Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kuwa BINADAMU hukosea MPAKA kwenda HAJA KUBWA!::-(

>> Sunday, December 27, 2009

[Tahadhari: Lugha ya tararila inaweza kumkwaza Mheshimiwa ATAFSIRIYE USTAARABU kinamna FULANI, kwa kuwa haijavalishwa chupi!:-(]





Kuna siku MHESHIMIWA achambaye,....

.... hustukia ANAHITAJI kuchamba KIREFU au tu kwa JUHUDI zaidi katika KUJISWAFI kwa kuwa Mheshimiwa pamoja na uzoefu WOTE siku hiyo kwa bahati mbaya hajapatia kunya VIZURI.:-(



Na kwa kuwa BINADAMU achambaye,...

... kuna siku hukosea mpaka KUNYA [ au kwa lugha ya kistaarabu:``hukosea kuachanisha mwili na kinyesi´´],....

.... jiulize ni nini basi BINADAMU mahiri asichoweza kukikosea ambacho anajulikana kwa kukifanya VIZURI. :-(






Swali:

  • Si unajua hata mzoefu wa kukata tonge la UGALI kuna siku katika staili ya kula hudondosha tonge?
  • Huwa unajipa ruksa kujisamee ukikosea kwa kuwa unajua kuwa taka usitake weye kama binadamu kila siku unakosea?
  • Si unajua kila siku ya Mungu kuna kitu unakosea ingawa ni baadhi ya mambo ambayo unayashupalia ukistukia UMEYAKOSEA?

  • Si unajua ni baadhi tu ya mambo ndio uchaguayo kuyastukia au tu tuseme ndio uyastukiayo TU kuwa umeyakosea wakati kila siku ni mambo kibao unayakosea?

  • SI unajua kuna wakati unapatia zaidi KUNYA kuliko WAKATI MWINGINE ingawa wakati uhitajio TISHU a.k.a MAKOKONEO zaidi au tu MAJI zaidi katika kufanikisha KUCHAMBA hutafsiri kuwa ni kwa sababu tu ulikosea KUNYA?


NDIO,...
..... unaweza KUNIBISHIA katika yote niliyosema lakini amini KILA siku ni baadhi tu ya mambo uyastukiayo UKIKOSEA wakati kila siku ni mambo kibao UNAYAKOSEA.:-(



Na pia kama tu swala la - nini ustukiacho ukikosea lilivyo kama tu swala ZIMA la nini kwa kawaida HULIKUMBUKA KILA SIKU- nikiwa na maana : ni mambo machache sana MTU KIBINADAMU huwa unayakumbuka kila siku ingawa katika siku ni mambo kibao huwa unayashuhudia, kuyafanya au kufanyiwa.:-(



Nimeacha NA KUMBUKA ni wazo TU hili MKUU na nia na madhumuni sio KUKUKWAZA Mheshimiwa!:-(


Namuachia Isaac HAYES arudishe ustaarabu kwa- I stand ACCUSED


Au tu Isaac HAYES amalize kwa kitu-SHAFT

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

mumyhery 1:25 pm  

mmhuu!!!

Yasinta Ngonyani 5:56 pm  

Duh!! kazi kwelikweli nimejifunza kitu fulani

Simon Kitururu 9:58 pm  

@Mumyhery: Mmhuu!
@Da Yasinta: Duh!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP