Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Matatizo YALIYOJITOKEZA baada ya WATANZANIA kufunzwa kufuata GREGORIAN KALENDA ambayo inadai leo ni MWISHO WA MWAKA!:-(

>> Thursday, December 31, 2009

GHAFLA Mzee akumbukaye kuwa alizaliwa wakati KIBAHA kulikuwa na SENENE wengi,...

....huanza kuonekana HAJAELIMIKA kwa kuwa hajui tarehe aliyo zaliwa.:-(


GHAFLA Kigoli mwenye bonge la TITI kuna ushahidi ni MTOTO,..
...kwa kuwa kuna vyeti vidaivyo ana miaka kumi na NNE tu na hafai KUOA.:-(



GHAFLA Mheshimiwa MTANZANIA anajisikia MZEE ,...

.. kwa kuwa kastukia kuwa eti miaka ya WASTANI wa MTANZANIA KUFA,...

... DUME ni miaka 51 na JIKE la KITANZANIA ni - miaka 54


Ghafla KUBWA JINGA lenye mambo ya KITOTO,...
... linakabiliwa na KUHESHIMIWA kama KUBWA kwa kuwa kuna uhakika lina miaka SABINI.:-(




Swali:

  • Unafikiri kwanini TANZANIA haifuati KALENDA ya KIISLAMU wakati walioleta UISLAMU walikuja na KALENDA ya KIISLAMU?

  • Unafikiri ni kwanini ETHIOPIA ni nchi pekee karibu na TANZANIA yenye KALENDA yake yenyewe?

  • Unafikiri ni kwanini BC na AD a.k.a "Anno Domini" na "Before Christ" havijulikani na wengi kuwa ni "CE" na "BCE" a.k. a "Common Era" na "Before Common Era" ?

  • Unazijua KALENDA NGAPI zitumikazo sasa hivi duniani ambazo leo sio MWISHO wa MWAKA?






Photobucket

NAKATIZA HILI wazo NYOKO hapa!

NAKUTAKIA HERI katika MWAKA MPYA Mheshimiwa!

ASANTE SANA kwa KUNITEMBELEA HAPA KIJIWENI MKUU!




Moja kwa moja tubadili kwa kumuachia AFANDE SELE arudishe- DARUBINI KALI



Au tu Mr EBO acheki uzoefu wake katika kukujulisha wewe- MBADO

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 10:23 am  

Sana tu. Ila hiyo Darubini Kali ina akili usipime.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! 11:56 am  

nahisi kwa kalenda ama bila kalenda nimekuwa muzee tayari :-(

na pia nahisi kuwa wewe huna kalenda :-(

Upepo Mwanana 12:44 am  

Maswali uliyouliza ni magumu.
Nakutakia heri ya mwaka mpya

Mija Shija Sayi 8:00 pm  

Yaani wee acha tu.

Yasinta Ngonyani 9:49 pm  

Heri ya mwaka mpya nawe pia ila usinywe ugimbi mwingi...lol

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP