Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Inategemea unaridhikaje na LABDA kwako ili uridhike NA MAISHA YAWE NA MAANA yahitaji UWE MALAYA!:-(

>> Wednesday, December 02, 2009

Maana ya MAISHA kila mtu huipata kivyake.

NA umuhimu wa MAISHA kila mtu ni kivyake.

Na labda si kwa bahati mbaya kuna tamu na CHUNGU
.

Na labda si kwa bahati mbaya KWA WAAMINIO , kuna SHETANI na MUNGU.

Na kama iwavyo kuna wapendao JOTO ,kuna wahusuduo BARIDI.



KIKUBWA nachojaribu kukijenga kwa hoja banangenge :

Labda umuhimu na kiletacho maana KWAKO hakihitaji tafsiri za WENGINE kwa kuwa WENGINE ni WENGINE na WEWE sio wale WENGINE.


Kwa hiyo labda siri ya furaha na kuishi maisha yakufarijio WEWE na YENYE MAANA kwako ni kujisikiliza weye MWENYEWE na kufanya yenye maana kwako na yajazayo roho yako KIBURI cha kuwa '' KAMA nanogewa, nikiungua wakumlaumu si mwingine bali ni MIMI MWENYEWE.'':-(


Swali:
  • Kwani weye ni yule apendaye kulaumu wengine kwa kuwa tu kwa kufuata ya wengine uliwahi pata gono?
  • Unafikiri kujilaumu mwenyewe na kulaumu watu wengine nini ni kitamu zaidi?

Tukiachana na hilo:

Kumbuka MAISHA ni mafupi,...

.... na kwa wengine hupata mimba sio kwa kuwa wanapenda watoto , ila ni kwa kuwa kwa kuwa na watoto na kulea watoto ndio maisha yao HUPATA MAANA na KATIKA MASWALA YA WATOTO ndipo wapatapo jibu la kwanini wako HAI na wana umuhimu kwa kuwahai DUNIANI,...
..... ingawa kwako labda ingetosha KUFUGA mbuzi na kuku wa kienyeji kutimiza hilo kwa kuwa watoto kwako kuwazaa una uke mdogo na kulea si staili yako.


Lakini kumbuka MAISHA ni mafupi,....

.... na kwa wengine ni NYUMBA wajengazo na MAGARI waliyonayo ndio yasababishayo wajisikie ni WATU WA MAANA na wanasababu ya kuamka tena kesho na kuendelea kujamba kidogo kama kawaida hasa wahisipo hakuna watu karibu,...

.... INGAWA kwako labda NYUMBA na GARI havitoshi na unahitaji KUFUATA DINI ili maisha yako yapate maana na ili utulie na kufarijika kwa kutokuwa na majibu ya kila kitu kwakuwa unajua MUNGU umuaminiye ndiye AJUAYE YOTE.


Na kwa wengine KUMBUKA maisha ni mafupi,....

...na labda kiletacho maana maishani KWAO wala sio kujua FIZIKIA na KEMIA kama wewe ila ni kujua tu kucheza MAYENU, mugongomugongo, BREAK DANCE, MDUNDIKO na SINDIMBA kidogo kabla ya kuchezewa sehemu zako za SIRI na mtaaalamu APATIAYE ili maisha yalete maana na wajue mpaka ni kwanini wanapenda sana CHUPI MPYA na za mauaua kuliko hesabu za Kalikulasi.:-(



Na,...

...Wengine kiwahangaishacho ni kujaribu kuwa na maisha MAREFU, ...

.....ingawa labda kwa mwingine MAISHA MAREFU hayana maana ikiwa kuishi kwenyewe kurefu TAFSIRI YAKE KWAO ni kujiongezea maisha ambayo UVITAMANIVYO NI DHAMBI, unaambiwa vinamadhara kiafya AU TU kuvipata kasheshe:-(


NALIKATIZIA WAZO HAPA!:-(

Swali:
  • Unauhakika maana ya MAISHA kwako haujatafsiriwa na mtu mwingine?
  • Unauhakika hujaribu kujiridhisha yako kwa kukopi ya wengine ambao labda hawasikii utamu wakibinywa jipu kama usikiavyo weye?

Hebu Al Green aongelee-Love and Happiness

9 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

chib 6:48 pm  

Tukifikiria ya kuwa maisha ni mafupi, basi hatutafanya cha maana au....., lakini usijinyime sana kama wapare, (natumaini sitaguswa kwa kutoa mfano tu....)
Halafu unasubiri kutumia sijui siku ya mazishi yako... :-(

Fadhy Mtanga 8:01 am  

Love and Happiness

Yasinta Ngonyani 12:16 pm  

Fadhy! inaweza kwa kinyume pia love ana unhappy!!

Simon Kitururu 12:45 pm  

@CHIB: :-)
@Askofu Fadhy: Hivyo vitu ni vya ajabu kweli.

@Yasinta: :-(

Yasinta Ngonyani 12:56 pm  

Mt. Simon unabisha au?:-(

Serina 6:17 pm  

Na watu wote wakasema...AMINA! :-D

Yasinta Ngonyani 5:13 pm  

Mt. upo wapi umejificha au unaumwa maana si kawaida yako kuwa kimya hivi!!!

chib 5:47 pm  

Hodiiiiiii, he! umefungua blog mpya nini. Rudi mkuu

Simon Kitururu 9:23 pm  

@Wote: Wajameni Nipo! Matatizo tu ndio maana !:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP