Kitabu chochote unaweza kuanza kukielewa vingine kama yaliyoandikwa UNAAMINI ni NENO LA MUNGU!
>> Tuesday, November 10, 2009
Stori zipo na zimeandikwa vitabuni ,.....
........na labda vitabu vingi ungevizimia tu kama KORANI , Biblia na,....
..... kama msomaji ungeamini usomayo ni NENO LA MUNGU.
Swali:
- Kama wewe ni Mkristo si unakumbuka stori za Biblia ungezielewa tu kama uelewavyo kitabu cha JUMA na ROZA kama usingeamini BIBLIA ni Neno la MUNGU?
- Kwani hujui usingeamini BIBLIA ni NENO LA MUNGU kuna mambo kibao ungeyapinga yasisitizwayo na BIBLIA?
- Hivi kwanza unasoma Biblia kweli?
Hili ni wazo tu MKUU!
Hebu SIZZLA KALONJI adai-Really and TrullyAu tu Lady Saw na SIZZLA KALONJI warudie-Good Love
4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Mtakatifu Simon ujuwe kuna watu wasomao Biblia kama wasomavyo stori za Shigongo aka wanasoma tu lakini hawataki kuyatekeleza yaandikwayo humo kama vile waambiwapo USIZINI wakati huo huo ana miadi na mke wa rafiki yake kipenzi na wa siku nyingi kiasi kwamba jamii ikijua anammegea mkewe inaweza hata kumfukuza kijijini huku jamaa anakohamia akiendelea kusoma BIBLIA huku akikazana kumwomba Mungu awasamehe wale waliomdisi kwani hawajui walitendalo akisahau kuwa kosa ni lake yeye asomaye Bible kama kitabu cha hadithi.
Usichoke kusoma sentensi hiyo ndefu.
Amina:-)
Wimbo ule ule. Kwangu naona kama hauchoshi vile. Nazungumzia Siku ya kublogu tanzania ambayo imekaribia sana. Tusisahau kukumbushana tulikotoka na tulipo.
Amina!
@Papaa Fadhy: Si utani!:-(
@Da Yasinta: :-)
@Bwaya: Si utani!:-(
Post a Comment