Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

HAPPY BIRTHDAY MALAYA WANGU!

>> Friday, November 20, 2009

[Tahadhari: hii ni barua ya Mheshimiwa MUME WA MTU!]



Kwa Mpenzi KIMADA!

Leo ni siku ya KUZALIWA KWAKO MPENZI na nakutakia MAISHA MAREFU na mafanikio katika yote uyapangayo mbeleni malaya wangu.

Samahani nitashindwa kuhudhuria sherehe yako,unajua tena nahisi MKE WANGU kashaanza kustukia kitu ,...
....na PILI unajua tena bado nashindwa kumuambia rafikiyo ambaye ndiye alisababisha tukutane ambaye naye kama ujuavyo ni malaya wangu pia BADO na nahisi atakuwepo kwenye pati yako.:-(

DUH !
  • Unafikiri wikiendi iliyopita kwenye pati ya rafikiyo , RAFIKI YAKO alistukia kitu kuhusu mimi na wewe ?

Kwa maana ilikuwa kazi kweli kujifanya kuwa bado sijakuzoea ,- na ilikuwa kazi kujizuia kukodolea vibastola vyako vipya , na tako jipya nililokununulia kwa WACHINA kwa kuwa sikutaka mgombane ,...
.....- Unajua tena MALAYA WANGU NI rafikiyo, tena halafu yeye sijamnunulia bado dawa zakukuza tako kama wewe, kwa kuwa ulinikataza!:-( ...


.......Ila mpenzi ama kweli unapendeza na GOBOLE ZAKO MPYA na naahidi tutaenda hivi karibuni kufanya shopingi mpya za chupi ZAKO mpya kama ulivyoomba kwa kuwa unajua tena SHEHENA YAKO YA NYUMA IMEKUA kweli mpaka hata kipofu aweza hilo kushuhudia kwa maana mtoto kalio sasa hivi FULU MTUTUMUKO na hata ukikaa sakafuni unanesanesa.LOL!

Kwa mara nyingine samahani nitashindwa kuhudhuria TENA kwa mara nyingine BIRTHDAY YAKO MPENZI kama mwaka jana na mwaka juzi ,- lakini hili swala la ndoa yangu INIZUIAYO KUSEREBUKA NAWE kwenye besidei zako HII kumbuka NI kama nilivyokuahidi, ni jambo la TEMPORARY tu .

Na mpenzi nakuhakikishia kuwa wewe ni mtamu kweli kuliko mke wangu, binamu yako na rafikiyo ukiwajumlisha , na sidanganyi ntakujengea nyumba mambo yakitulia maana unajua tena siku hizi kazini wachawi wengi kwa hiyo naangalia sana watu wasije wakaniharibia ulaji. - unajua tena wachawi wengi siku hizi na nahisi ulishuhudia mwenyewe wale jamaa wa ofisini tulio kutananao Bagamoyo tukivinjari ambao NILIOKUTAMBULISHA wakiwawanashangaa kuniona KULE nikivinjari NAWE kwa kuwa wao kule ni shughuli za waganga tu wazifuatazo kule.

Tukiachana na hilo; - mpenzi mwenzio nashindwa hata nifanyeje kwa jinsi navyokuwaza.
Naahidi kama nilivyoahidi mwaka jana na mwaka juzi ; ''NIVUMILIE tu nantamuacha tu MKE wangu kama nilivyo kuahidi mwaka juzi na pia nta muacha pia MALAYA wangu mwingine ambaye ni rafikiyo na haki ya nani KUMBUKA ni kweli hata wakinipa msosi WA KIKUBWA nilie chini huwa kelele zote ni jina lako. :-(

Unajua tena nakupenda zaidi wewe MWANAKWETU halafu unajua wewe na mimi ni kabila moja kwa hiyo tukinogewa tunaweza hata kunena kwa lugha.Lol!

Mpenzi pokea basi Ki RAV4 kwa sasa kama zawadi ya BIRTHDAY na sherehekea vyema malaya wangu BIRTHDAY YAKO mnono hawala.

Wako,
Mme wa MTU a.k.a UMCHUNAYE BUZI.



P.S :Usigawe kwenye PATI mwenzio na WIVU, na usimwambie mtu kuwa ni mimi niliyekununulia Ki-RAV4!:-(
MWAAh!



Swali:

  • Hivi ni kawaida yako weye msomaji kusoma barua za watu?LIONE VILE!
  • Unafikiri SINARIO HII haiendelei sasa hivi kwa watu fulani mahali fulani Bongo nyoso/Tanzania?
  • Unafikiri mke na kimada nani kwa kawaida hupewa zawadi au huandikiwa barua tamu zaidi?
  • Unajua hasa ni tofauti gani itofautishayo tofauti ya umuandikiavyo ndugu mpenzi na limpenzi tu ikiwa kiongelewacho katika barua zote ni chuki kwa kuwa wamekuchukiza?

NAACHA WAZO na haki ya nani sina uhakika kama kunafundisho au kwa nini nimeandika TARARILA HII!
IJUMAA na WIKIENDI NJEMA MHESHIMIWA!


Ngojea LES MANGELEPA wabadili hali ya hewa na kuleta BUSARA kwa kitu -NYAKO KONYA


Au tu Ochestra Super Mazembe walete tena kitu-SHAURI YAKO

7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

shamim a.k.a Zeze 2:33 pm  

hahahahaah nimekusoma mtakatifuuu...nimeipenda iyo FULU SUTI jamaa alomnunulie...LIONE VILE..wink

nilikatiza maeneo

Fadhy Mtanga 3:16 pm  

Mkuu, siku zote huwa nanogewa na tararila zako, lakini leo imefunika zote. Niseme nini tena Askofu miye?

Simon Kitururu 3:39 pm  

@Shamim + Askofu Fadhy: :-)

chib 4:35 pm  

Sijacheka siku nyingi kama nilivyofanya leo.
Sijaamua kutafsiri utakatifu wako ha ha haaaa

Anonymous 9:21 pm  

ROTFL :D

malkiory 7:39 pm  

Mtakatifu Simon Kitururu, kwa haraka haraka ukiisoma hii article unaweza dhania ni mzaha lakini kumbe imebeba ujumbe mzito. Kama ilivyokawaida ya binadamu huwa hupenda kujaribu mambo mapya, lakini pengine ni tabia ya mtu tu. Nyumba ndogooooo......!!!!!!!!!!!

Simon Kitururu 9:08 am  

@Mkuu CHIB, Mkuu MALKIORY na MSHAIRI mpenzi SERINA : :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP