Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KIFIKIRIWACHO kikiandikwa!

>> Thursday, November 26, 2009

Kilichoandikwa LABDA ,...
...kinatiaaibu KILE kilichofikiriwa ndio maana UKICHAMBUA wawezakuta KATIKA wasomaji kila mtu kakielewa kivyake!


Na LABDA,...
... ukifikiria kuandika UFIKIRIACHO, -wakati wa kukiandika sio utakachokiandika ingawa UTARIDHIKA kwa kuwa kimebeba tu baadhi ya sifa za ULICHOFIKIRIA kiaina yake.:-(


Na hakuna LABDA,....
...... katika ukweli ulichofikiria ukajaribu kukiandika wasomao wengi tu hawata kuelewa kivyako kwa kuwa MTUZ zinamchezo wa kuelewa VITU kila mtu kivyake.:-(


Swali:
  • SI unajua unaweza kuandika stori ya maringo ya bata ya kutembea anajisaidia haja tukufu ya uharisho halafu kuna mtu akafikiri unamsema YEYE wakati anajijua yeye sio bata na siri yake ya kuwa aliwahi kujiharishia kidogo wakati anakaribia choo huijui?
  • SI umestukia kwa hiyo hata ujitahidi kuziandika fikira zako za busara kiaina gani kuna watakazozielewa ni PUMBAVU?
  • Unauhakika umewahi kuandika ufikiriacho na ukakidaka katika maandishi kisawasawa kiasi ukipewa nafasi huwezigeuza sentensi?
  • Unafikiri kilichoandikwa kinadaka hali halisi ya kilichofikiriwa?
NI WAZO TU!

Hebu FALLY IPUPA abadili kwa kitu- MABELE

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP