Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

HEBU kwa heshima tutumie neno KUNAJISI na sio KULAWITI wakati tunaangalia swala zima la KUBONGONYOROKA kwa MILA na DESTURI katika JAMII!:-(

>> Friday, October 16, 2009

[Tahadhari: Wazo limepinda!]

Tukiiangalia TANZANIA, kwa kubobea katika mchanganyiko wa MILA na DESTURI za makabila,...
....haishangazi kumkuta mpaka MMASAI ajulikanaye kwa MAZIWA na NYAMA akiwa ana kula bonge la UGALI na katika chai mkagombania CHAPATI.


MILA na DESTURI za kikabila,...
....NI balaa katika JAMIII IGEUKAYO kama TANZANIA halafu ambayo JANDO na UNYAGO ni televisheni na CHUO KIKUU cha swala siku hizi ni KICHENI PATI.


Kwa kuwa kwa MILA na DESTURI za makabila,...
....kuna mambo ni MWIKO au AIBU kuyaongelea, kwa UDADISI , kupenda sifa, au tu kwa KUTOULIZIA KWA KUJIFANYA MJUAJI aweza kujikuta mjanja KALAWITIWA , au hapa kwa heshima tu tuseme TU kuwa KUNAKO NANIHII kageuzwa PATI.:-(




Na kwa ilivyo TANZANIA sasa hivi, kirahisi MTOTO asili yake ni KIGOMA atajikuta anaishi DAR-ES-SALAAM na anafuata MILA na DESTURI za jirani yao za kikabila,...
..... na kwa kuwa jirani anatoka BAGAMOYO - kukiachana na yule wa nyumba ya upande wa pili atokaye KARAGWE ,- KUMBUKA kwa jirani NI SHULE kutokana na kwa kuwa, kwa watoto wa jirani ndiko MTOTO ashindako zaidi kuliko kwa wazazi ambao hata WAZAZI WENYEWE wakirudi kutoka kazini huwa wamechoka tukiachilia mbali kuwa

....WAMECHOKANA,......

..... kirahisi MTOTO aweza changanyikiwa AKIPEVUKA na kustukia ANAHAMU ya KUONJA na ampendaye KIHASI na CHANYA ni MCHAGA aiyekulia KIGOMA mwenye kuathiriwa na za KILUGURU DESTURI na MILA katika kumlenga ajiingize kichwakichwa, hivi amuandalie TOGWA au MBEGE kama kinywaji kwenye aiandaayo PATI.


Na tukiacha utani , katika MILA na DETURI zilizochanganyika za makabila,...
....kumbuka BAOLOJI YA MWILI haijui TAMADUNI wala MWIKO, na kwa akuaye akianza kuvutiwa wakati ya JANDO na UNYAGO hajayapitia , aweza NAJISIWA mtu wakati dhambi iliyokuwa inalengwa ilikuwa tu ni ya UASHERATI ,halafu MASIKINI kwa kutojua kuvumilia , ya FARAGHA akajikuta kayaonjea tayari halafu ghafla kwenye PATI!:-(

Swali:
  • Unafikiri kwa wenye TELEVISHENI, kati ya WAZAZI na episodi ya ISIDINGO a.k.a THE Bold &The Beautiful, ni nani mwalimu mzuri wa penzi ni nini ,KUGAWA hovyo NI UMALAYA, KUNA UKIMWI, tukiachilia mbali swala zima muhimu la jinsi ya kukata DENDA?
  • Unafikiri kwa hali halisi ilivyo na jinsi MILA na DESTURI ziwakatavyo kauli WAZAZI kuongelea swala zima la MAMBO MPWITO, when nature calls mdadisi hawezi kujikuta kakosea kionjeo kabla ya kupatia shabaha zilengwe wapi?


NI WAZO TU MHESHIMIWA na haki ya nani NIMELIACHA!

Hebu TIPPA IRIE alalamike katika -Rebel on the ROOTS COrner


Au tu BASCOM X arudie simulizi ya hali halisi katika -EYES on the the PRIZE

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Chacha Wambura 8:55 am  

mwanangu leo umekamua kisawasawa!!!

Keep the pace up!!!

Simon Kitururu 11:33 am  

@Kadinali Chacha Wambura: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP