Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Watakao KUJULIKANA MAARUFU labda BADO wanachagua watakacho ujue na ikibidi, sio kuwa HUWA wananuka KIKWAPA!

>> Wednesday, November 04, 2009

Binadamu kwa kawaida huwa hataki umaarufu,....
....zaidi ya kutaka atambuliwe kwa vyake atakavyo viwe maarufu.

Na kwa sababu binadamu hana wa MALAIKA umaarufu,....
.... kumbuka kama ni mtu HATA KAMA anajulikana sana VIPI , huyo bado ukimnusa eneo ana harufu.
Swali:
  • Umeshawahi kuhesabu angalau vitu vijazavyo idadi ya mkono mmoja vimfanyavyo hata yule maarufu sana ajulikane kwa huo umaarufu?


Ndio , LABDA ni baadhi ya vitu tu vichache, kama sio KIMOJA ambavyo vimfanyavyo mtu ajulikane kuwa ni maarufu,.....
.....na kumbuka tu hakuna fomwula katika hili ndio maana hata kwa kutembea uchi, KUJIPIKILISHA, wizi , UMALAYA na sio tu UANASIASA na kabumbu viwezavyo kukufanya maarufu.
Na inatisha kwa kuwa inamaana hata wewe kama sio bado maarufu,.....
.... labda uko hatua moja tu pembeni ya kitakacho kufanya uwe maarufu ingawa cha kusikitisha labda wala WEYE hutaki UMAARUFU!:-(



NIMEACHA na hili ni WAZO TU MHESHIMIWA !
Kumbuka wazo la Mtakatifu SIMON KITURURU wala sio KORANI wala BIBLIA imlengavyo mwenye dini, kwa hiyo kulibishia RUKSA na hutaenda kwa hilo JEHANAMU ukachomwe na MUNGU apendaye watu!



Ngojea Dr Dre anipe-Lil' GHETTO boy



Au tu Dr Dre na ICE CUBE wanipe-Natural BORN Killaz{Tahadhari: lugha na stori vyote vichafu kiaina!:-(}

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

malkiory 6:56 pm  

Hivi ni kipi kinamtegemea mwenzake, unatakiwa uwe maarufu kwanza ndipo ujulikane? au kinyume chake pia ni sawa.

Simon Kitururu 7:03 pm  

@Mkuu Malkiory: Nafikiri inatakiwa ujulikane kwanza halafu ndio uwe maarufu halafu baadaya kuwa MAARUFU ndio second generation ya wakujuao inapofuati.Kwa hiyo naamini uko sawa kuwa kinyume chake pia ni sawa.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP