagulia aina ya chupi kama ifuatavyo:


Chupi yetu ya asili/Kitamaduni.

Mimi niko hapo kwa nyuma ukiangalia vizuri pichani.

Hii chupi inamanufaa sana na naamini kama wewe unahusudu mambo ya chapuchapu unanielewa.












Chupi ya dada afikiriaye au ajijuaye ni bingwa wa kuchamba vizuri na atakudaka ukimchungulia au tu kufarijika kwa- ua zuri lapendeza - kabla hujaendeleza dhambi.

[Tubu Mkuu LAKINI kama umeingia majaribu ya dhambi ya kiuasherati !]
















HILI ni Bonge la chupi lifanyalo tu kazi VIZURI SANA kama itegemewayo kufanyika na chupi.












Swali:
  • Bado hujastukia jinsi utamaduni na afikiriavyo mtu kunavyo mchagulia aina ya utamaduni wa CHUPI?


NGOJEA TURUDI kwenye hoja ya taralila ambayo ni FINLAND vs TANZANIA kiutamaduni...

Kama Mtanzania unaweza kushangaa sana baadhi ya mambo ukikatiza mitaa ya Ulaya Kaskazini kama vile :
  • Maswala ya fikira za UCHI
  • Mahusiano ya Mtu na Mtu
  • Dini
  • Msosi
  • Ufanyaji KAZI
  • Nk.
UCHI

Ndio , kama umetokea katika jamii kama ya Tanzania unaweza ukatishika siku ukikaribishwa SAUNA na familia nzima ya watu - Kuanzia BIBI mpaka wajukuu zake ambao wote wako UCHI.

Au tu unaweza kushtushwa ukistukia umekwenda kwa mtu halafu ukakuta ni Baba na Binti yake wanatoka uchi kwenye SAUNA ili kwenda kujidumbukiza ZIWANI kupoza joto la sauna huku wakiwa FULU kuchekelea. Hapa kama MTIZED unaweza kujikuta unaanza kufikiria labda JOGOO ninaonja kifaranga chake ,wakati wahusika waongeayo na kufikiria wala hayagusi sehemu za KUJIGIDANIA kimwili. Yani wako fulu Baba na Mwana na swala ni sauna na si kingine.
Kwa kifupi WAFINI na WATANZANIA katika swala la kukaa uchi na tuwafikiriavyo waliouchi kunatofauti kubwa. Na kwa kawaida UFINI ni TITI KUBWA ndio kidaka BUZI na sio tako kubwa kama liwapalo MACHUNA BUZI wa BONGO ndoano.
Na govi ni TUKUFU mitaa ya FINLAND, na kama dume zima limetahiriwa basi ujue ni YAHUDI au ISLAMU kitu ambacho kwa nchi kama FINLAND asilimiani zero nukta ziro zero sifuri tano au kitu kama hicho, ndio ujazo wa Mtu hizi zenye mila ziaminizo katika kukatajando zilivyo kiidadi.

Kwa hiyo usishangae ukijichanganya DUME ZIMA kwenye MASAUNA , watu wakawa wanaacha kushangalia nyonyo ya mdada aliyekaa pembeni yako waliyoizoea kuiona na kuikodolea pembejeo yako iliyonolewa, na labda ILINOLEWA kwa sababu usizozijua.Ndio, wanaweza kukuchungulia pia kuhakikisha kama kweli watu weusi wanabaraka za punda kwa ukubwa wa pembejeo za uasherati.:-(

Swali:
  • SI unakumbuka katika ngoma zetu kibao Bongo ilikuwa kawaida akinadada kucheza nyonyo nje na kwa watazamaji kucheki nyonyo ya mkatika kiuno mambo yalikuwa si fulu kuyatamani kimfadhaiko?
Mtu na MTU

Kama umezoea kusalimia kila mtu unaweza kujisikia vibaya!

Mtu anaweza kustuka kama vile umemtukana kwa kusikia salamu yako , na kama YEYE bado ni mstaarabu badala ya kukujibu anaweza akakuulia'' DO I know U?''.

Kwa kifupi FINLAND kila mtu kivyake na ingawa watu hudai kuwa karibu nchi zote za magharibi ziko hivyo, kwa uzoefu wangu binafsi wa nchi kadhaa wa kadhaa ,NCHI nyingine za MAGHARIBI hazijafikia FINLAND hasa kwa sababu WAFINI ni wakimya na hawana porojo a.k.a small talk katika tamaduni yao.Wao ni watu wakuchuna zaidi a.k.a no non sense kwa wasiyemjua.

Na kingine ni kwamba FINLAND ni moja ya nchi ambayo mfumo wake WA SERIKALI unafanyakazi haswa na karibu kila kitu serikali inafanya ikibidi. Na maanisha, ikibidi serikali INAINGILIA MPAKA FAMILIA YAKO - itamsomesha mtoto wako mpaka Chuo Kikuu tokea ikunyang'anye kwa kuwa TU ulimfinya akapigia simu wahusika umemfinya. Na kutokana na Serikali ilivyokuwa inafanyakazi ipaswavyo imefikia mpaka hata mtoto wako hakuhitaji sana kama Bongo na huwezi kumtisha mtu kwa lolote kwa kuwa kama yeye ni Mfini basi Nyumba hawezi kukosa na anauhakika kuwa hafi na njaa. Kirahisi kuanzia asiye na kazi na Mkurugezi wa Kampuni kila jioni unaweza kuwakuta baa moja na kila mmoja anakunywa kwa starehe yake bila kuomba ofa wala kutishwa na mwenye hela katika maswala ya kipooza koo kabla ya kwenda nyumbani.
Kwa kifupi uhusiano wa mtu na mtu ni tofauti FINLAND ukilinganisha na TANZANIA au tu NCHI kama UINGEREZA na akuitaye rafiki kama ni Mfini mara karibu zote huyo ni rafiki kweli na sio porojo kwa kuwa mpaka kuzoeana naye kwenyewe mkizoeana basi kazi ilikuwapo hasa kwa kuwa MTU HIZI hazina sana porojo.

Dini
Finland inasemekana ni nchi ya KIKRISTO na kanisa kuu ni la KILUTHERI ingawa waendao kanisani wanahesabika.
Kutatua hilo swala la mahudhurio , FINLAND inawatoza sadaka Wafini kutoka kwenye mishahara yao. Yani inamaana ukipata mshahara wanakata sadaka huko huko , kwa hiyo uende au usiende kanisani weye sadaka umetoa.
Unaruhusiwa lakini kujitoa katika KANISA , na kama ujuavyo kuna wale wasio wakristo pia kama Wayahudi, Waislamu, ...nk. Ila kasheshe inayojitokeza ni kwamba karibu maeneo yote ya makaburi humilikiwa na makanisa, kwa hiyo kama unampango wa kufia FINLAND si jambo la busara kujitoa kanisani iliwasiilambe sadaka yako kwa kuwa watakudaka ukifa kwa kuwa kama sio memba wa kanisa kaburi sio bure kwako.

Na kama kawaida WAZEE ndio fulu kujichanganya MAKANISANI na sababu nadhani unajua!
Na FINLAND unaweza kutukania MUNGU kirahisi bila watu kupandisha jazba wala kukuona waajabu. Naamini DINI na aidia nzima ya MBINGUNI na JEHANAMU havina sana nguvu kama BONGO Tandale au kule Matombo.

CHAKULA
Kwa kawaida kama umezoea bonge la UGALI utashinda na njaa.

Na mapishi ya Kifini kibao si yakutumia viungo sana kwa hiyo kirahisi unaweza usilisikie supu kama umezoea angalau pilipili na binzari kwa mbali , bila kusahau kitunguu swaumu. Kwa kifupi kiungo kikubwa ni mate yako a.k.a ladha ya kutokuungwa.

Kirahisi menu ya kifini ina:

Viazi ulaya, Mikate, Sausage/Makkara, Majani majani kwa mbali,Mtakatifu Nguruwe kwa sana, Samaki- unajua tena wana maziwa elfu kibao, Kwa kifupi mchanganyiko wa vyakula hivyo nilivyovitaja huliwa tu kutegemea na ni nini kinaendelea.... Soseji huenda sana na Ketchup na Mustard hasa iitwayo Turun Sinappi Chakula cha wanafunzi kilichozoeleka ni -Sandwich Ingawa chakula cha wanafunzi kutoka bongo kilicho zoeleka zaidi ni -Kuku kutokana na bei Pombe Wafini wanapandisha sana . Kinywaji wanywacho sana ni Koskenkorva kwa sana, Bia, kila kilevi, Wine lakini hainywewi kama wanywavyo Wafaransa.Wafini kwa asilimia kubwa kinywaji wakinywavyo ni fulu kubugia na si mambo ya adoado.



KUFANYA KAZI!

Hawa jamaa ni wafanya kazi sana! Yani wakienda kulewa ni fulu kunywa pombe lakini wakirudi kazini ni KAZI na kahawa sana.Na ukizoea ufanyaji kazi wao ukirudi bongo lazima udhani BONGO watu wanafanyakazi katika SLOW MOTION.

Halafu ni ma- perfectionist. Kwa hiyo hata siku moja usiamini Mfini akikuambia hajui Kingereza, Kifaransa, Kijerumani kwa kuwa hata aongeaye hizo lugha kukuzidi ukimuuliza anaweza kudai hajui kisa labda kama ni Kingereza anaamini asiposaundi kama Queen Elizabeth basi yeye bado Kiingereza hajui. Na kama unaingia kwa gia za kisanii, kumbuka karibu asilimia themanini ya Wafini kuna chombo cha mziki wanakipiga na kujua kukisoma kimziki ingawa hawajiiti wanamziki kwa kuwa wanafanya shughuli nyingine na wanaona aibu kwa kutojiamini kuwa wanabwenga chombo. Kwa kifupi ukiingia kichwa kichwa unaweza kutoka nishai kwa kukutana na mtu ambaye anaweza akakufundisha mambo ya Bongo ambayo wewe mwenyewe huyajui.





NAACHIA HAPA MKUBWA na natumaini unakumbuka GOOGLE ipo ukitaka kuelewa mpaka Wafini wanapendelea Chupi za aina gani!

BAADAYE MHESHIMIWA!


Ngojea nimuachie mwanadada KOFI ajivunie weusi kitu ambacho nahisi Wazungu wakijivunia Uzungu inaweza kuitwa ni ubaguzi katika-BLACK PRIDE

Au tu ni muachie naye mvulana Vivian Jones alete kitu-Good Morning

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Faith S Hilary 5:45 pm  

Well it was a LOT of reading but I managed lol! ila mimi bado sielewi watu wengine wakisema "utamaduni wa mtanzania" iwapo mtu kavaa something like a bikini na kusema sio utamaduni wetu. Mimi sijui utamaduni kwa kiTanzania ukoje ikija kwenye mavazi, kwamba women have to cover themselves all the time? Anyway nimependa hii Finland and Tanzania..tho stil sielewi what "people" "say"

Simon Kitururu 7:12 pm  

@Candy1: Tanzania yenyewe si ndio hiyo imezaliwa juzijuzi na mpaka sasa Muungano wenyewe na Zanzibar ukiniuliza mie hata sina uhakika tunako endelea. Kwa hiyo labda kama hata Tanzania kama nchi haina uhakika si ajabu kwa Watanzania kutokuwa na uhakika na nini ni Utamaduni wa Mtanzania.


Ila nawasiwasi kama bikini ni utamaduni wa Tanzania kwa kuwa bikini ni vazi ambalo kirahisi unaweza kufuatilia history yake na mpaka lini hata nchi za Magharibi zilipoanza kuziona ni za kawaida baada ya Movie za Holywood.

malkiory 7:39 pm  

Mkuu hongera sana kwa kulichambua na kulichanganua hii mada nzuri sana kuhusu tamaduni za Kifini na Tanzania. Utadhani umeishi Ufini takribani miaka 20 hivi.

Simon Kitururu 2:05 am  

@Mkuu Malkiory: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP