Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MPENZI una UBONGO KISURA KWELI!

>> Tuesday, December 15, 2009

SAMAHANI Do not DISTURB!

...... a.k.a usinisumbue , NATONGOZA mtoto nidhaniaye ana miakili KEDEKEDE :


''Nakusabahi WAKWETU hujambo lakini!.....,....

......Yani MPENZi ubongo wako ulivyovaa ULIMBWENDE wanifanya nakupenda mpaka najisikia MAUMIVU!

Hivi mpenzi UBONGO wako unaupodoa na nini MWANAKWETU mpaka umevaa ULIMBWENDE namna hiyo? Halafu KIPENZI yani MPAKA cheko lako limekaa mkao wa MIAKILI tu , UNANAFASI twende chumbani kwangu tukajisomee?......................,.................´´
-nimemaliza kutongoza na NISHAKATALIWA.:-(




Wakati tunaishi katika DUNIA ambayo mvutio wa TAKO LA MTU wathaminiwa kuliko AKILI na UBONGO wa MWENYE TAKO,.......

.......chakusikitisha NI KWAMBA INAZIDI kuwa vigumu kusikia hata MTONGOZO ambao MANENO YAKE MATAMU yamebobea katika UBONGO na AKILI ZA MTU kutokana na kwa atongozwaye kuvutia kwa UBONGO na AKILI ZA KIUTU,....

...... hasa kwa kuwa atongozwaye ULIMBWENDE wake KWA ATONGOZAYE unahusianishwa ZAIDI na avutiavyo SEHEMU ZA SIRI a.k.a NYETI ZAKE kuliko UBONGO WAKE .:-(



Swali:
  • Unafikiri ni kwanini MAJINIASI a.k.a WENYE MIAKILI KEDEKEDE wanahesabika tu duniani?
  • Unauhakika mwanao atakuwa na MIAKILI kedekede kukushinda wakati wewe mwenyewe unaovutiwa NAO zaidi ni WAJINGA ingawa kwa kujipodoa ni Maprofesa?

  • Ukitongozwa ukakubali unafikiri ulipenda akili za aliyekutongoza au tu kwa kuwa ana BENZI na SURUALi ya pekosi dizaini GUCCI?
  • Kama akili ni SURA unafikiri MPENZI wako ulimpendea SURA NZURI?

NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA!:-(


Hebu Klyinn Ft Blue twalete- NIPE MKONO


Au tu Juliana Kanyomozi & Bushoke walete tena- Usiende Mbali

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! 7:26 am  

nahisi hata kusoma hapa nimetongozwa japo sijui nani kanitongoza....lol

cheers

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! 7:28 am  

nahisi hata kusoma hapa nimetongozwa japo sijui nani kanitongoza....lol

cheers

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP