Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kuwa BINADAMU hushabikia mpaka MPIRA!:-(

>> Thursday, November 05, 2009

Ukitaka kujua BINADAMU ni kiumbe cha ajabu sana,...
....hebu kiangalie kiumbe hiki wakati kiko BIZE kinashabikia kitu!

Swali:
  • Unauhakika ushaliangalia BINADAMU vizuri wakati lishangiliacho eti NI watu wanafukuza KIDUDE CHA MVIRINGO kinachodundadunda ?
  • Ushaangalia wakati binadamu washangiliacho ni mtu anampiga mwenzie kwa kuwa eti inaitwa NDONDI?
[Wakati unafikiria swali langu JARIBU PIA kufumba macho na utafakari jinsi hata Kunguru na Bata wanafikiria nini KUHUSU akili za binadamu wakiona binadamu wanashangilia mtu anafukuza mpira]


Tukiachana nahilo naweza sema.

USHABIKI ni aina ya UBAGUZI ,...
....ambacho ukipendacho ndicho wataka kishinde.:-(

USHABIKI ni UBINAFSI,....
..... kwa kuwa unazalisha upendeleo na ikibidi KIUSHABIKI utajipendelea.:-(

USHABIKI ni aina ya UKICHAA,....
..... angalia tu na wala huhitaji HATA kuchunguza na utakuta mpaka WATU WAZIMA wanashangilia kabisa au WAMENUNA TU kisa eti labda kuna mtu kapiga teke mpira.:-(

USHABIKI ni PENZI,....
..... wawezajikuta unashangilia udhaifu au umjuaye anakosea na UKWELI USIUKUBALI kama tu ung'ang'aniavyo kuwa WATU TU WANAMUONEA WIVU MKE WAKO na si malaya, kisa umependa.:-(

USHABIKI ni DINI,....
..... nadhani unajua kuwa DINI kama tu USHABIKI ni vitu visivyoeleweka na HUPATA UMUHIMU kwa BINADAMU kwa kuwa binadamu katika mapungufu yake anajaribu kujazia UTUPU WA MOYO katika KUFARIJIKA ,.....
......ndio kisa cha kwanini unadundwa moyo KWA KUSIKILIZA YA MUNGU ambayo hujazia ya roho......
....NA ......

....UNADUNDWA MOYO PIA hata kwa kushabikia eti Miss Matombo ndio mzuri zaidi WAKATI HATA KAMA unajua katika uzuri wa kitu LADHA HUTOFAUTIANA jichoni mwa mtu na MTU , kwa kuwa tu kitendo hicho CHA KUSHABIKIA UJINGA nacho hata kama ni chakijinga , bado kinajazia kama DINI kwa kukuna ILE KITU ROHO INAPENDA.

DUH NAKATIZA HILI WAZO naona linaanza KUNISHINDA n'sije pitiliza bure halafu ukajikuta UMEKUWA MSHABIKI WANGU!:-(

Swali:
  • Unauhakika USHABIKI wa kitu au tu PENZI sio aina ya UKICHAA?
  • Si unajua BINADAMU ukimpa nafasi anaweza kushabikia hata mende kama hata kuku wakushabikia hawapo?
  • Umestukia labda ushabiki ni moja tu ya kitu kionyeshacho BINADAMU KUNA KITU KAPUNGUKIWA ndio maana ananogewa KUSHABIKIA KITU yote ikiwa ni katika KUJAZIA kitu tu vile maishani ambayo mara BWELELE maana zake zimejaa UTUPU?

BASI NIMEACHA na kumbuka MHESHIMIWA hili ni WAZO TU!



Tupumzike kwa kwenda U.S.A kuwaangalia Binadamu wakishangilia Mende
HAPA


Hebu tu twende na NAMIBIA tena TATE BUTI arudie kitu -EFENGE




Au tu turudi BONGO NYOSO kukutana na PROFESSOR Jay adai tena-Hapo VIPI

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 10:19 am  

ndio maana siangaliagi mpira. yaani watu 22 wanafukuza kadude kaliko jazwa hewa, si kila mmoja atafute ka-kwake na kukimbiza tu??

any way ni kudunda na ni kwa NYEGE ndno twazaliana na ni kwa lidude kuvinmba ndo taaaa

Simon Kitururu 12:08 pm  

@ Kamala: :-)

Yasinta Ngonyani 6:07 pm  

Umenikumbusha sikumoja nikiwa TZ nilikuwa mpirani na dada mmoja sasa ktk kushangalia mpira nikastukia napigwa mateke. Nia yake kubwa ilikuwa naye aupige ule mpira. Jamani, jamani!! Kazi kwelikweli.

chib 6:22 pm  

Mtu akikuita kichaa usikasirike, kwani kila binadamu ana kiwango fulani cha ukichaa. Wanasema hata ukiwa mkimya sana, basi una aina fulani ya ukichaa

Simon Kitururu 11:01 am  

@Dada Yasinta. midadi hiyo!:-)
@Mkuu CHIB: Kunawatu huwezi kuwakomvinsi kwa hilo la kuwa wana kaukichaa kwa mbaaali!:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP