Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

PETE YA HARUSI, msalaba KIFUANI /jengoni, PICHA YA Rais NYERERE ukutani,.... vyote kialama vikifanana na HERENI imtambulishayo MSENGE!:-(

>> Wednesday, December 30, 2009


[Tahadhari MHESHIMIWA: Tararila hii ina ZIGZAG katika Mtiririko ,Lugha iliyotumika, na Mifano pia. Kwa hiyo kama weye ni mtoto , Mavi kwako ni rahisi kuyaita Kinyesi na Matako unadhani ni ustaarabu kuyaita makalio- unaweza usielewe naongelea nini au kwa kifupi hii tararila haikufai.:-(]







Kwa kuwa YASIYOTUHUSU,...


...kuna wanaopenda tujue,...



.....YAWAHUSUVYO.....


... binadamu hutumia mpaka ALAMA katika vielelezo ili tu YASIYOTUHUSU nayo TUYAJUE.:-(


MATOKEO yake,....
.. mpaka PENDO BINAFSI LA watu wawili,......

..MME na MKE hulazimika katika jamii fulani fulani kama YA WATANZANIA kulivalia PETE ili kutuhakikishia siye KISICHOTUHUSU ,....


....kuwa wako katika NDOA na MPENZI wakati SIRI YAO YA MOYONI kuhusu HIYO NDOA ambayo ndio JAMBO LA muhimu KATIKA NDOA,..

... inapiga kelele;..

  • HII sio NDOA

  • Napenda pesa zako na sikupendi wewe.

  • Wazazi wasingenilazimisha usingenipata, na jamii isingetegemea nipate mimba NIKIOLEWA nisingekupa kidude ng'o labda unileweshe.

  • Niko nawe kwa kuwa nilipata mimba kwa bahati mbaya na nikakosa wakumsakizia mimba kabla WEWE hujajiingiza kichwakichwa katika zile TAIMINGI kwa ung'eng'e ziitwazo ;``just at the right time´´.

  • Wewe Msichana INGAWA NIMEKUOA ni kweli unasura kama SAFARI BUTI iliyochakaa nisiyoipenda na inukayo uvundo . Lakini BABA yako tajiri kama MENGI na nazimia sana hilo MPENZI ingawa ASANTE NYINGI ZIENDE katika jinsi ulivyoniachia kazi ya kuchagua mahausigeli hapa nyumbani kitu ambacho kimenisaidia kuajiri mapoozeo yanisaidiayo kujisikia KURUDI nyumbani na hata kulala chumba kimoja na wewe. Na kuhusu sekretari wangu ofisini asaidiavyo kunifanya nikuvumiliea kwa kuwa hujamstukia BADO ngojea hiyo iwe siri yangu kwa sasa.


  • NK. :-(


Swali:

  • Si unajua pamoja na PETE KUVALIWA bado kuna wapendao na kuvutiwa na WAUME au WAKE ZA WATU na wakikuona na PETE ndio wanajua wamempata wa KUMTONGOZA?


  • Kwani unafikiri kwa mpenda MUME au MKE wa mtu ANAKWAZIKA NA PETE mpaka ahitaji PETE IVULIWE saa na wakati wa kufanikisha UASHERATI a.ka KUZINI a.k.a KUCHOKONOA DAFU ikifika?



-Tuendelee...-




KWA kuwa YASIYOTUHUSU;....

...kuna wanaopenda tujue,....

... YAWAHUSUVYO,....




MATOKEO YAKE,....

.... kuna WAKRISTO wafikiao kuvaa MSALABA ili kuwahakikishia yasiyowahusu UISLAMU au tu UBUDHA haupandi kwao,...

....KITU ambacho LABDA wangejisikiliza MOYONI wasingehitaji kuhakikishia WENGINE ukristo wao SASA HIVI kwa kuwa WANGESTUKIA kuwa hata UKRISTO wenyewe MOYONI MWAO hawauelewi na bado kiimani HAUJAPANDA VIZURI:-(



Swali:

  • Unauhakika wahubiri wahubiriao wengine INJILI wangetumia busara wasingestukia wao ndio wahitajio zaidi injili ya Mheshimiwa YESU?

  • Unafikiri alama ya MSALABA kwa wengi sio PAMBO tu kama KINYAGO cha Kigoli mcheza SINDIMBA cha Mmakonde?

  • Unafikiri vyako vya MOYONI ni DHAIFU KIASI GANI mpaka wajanja kama akina PAPA WA KANISA LA KIKATOLIKI ikabidi wavalishwe bomba la GAUNI na KOFIA ukubwa KIKAPU , Mchungaji wa KILOKOLE Morogoro akalazimika kuhubiri kwa sauti ya Kizungu, SHEKHE wa KIBENA akalazimika kuwa na lafudhi ya Kiarabu katika kushuka neno,.... ILI tu kudaka utulivuwako ULAINIKE wakati unapewa NENO la MOLA?


  • Unafikiri vyako vya MOYONI ni DHAIFU KIASI GANI mpaka ukitaka kujaribu TUVIJUE WEWE MWENYEWE HAUTOSHI mpaka inabidi utafute msaada wa ALAMA FULANI FULANI kama vile MSALABA au tu HERENI SIKIONI ili tu tujue PENDO lako ni la KISENGE?



-Tuendelee,...-



KWa kuwa YASIYOTUHUSU,....

... kuna wanaopenda tujue,....

.... YAWAHUSUVYO,...



MATOKEO yake,...

.... ndani ya TANZANIA kuna MABEPARI na MAFISADI kibao ambao katika kuta za ofisi au nyumba zao kuna PICHA YA Rais NYERERE,...


... kitu ambacho LABDA HAKITUHUSU ingawa hakiachi kushangaza hasa ukifikiria imekuwaje MHASISI wa SIASA YA UJAMAA na KUJITEGEMEA asiyehusudu UBEPARI anafanya nini katika ukuta wa FISADI BEPARI ambaye anaamini UBEPARI kama tu UBIKIRA wa BIKIRA MARIA ni kitu kinachoeleweka kirahisi na ni KITUKUFU!:-(




Swali:
  • Unakumbuka lakini Siasa ya UJAMAA na KUJITEGEMEA kuna iliyowafanya wawe WATEGEMEZI na inazidi kufa leo hii chini ya walewale waliokuwa WANADAI wanaamini hiyo SIASA na pia waliitikia sana ZIDUMU FIKIRA za MWENYEKITI ambaye moja ya fikira zake ilikuwa ni AZIMIO LA ARUSHA na SIASA ya KUJITEGEMEA?

  • Unauhakika kwa MAFISADI MABEPARI, picha ya Rais Nyerere hawaitumii kama ALAMA ya;`` UJAMAA ZIII na UJANJA NI KULIA OFISINI OYEEE!´´?

  • Unauhakika kama wewe MTANZANIA una picha ya RAIS NYERERE ukutani mwako, MZUKA /Mzimu wa MWALIMU NYERERE ukipitia NYUMBANI KWAKO hausikii KICHEFUCHEFU?




NDIO,...

....tukiachana na VINDUMBWENDUBWE kibao katika HOJA ZANGU kibao HAPA ZENYE KIBIONGO,...



.....labda bado kuna UKWELI kuwa,...

... ALAMA KIBAO,...

... kama tu ilivyo MISALABA kwenye makaburi ya WAKRISTO kwa wengi,...
.... ni MAPAMBO TU.:-(






NDIO,...


....ALAMA,...


....kama tu madoadoa usoni kwa KISURA,....


.....inaweza tu kumaanisha KISURA aliwahi kuwa na VIPELE VYA UCHAFU na wala ALAMA ZA madoa HAYO hazimaanishi kuwa KISURA aliwahi kuugua TETEKUWANGA utotoni ,...



....kama tu ile alama ufikiriayo ni ya NDUI ukweli wenyewe ni KWAMBA hapo alikuwa na BONGE LA JIPU.:-(





Swali zaidi kiduchu:
  • Si unakumbuka KUTONIELEWA hasa kama tu kuna kitu umefikirishwa kwa kunisoma katika tararila hii RUKSA?




NIMEACHA WAZO Mheshimiwa na KUMBUKA hili ni wazo tu MKUU wa KITENGO!:-(


Hebu Michael Jackson kama Spike Lee alivyo Direct atupe- This IS IT




Sijui kwanini bado -JULIE naye ananitekenya kichwani kama tu adaivyo Oliver N'goma



2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! 10:33 am  

duh!

sina hakika kama kuna kuvua pete kunako tendo na avuae huwa ni mnafiki kwani pete haina macho au vinginevo anaogopa itachafuka ama itaona kitendo.... :-(

nina hakika fisadi akisoma hii makala atawaza kama wewe na atakuchukia na kusema...lione hilooo linaamsha walolala... :-(

mziki na pilau lake...duh sijui manake...lol

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 10:42 am  

sasa kwa nini hujaweka picha yangu ya mkono wa kushote wenye pete mpya inayonng'ara bado!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP