Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

CHUPI ibanayo, bado INABANA hata kama haichaniki kwa kuwa aivaaye ANAPATIA STAILI ya KUINAMA!

>> Thursday, December 03, 2009

NDIO!

....Ni suruali ILIYOBANA na sio CHUPI ambayo kwa kawaida NDIYO ishuhudiwayo NA ASIYE KIPOFU ikitatuka wakati MWENYE TAKO hata AMBALO HALIJANUNA anainama kuokota kidude,...


.... na KATIKA HILO pia kwa kawaida ABANWAYE na PEKOSI au tu KIFICHA NYETI anajua NYUPI au SURUALI YA KODRAI BWAYA YA MTUMBA haikuanza kubana makalio wakati huo IKITATUKA na KUNAUWEZEKANO ni staili tu ya kuinama iliyochana KISUGUA NYETI muda HUO:-(



NDIO!
...Chupi a.k.a KIFICHA NYETI au SURUALI AINA YA PEKOSI YA MTU iliyobana NYUMBA YA MILANGO YA HAJA KUBWA NA NDOGO itatukayo mtu akibinuka kuokota kidude,....

... mara karibu zote SABABU ZAKE ZA KUTATUKA au kuchanika KWAKE ,sio kwa kuwa inabanwa na tako KIBONGE hasa tu KAMA UTACHUNGUZA VIKOROMBWEZO VINGINE vifanikishavyo CHUPI YA HALIMA/Hamisi , ILE SAFI , mbele ya MNUNIO WA KITU SAFI a.k.a MLANGO WA KIDONGOLOSO WA NYETI kama vya umadhubuti wa kitambaa ,NYUZI na kadhalika kadhaa wakati wa mtatuko HUO:-(


Ngojea nilainishe kachori:

Na maana kuwa WAKATI unakosea kosa moja, kunamlolongo wa mambo yaliyoko nyuma ya hilo tendo ukosealo NDIO MAA UMEKOSEA HILO NA SASA HIVI.:-(

Kielelezo :
  • Kwa mfano kama KOSA LAKO ni kirahisi unafanya UMALAYA.
Siri ya kosa lako hilo la UMALAYA linaweza kuoanishwa na mlolongo wa mambo MENGI kwa mfano;

- labda tokea mtoto ulifunzwa kugawa na haukustuliwa KUWA kuna tofauti kati ya kugawa PEREMENDE au BAZOKA na MWILI, kimaumbile yako au kibaolojia WEWE kila baada ya sekunde kadhaa badala ya kufikiria msosi UKIWA NA NJAA kwa kawaida WEWE unafikiria sehemu za siri kitu kikufanyacho unakuwa MAHARAGE ya MBEYA a.k.a MAJI MARA MOJA, umechacha na akili zako zifanyavyo kazi na mazingira uliyokulia YALIVYOKUFUNZA yamekufanya uamini kujifunza ufundi seremala ili uishi na kulaliwa na kupewa UTUPU uupendao tu halafu unalipwa KATIKA HITIMISHO ukahitimisha ni rahisi kulaliwa au kubinuka kuliko kuchonga vinyago.:-(

  • Kwa mfano kama kosa lako katika kuwakilisha RIWAYA lilisababishwa na kukosea UNG'ENG'E' a.k.a KINGEREZA.

Siri ya kwanini UNG'ENG'E KWAKO haupandi linaweza lisisababishwe na kitu kimoja tu kuwa una ulimi mzito hasa ukiangalia mlolongo ulio kukumba wa kuwa MWALIMU wako mwenyewe aliyekufundisha Ung'eng'e kwake mwenyewe UNG'ENG'E ulikuwa haupandi vizuri , hujawahi kukutatana na waongeao Kiingereza kwakuwa hata Padre wa kijijini kwenu na marafiki zake WATASHA walikuwa ni WAITALIANO ambao kwa bahati mbaya ung'eng'e ulikuwa unawatoa jasho na HALAFU wanashuka KILUGURU na KISWAHILI utafikiri ni MKUDE, halafu bila kusahau ukweli wenyewe kuwa WEWE NI MVIVU WA KUJIFUNZA MAMBO yaliyoko nje ya UDAKU ,....nk.

NALIKATIZA WAZO HAPA.:-(



Swali:
  • Umejaribu kuninielewa naongelea nini Mwanakwetu?
  • Kwa hiyo umenielewa sasa KUWA wakati unaharibu hiki , UHARIBIFU WAKO WA HIKI kunauwezekano umechangiwa na KILE ambacho kinaweza kisihusianishwe kirahisi na HIKI?

  • Unakumbuka wakati unazungumzia CHUPI moja , unachogusia pia ni ushirikiano wa kitambaa, nyuzi na labda hata rababendi ishikiliayo chupi yako kiunoni ambayo vyote kwa USHIRIKIANO HUO hufanya CHUPI YAKO iwe CHUPI yenye mauaua?

NIWAZO TU HILI Mheshimiwa na NIMEACHA!:-(





Ngojea Barrington Levy abadilili kama alivyofanya 1984 katika- Here I come


Nimuache juzijuzi katika-Too Experienced


Au nimrudishe tena enzi katika -Murderer


Au tumalizie kwa kwenda Uingereza mwanzo wa Jungle MYuziki katika kitu cha jungle enzi hizo ambacho katika jango miye nikiwa mpenzi wa staili hiyo najua bado ni kikali. Dr Edo Mtafungwa unakumbuka enzi? -




Au ngojea niache picha na wadau Juzi ya jana nilio kuwa nao wakati Mtaalamu Barrington Levy anatunong'oneza.


Photobucket




Photobucket




Photobucket



Photobucket




Photobucket





Photobucket




Photobucket




Photobucket




Photobucket








Photobucket



Photobucket




Photobucket



Photobucket


Photobucket




Photobucket




Photobucket



Photobucket




Photobucket



Photobucket

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 6:53 am  

Leo sijaona picha ya bilauri. Ama ulibanwa sana na chupi ukashindwa kuinama na kuichukua?

Simon Kitururu 11:47 am  

@Askofu Fadhy: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP