Waogopacho zaidi WATU a.k.a PHOBIA!
>> Sunday, November 01, 2009
Ukiniuliza mie ntakuambia moja ya kitu,....
....WATU kibao wakiogopacho KULIKO VYOTE wala hakiko katika mfumo wa Mungu, Nyoka, N'ge, BABA, Ukimwi, Sehemu za siri kubwa za lijamaa au..........
Naamini kiogopwacho sana DUNIANI kinaweza kuvumbuliwa na swali:...
''HIVI WATU WENGINE WANANIFIKIRIAJE?''
a.k.a
a.k.a
''MAONI YA WATU WENGINE''.
Kwa ung'eng'e huu uoga ukondani ya hii PHOBIA iitwayo Allodoxaphobia au Fear of opinions.
Ingawa woga huu watu wengi hawautambui na hata UKIWAULIZA utastukia wajuacho AU WASTUKIACHO TU ukidadisi kuwa wanaogopa nini, watadai LABDA ni MENDE,....
....lakini UKWELI WENYEWE mimi naamini huu uoga wa MAONI YA WENGINE ni MKUBWA kiasi kikubwa na moja ya matatizo/ATHARI zake ni kulazimisha watu wasiishi AU KUFANYA kama wao kivyao ,na kusababisha MPAKA mwenye roho mbaya kujikuta ili kutimiza afikiriayo ni MAONI YA JAMII, anasomea UDAKTARI wakati wagonjwa wenyewe hawapendi.Au tu unawezakukuta mwenye kipaji cha UFAGIZI wa JIJI anajikuta ndio NESI wako wakati anaogopa damu na harufu za dawa kisa anaogopa tu kutumia kipaji chake kwa kuwa KIMAONI YA WATU kuwa mfagizi sio poa.:-(Usipoangalia dume zima mpaka UNAWEZAKUOLEWA na dume lenzako kisa unaogopa MAONI YA JAMII UISHIYO au tu kusemwa vibaya,...
.... kama tu....
.......yawakutavyo AKINADADA WATUKUFU katika jamii ya BONGO waogopavyo kuachika katika ndoa ZIWASULUBUZO kisa woga wa MAONI ya NDUGU, Mchungaji, SHEKHE na bila kusahau MAONI YAWATISHAYO ZAIDI yaliyoko kwenye vicheko vya kipashkuna vya MASHOGA wa nyumba ya pili waendako kusukwa nywele.:-(
Kwa kifupi MAONI ni BALAA!
Unaweza kujikuta maisha yako yote KAMA UNAVYOYANG'ANG'ANIA SASA HIVI mpaka ufikiriavyo yatakayo tokea MBINGUNI au JEHANAMU ukidedi/KUFA ,....
..... yote ni MAONI YA WENGINE ,......
......au kwa asilimia uzito bonge la tani YAMEATHIRIWA NA MAONI YA WENGINE!:-(
Swali:
- Hujastukia binadamu hawaogopi Mungu KULIKO WAOGOPAVYO WATU WANAWAFIKIRIAJE ,ndio maana kila kona uiangaliayo watu ni FULU KUFANYA DHAMBI wajuazo ni dhambi chini ya mwavuli wa kudhani wafanyacho machoni mwa WENYE MAAONI NI BAAAB KUBWA, na mpaka hata wale waendao makanisani au misikitini wengi ni kwa ajili ya FULU KUJIONYESHA dini zinapanda hasa kama wako katika jamii zenye ustaarabu wa kinafiki wakujifanya KAMA NI MSTAARABU basi jifanye dini inapanda?
- Unauhakika hata nguo uliyoivaa sasa hivi hukufikia kuivaa hiyo kwa kufikiria MAONI ya wengine watu yatakaa mkao gani katika kukufikiria?
JUMAPILI NJEMA!
Mie namsikiliza 2PAC katika-I wonder if Heaven's got a Ghetto.
AU tu 2PAC aongelee tu tena ya -Dear Mama
6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Kwa ufupi, ni kwamba binadamu anamuogopa binadamu mwingine zaidi kuliko chochote. Samahani kwa wale walio okoka, wengi wao wanafanya maovu na kujificha mbele ya macho ya binadamu wenzao, lakini huyo Mungu asiyeonekana na kuaminika yupo kila mahali hawamuogopi asilani.
Kitururu ngoja nikwambie, nimepita hapa na baada ya kusoma ujumbe huu nikaishiwa kabisa la nyongeza maana umeongea yote, nikataka kukuachia maoni kwa neno moja tu, lakini nikamkumbuka yule jamaa aliyesema hapa hatutoi maoni ya kueleweka zaidi ya duuh, umenena n.k. Nikasita kidogo nakuanza kutafuta maneno mengi nikakosa, ghafla nikastuka hah! Kitururu anasema nini na mimi ninafanya, Yaani naogopa kutoa maoni kwa neno moja kisa nitaelewekaje?******* kabisa uoga huu.
Kuanzia leo nitajitahidi kuwa huru na ugonjwa huu hatari. Ubarikiwe Kitururu kwa kutushtua.
@Mkuu CHIB: Si utani ulichosema Mkuu!
@Da Mija: Si utani hili tatizo lipo sana ingawa tunalipuuzia!Na ni kweli kirahisi mtu unawezajikuta unakuwa mtumwa wa maoni ya wengine. Miye naamini ni vizuri kujifunza kutoka katika maoni ya wengine lakini si kuyaogopa kama tuyaogopavyo.
Halafu Damija na CHIB Asanteni sana kwa kunitembelea kijiweni hapa!
Usiponiona mkuu, una haki ya kunihoji kulikoni. Nikiwa na nafasi huwa napita kama tembe za maumivu, yaani kutwa mara tatu!!
Salamu tu kwa leo!
@Mkuu CHIB: Asante Mkuu!
@Serina: Salamu nimezipokea na nashukuru hujaninsahau!
Post a Comment