Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa wote WAISHIO au WAWAFAHAMUO MAPROFESA ambao hawakwenda shule!

>> Friday, October 02, 2009

[Tahadhari: Stori hii kwa kifupi imeibuliwa na kumbukumbu zangu za BABU YANGU Mzaa BABA , Babu MRINDE aliyefariki mwaka jana!:-(]


Mimi naamini kuna MAPROFESA wengi wanatutoka kila siku na kwa bahati mbaya wanafariki na taaluma, ujuzi na yote wayajuayo sasa hivi hata wakati huu unaponisoma bila wengi kustukia tunachopoteza!:-(

NGOJEA nikupe stori kifupi ya BABU yangu MRINDE tuliyemzika mwaka jana akiwa na miaka 105 ili unielewe kirahisi nachotaka kusema.:

Babu yangu MRINDE ni miongoni mwa wale watu ambao nawaita MAPROFESA ambao hawakwenda shule.

Huyu Mzee kuandika na kusoma alifundishwa na Wajerumani na wala madarasa ya kawaida hakwenda sana. Pamoja na kusoma na kuandika alifunzwa ufundi cherehani ili awe anawashonea Wajerumani nguo. Ukiachana na aliyojifunza kutoka kwa Wajerumani huyu Mzee alikuwa ni mtaalamu wa mimea na faida zake mwingine simjui afahamuye hivyo kama alivyokuwa mtaalamu yeye.

Alikuwa anauwezo wakutibu mpaka mifupa kwa dawa za mitishamba yani ukivunjika mguu huhitaji P.O.P wala nini. Akichanganya mambo wewe uliyevunjika huchukui raundi utatembea au kuutumia wako mkono. Halafu haya maswala ya magonjwa mengine yeye ilikuwa ni swala la kuingia msituni akirudi na mizizi na majani fulani unakaswende, tumbo linakuuma au tu magonjwa mengine kibao yeye alikuwa anasawazisha. Alikuwa anaijua misitu ya Upareni , mimea yake na faida zake sijui kama nani vile. Ilikuwa uugue gonjwa la ajabu kabisa asilolijua ndio asiwe na janja yake kwa tiba za asili.

Tukitoka huko, huyu Mzee alikuwa anashona na kubuni mitindo madizaina wa siku hizi wanguo wanasingiziwa. Na mpaka alimuopoa BIBI ambaye alikuwa ni mtoto wa Chifu kabla Nyerere hajaufuta UCHIFU, kisa ufundi wa nguo na ubunifu[Lakini nafikiri unajua tena na tundu ya mafundi nguo, mwanadada akija kupima sketi wampima na kifua:-)].


Uwezo wake wa kuongoza na kutatua maswala ulifanya awe miongoni mwa viongozi vya vya ushirika enzi hizo upareni[vyama vya walima kahawa ] na kwa kujisomea mwenyewe na kwa ujuzi wake wa mambo kemkem ukiongea naye au tu akikuandikia huwezi hata siku moja kuhisi hakusoma hasa kwa staili yake ya kujenga hoja na kujazia facts , kujua unafikiria nini [utafikiri mcheza chesi] na kwa ujumla upakuaji wa swala kiundani nk.
Ukienda kwenye ujasiliamali ndio kabisaaaa! Hawa ndio wale Wazee enzi hizo waliokuwa wanaenda Mkoa kwa mkoa kusaka bidhaa na maswala ya maduka na mengineyo kemkem, kifupi alikuwa MJANJA.

Sasa ngojea nikupe dhumuni la kukusimulia yote hayo hapo juu ambayo hayakuhusu:

Babu yangu Mrinde alifariki mwaka jana na chakusikitisha MENGI aliyokuwa anayajua kafa nayo.:-(


Hakuna mtu hata mmoja nikiwemo MIMI aliyejifunza kwake mengi na kuyahifadhi kwa ajili ya faida kwa wengine. Hakuna tena kwenye familia ajuaye mimea kama yeye, hakuna awezaye kutibu kwa kutumia mizizi na mimea [mambo yote hospitali:-(] .Hakuna hata ajuaye staili yake ya ushonaji wa mavazi au alikuwa anafikiriaje kutoka na dizaini mpya. Yani naweza kuodhoresha vitu kibao hapa ambavyo alikuwa gwiji na kafanavyo.:-(

Na ukifuatilia kwanini mtaalamu kama yeye kafariki na hakuna ajuaye au kurithi ujuzi wake utapewa sababu kirahisi kwenye familia.

Babu Mrinde yeye alikuwa anahusudu wasomi nahisi kwa kuwa yeye mwenyewe hakwenda shule. Na ukitaka akuonepoa wewe nenda shule . Sasa kwake chamuhimu ilikuwa ni kusomesha watoto wake. Na kwa sababu fulani enzi hizo akiwasomesha akina BABA alikuwa anahusudu UALIMU na UCHUNGAJI wa KILUTHERI kwa kuwa enzi hizo profesheni hizo UPARENI zilikuwa maarufu. Na watoto wake kama Baba na wengine waliokwepa profesheni hizo ilikuwa ni kwa bahati tu. Na ili kuhakikisha watoto wake wanakuwa wasomi alikuwa hataki kabisa wajihusishe na alivyokuwa anafanya yani kulima kahawa, biashara za duka, ufundi nguo n.k .Kwa mfano kwa mtoto wake ilikuwa ni mwiko kukaa kwenye cherehani kwakuwa alikuwa hataki waje kuwa kama yeye.

Lakini kinachosikitisha zaidi ni kwamba baada ya watoto wake kusoma na mpaka akina sisi kuzaliwa hakuna aliyejishughulisha kujua mengi aliyokuwa anayajua mpaka ikawa too late:-(

Wengine tulipoanza kustuka Babu alikuwa kashazeeka mpaka mara kibao ukitaka asikusahau basi inabidi ushinde naye mahali pamoja. Ilifikia ukiwa naye sebuleni halafu ukatoka nje , ukirudi tena inabidi ujitambulishe tena wewe ni nani kwa kuwa kashasahau tena ndiye uliyekuwa unaongea naye muda si mrefu. Alifikia mpaka kusahau kala ukiondoa tu sahani!:-(

KWA KIFUPI tulichelewa kudaka Busara na ujuzi wake na Babu Mrinde akafa nazo



USHAURI KWA MSOMAJI:

Ningependa yoyote mwenye kujua WAZEE KAMA HAWA wajaribu kujifunza kutoka kwao na KUANDIKA WAJIFUNZAYO au angalau KUYAHIFADHI, kwa kuwa tunapoteza sana TAALUMA na UJUZI wa mambo mengi ya manufaaa kwa kuwaacha hasa hawa MAPROFESA ambao hawakwenda shule WAFE nayo.

Na wengi kama Babu yangu ambaye alizimia Wajerumani na elimu yao na kuamini ni bora kuliko yake alichofanya ni kuacha hata yale mengine bora ya kiasili kuwafunza watoto wake kwa sababu aliamini wamesoma na hawayahitaji.


Kumbuka tu HAWA WAZEE ukija na shule yako wanaweza wasikufunze kwa kuwa tu wanaamini wewe ni msomi lakini naamini kuna mengi ya kujifunza kutoka kwa WATAALAMU HAWA na kwa udadisi waweza kujikuta unajua kitu ambacho faida zake ni kwako NA kwa jamii nzima na bila udadisi wako kingepotea.

Kuna mengi wazee wetu wayajuayo kungekuwa na chuo basi labda wao ndio wangekuwa walimu wa Profesa wa swala.

Narudia:
Tusiwaache MAPROFESA hawa ambao hawakwenda shule waondoke tu na taaluma zao ambazo nyingine tusingeleweshwa na hizi shule zakuletewa tungestukia ni bora kuliko yote tuyasifiayo YAKULETEWA na wageni.

NI HILO TU!

Ngojea Remmy Ongala abadili kidogo ingawa sio saaana kwa kibao -Siku ya Kufa







Narudia baadhi ya picha za kabla ya KUMZIKA Babu yangu MRINDE ambaye kwa mengi aliyobobea bado sijakutana na mtu mwingine kwa hayo aliyebobea kama yeye na ndio kisa changu cha kumuita Profesa na ndio kisa cha kuandika post hii....

Photobucket
Bibi akimuaga Babu kwa mara ya mwisho




Photobucket


Photobucket
Hapo ndio imetoka hiyo:-(





Babu alizikwa Mbaga Manka, kufuata sheria za kikristo na usharika wake ulikuwa huu hapa niliosimama mbele ya kibao chake... ..
Photobucket





Na ni mwaka mmoja leo tokea nitoke BONGO, asanteni wote mlionipa kampani safari iliyopita Bongo na samahani kwa kuwarudia kwa picha baadhi yenu kama hivi...

Morogoro...



Photobucket
Papaa Araway


Photobucket
Kusirie


Photobucket
Mkuu Rasta

Photobucket
Maya Davie Kitururu

Photobucket
Br Kheri Kitururu &Br Davie Kitururu



Photobucket



Photobucket
Sir Marcus Davie Kitururu



Photobucket
Sisi the DJ

Photobucket
Mr Mzee a.k.a. King of the Table





Photobucket
Bila kusahau Kijiwe hiki cha home


KILIMANJARO

Photobucket
Ras Luta Irioko Kitururu

Bila kuwasahau wote wengine...

Arusha

Photobucket
Muzee wa porojo asante kwa kutuvunja mbavu!


Photobucket
Asanteni Maanko Zangu



Mwanza

Photobucket
Kiki


Photobucket


Photobucket
Bila kusahau view hizi kutokea kijiwe cha Tilapia.


Bagamoyo

Photobucket
Jhikoman

Photobucket

Photobucket
Bila kusahau Historia




Photobucket
Bila kuisahau Bahari



Dar-es Salaam

Photobucket
Papaa Manento Kitururu

Photobucket


Photobucket
Eli


Photobucket
Adelino


Photobucket
The Chef



Photobucket
Papaa Ogola


Photobucket
Papaa Agapiti



Photobucket
FJ na Prosper


Photobucket
Rasta Luiham na Chediel

Photobucket
Bila kusahau burudani kutoka Machozi Band


Photobucket
Mzee Merinyo wa Afrika SANA

Photobucket
Mkuu wa Wilaya

Photobucket
Gayo



Photobucket
Dj Peter


Photobucket
Mhina wa The Tanzanite Band


Photobucket
Pilot wa Kibajaji nilichokizoea

Photobucket



Photobucket



Photobucket


KWA UJUMLA nawakumbuka wote na MUNGU akipenda tutaonana hivi karibuni!

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Unknown 9:53 am  

Kumbe unatoka Manka? Hata mimi huko ndio kwetu, na nina picha nyingi nimepiga hapo Manka Mission. Pole sana kwa kufiwa na Babu.

Simon Kitururu 10:11 am  

@WIM: Asante !


Mbaga, Manka huko ndio asili .Sema tu sikuzaliwa wala kukulia huko.Ila Bibi na ndugu wengine wengi wapo huko. Kwa ujumla naweza kusema pale Manka mie kuoa itakuwa vigumu kwa kuwa karibu kila mtu ni ndugu ukizingatia Chifu upande wa Bibi alikuwa na wake wengi.:-)

Ila Marehemu Babu kwa asili kabisa alitokea Vudee na huku Mbaga Manka alikuja enzi za Wajerumani na akaoa pale juu Kitala kwa Chifu na ndio ikawa makao makuu .

Mimi nilifikiri wewe unatokea maeneo ya Usangi sijui kwanini.

Yasinta Ngonyani 3:27 pm  

Simon pole sana kwa kufiwa na babu. najua alikuwa mume mwenzako au?:-) Pia asante kwa taswira hizo hapo juu mimi sitoki huko Manka....LOL

Anonymous 8:20 am  

Amani kaka.

Rasta hapa.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP