Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

WIVU a.k.a NIKIKUONEA donge!

>> Friday, November 06, 2009

Nikikuonea donge,....
.... LABDA ni DALILI kuwa siridhishwi na yangu na NA SIKUJUI vizuri wewe ndio maana natamani kuwa wewe au tu kuwa na VYAKO!:-(

Ila mwenye DONGE,...
..... ukweli wenyewe si kwamba hana au ataridhishwa na YAKO.:-(

Na kama HATA vile kwenye UGALI ushuhudiavyo wafinyangao TONGE,...
.... kuna wapendezao na tonge utafikiri walizaliwa ili wasilie uma na kisu, au tu UKIWADEKU utafikiri wanaundugu vile na tonge KWA WAPENDEZAVYO NALO ingawa wanalifinyanga kwa staili tu kama YAKO.:-(


Lakini wakati unaona DONGE,...
... KIPINDI HICHO haki ya nani WEYE kunauwezekano MKUBWA unawaza ya WENGINE kuliko uliyonayo kibao ambayo ni baaab kubwa, YAKO.:-(

Swali:
  • Unakumbuka sababu kubwa ya kumuonea wivu mtu ni kutomjua vizuri huyo mtu?
  • Unakumbuka wivu WA MTU hutokana na kutoridhika tu na chake KITU huyo mtu, na cha ajabu ni kwamba KURIDHIKA kwa kawaida mtu WALA hahitaji kitu?
  • Umeridhika na yako,?
  • Hivi kuridhika ni siri ya WAPUMZIKAO au ni ile ya UZEMBE?

NI WAZO tu MHESHIMIWA Othrong'ong'o!

Hebu MOMBASA ROOTS watuletee-DISCO CHAKACHA


Aut u MOMBASA ROOTS washauri ukatike katika kibao-KATA


Au turudi BONGO NYOSO The KILIMANJARO BAND waongelee ya -KACHIRI

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP