Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Binadamu huhitaji kitu kimoja tu awe MAARUFU au KUFANYA BINADAMU WENGINE wamuone WAMAANA au mjinga kwa mbaaali!:-(

>> Friday, November 20, 2009

Kumbuka wote uwajuao au kuwasikia kwa kufanikiwa au tu MIAKILI hata kama walifanya mambo ELFU ,....

... sifazao zifanyazo uwajue/KUWASIKIA/ au hata kuwazimia mara nyingi ziko kwenye kitu KIMOJA TU walichowahifanya.

Na utaahira wa TAAHIRA wa binadamu adhaniwaye ni taahira au ana kichaa na MAELFU,...
.... hugeuzwa tafsiri na MAMILIONI mara moja TU NA kuwa ni AKILI NYINGI ndio maana KIJEBA HAELEWEKI , akigundua kitu kimoja tu ambacho wenye akili kwa akili zao WALISHINDWA KUFANYA:-(

Na kwa bahati mbaya UKUBWA wa kitu kimoja HAUNA KIPIMO maalumu au kipimo kimoja MAARUFU ,...


... kwa kuwa KIMFANYACHO MTU AWE MAARUFU inaweza tu ikawa ni -Goli moja tu lililomfanya mtu awe BABA ya Obama na kuwa maarufu kwa hilo au Goli MOJA lililo sababisha Yanga imfunge SIMBA na kumfanya mtu aonekane muhimu kwa washabiki wa Yanga kwa hilo, uvumbuzi mmoja kama tu ambao ulianzisha EINSTEIN ajulikane DUNIA NZIMA kwa miakili hivyo au hata malezi ya wazazi wako KWA STAILI MOJA tu isababishayo WOTE TUDHANIE wazazi wa Venus WILLIAMS na Serena ni kiboko kwa kuwa wamelea mabinti WAKAWEZA kupiga kimpira kinachodundadunda na KUSABABISHA WATU WAWAZIMIE KULIKO aliyegundua CHLOROKWINI ingawa labda walitumia zaidi muda kuwafunda MENGI zaidi ambayo hatuyaoni ambayo ndio siri halisi ya mafanikio yao ingawa hutuoni wakiyafanya.:-(


Ndio ,...
.... chaajabu LABDA PIA ni kitu kimoja tu inahitajika USIJUE ili kukufanya UWE MAARUFU tusahau UNAJUA KWELI HESABU na ni KUTOONGEA VIZURI tu ndio kunafanya DUNIA NZIMA tuamini wewe ni RAIS GEORGE BUSH wa akili wastani wakati labda weye JINIASI na UNABOMBA LA MIAKILI tu kwa tusichoshuhudia UKIFANYA.:-(

Swali:
  • Si unakumbuka ni umaarufu wa kitu kimoja TU KIBAYA kwa mtu mmoja unaweza kusahaulisha watu kuwa kwa mengi wewe ni BONGE LA MTU MZURI kwa wengi?
  • Unafikiri tabia za binadamu za KWA KAWAIDA KUZIMIA mtu kwa kitu kimoja tu na kumuona Bonge la David Beckham kwa kila kitu INGAWA AJUACHO AFANYACHO DAVID BECKHAM NI KIMOJA ni mjanja ,wakati dunia yenyewe ina mengi na YAHITAJI MENGI na katika hayo yote labda la David Beckham NDILO si la muhimu na ni la kisenge kwa asiye msenge?
  • Ukifikiria sana si unaweza kugundua mpaka kitu kimoja tu KWAKO kilichomfanya mpaka Yesu kawa bonge la Supa STAA a.k.a Bonge la maarufu/YUKO JUU?

KUMBUKA hili NI WAZO TU MHESHIMIWA!

Tuondokane na wazo kwa msaada wa dada kutoka GUINEA kwa jina ALAMA KANTE alainishe kwa ndude-DIS MOI



Au tu KEKELE na MBILIA BEL walete-Yo Odeconer

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP