Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

sababu NATAKA kweli kwenda MBINGUNI!

>> Thursday, November 26, 2009

1. Nimetishwa kuhusu ya Jehanamu!

2. Nimetishwa

3. Nimetishwa

4. Nimetishwa

5. Nimetishwa

6. Naogopa kufa, na sijui baada ya kufa bado kama nilikufa na vipele , vipele vitaendelea kuwasha au vipi!

7. Wauza ya MBINGUNI wana -AHADI kibao NONO kuhusu kwenda mbinguni na napenda VINONO.

8. Kibano kimezidi DUNIANI.:-(

9. Ulafi kwa kuwa nasikia MBINGUNI kila kitu BWELELE.

10. Vakasheni kidogo , -si unajua tena kubadili kiduchu hali ya hewa Mkuu!


Swali:
  • Wakati weye mzinzi ujuaye KUGUNA TU na kuimba na mapera hupendi, ukidai unatamani kwenda MBINGUNI unauhakika unatamani nini?
  • Unauhakika hakuna kitu kimoja tu ambacho husababisha MTUZ kibao ziamue kujitahidi KUJARIBU kwenda mbinguni zikifa?

  • Halafu nyie muaminio ya -reincarnation, au tu nyie wapagani ambao hamzimii MBINGUNI hamfikirii ni kwa sababu hamjakutana na TISHA TOTO MZURI au tu yule auzaye uzuri wa mbinguni kama chokoleti vile?YAONE VILE!
  • Unafikiri baada ya muda fulani MBINGUNI hutataka VAKASHENI kidogo duniani kwa kuchoshwa na kila siku kumsifia MUNGU?
  • Unauhakika ni kweli kimoja kikuvutiacho kuhusu MBINGUNI nikutaka kumuona MUNGU?
  • Unafikiri SISIMIZI anamuona mtu na UKUBWA WAKE WOTE, na kama unahisi hamuoni ,huhisi kuwa labda SISIMIZI hudhani WATU NI MUNGU?
HILI NI WAZO TU MKUU usikonde!


Au hebu tuwasikilize wajanja watuelezee sababu zakutaka kwenda Mbinguni katika -NATAMANI KWENDA MBINGUNI


AU tu Naughty By Nature wadai tu - Everything's Gonna Be Alright

7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 1:59 pm  

kwenda mbinguni,
unahitaji kuwa mtakatifu ili ukiwa mbinguni uimbe nyimbo kwa shangwa pia uwe malaika mungu. MMMhhhh mie natamani kuwa malaika ambaye naruka ruka kwa shngwe

Simon Kitururu 2:05 pm  

@Da Yasinta: Unauhakika Malaika wanarukaruka kwa shangwe na sio kurukaruka ndio kibarua chao?

Na siunakumbuka shangwe unaweza kuipata hata kwa kulala chali?

Yasinta Ngonyani 2:33 pm  

Mt. Simon nina salam zako:-)
Na kuhusu hilo hapo juu:-(

Mzee wa Changamoto 6:55 pm  

Hivi ulinijibu kama wewe ni Mtaka-tifu ama Mtakatifu?
Labda una "tifu" ya fujo hivyo wataka fujo
Subiri waliokutisha wasome hapa uone tisho lijalo. Nahisi tutakupoteza kwenye ulimwengu wa ku-blog maana utatishwa mpaka ushindwe ku-blog

Simon Kitururu 12:03 am  

@Da Yasinta: Ntakutafuta.
@Mzee wa Changamoto: Sikumoja tukikutana utaamini ila kila anijuaye anajua jinsi nisivyo na fujo.:-(

Walionitisha,- sidhani kama wananisoma .


Kwani unafikiri watu wanasoma Blogu zisizo za udaku?:-)

chib 3:10 pm  

mtaka-tifua ndio maana halisi ya Simon au vp.
NI KWELI... We Weka mambo ya injili tupu, blog yako inaweza kuota buibui

Simon Kitururu 3:29 pm  

@Mkuu CHIB: Limetokea tayari hilo kuna mtuz kadhaa zinadai nakufuru na hazitanitembelea tena. Kwa bahati mbaya siwajui na wala sikuwaalika kijiweni hapa ambako nilipoanza kuandika msomaji nilikuwa miye mwenyewe.

Na shangaa kuwa kijiwe watu wengine wawezavyokushindwa kustukia kuwa huwezi kumzuia mtu kufikiria kinamna fulani na hata nisipoandika haina maana sifikirii hivyo.

Ndio kisa nimerudia posti ya zamani hapo juu.:-(

SIJATISHIKA bado lakini ingawa natishwa chobisi na nahisi mmoja wapo ni ndugu yangu nahisi.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP