Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ujifunzacho kirahisi CHOONI!

>> Monday, December 28, 2009

CHOONI ni mahali pazuri PA kujifunzia kirahisi kuwa MAISHANI kuna vya lazima VINUKAVYO,....

..... na maishani HARUFU ya vitu VILEVILE vyenye jina LILELILE hutofautiana DIGIRII za MNUKO hata kama chanzo cha harufu kina jina LILELILE .:-(





SWALI:
  • Au?

Na ukitoka chooni waweza kujikuta umestukia kuwa SI VIBAYA mara kwa mara kukatiza SHUGHULI nyingine muhimu kama vile kazi kwa ajili ya shughuli nyingine NDOGO NDOGO za muhimu kama vile KWENDA MSALANI kwa ajili ya KUTATUA haja ndogo kwa manufaa yako au tu ya MWILI WAKO .



Na ukitoka CHOONI ,....
.....kwa mafanikio ya chooni hasa kama ulibanwa sana KABLA YA KWENDA chooni, waweza stukia kirahisi na kuelewa KIRAHISI nadharia nzima ya ``BAADA ya KAZI NZITO kuna FARAJA´´, hasa kama kilichokupeleka chooni kilihitaji juhudi na kilikuwa na uzito angalau katika JINSI ulivyokuwa unajisikia kabla ya kukifanikisha huko msalani,..
.... NA kwa MAFANIKIO YAKO hayo CHOONI wajisikia FARAJA na ahueni katika HALI YAKO.



Swali:

  • AU?
  • SI unajua ingawa matunda ya shughuli za chooni hudumbukizwa chooni hudhani moja ya funzo la hilo ni kwamba si lazima matunda ya kazi yako yaliwe au watu wengine wayaone?
  • Mheshimiwa kama ulifanikiwa LEO kwenda CHOONI ,umejifunza nini leo huko chooni?
  • Si unajua mahali popote kwa mjanja ni SHULE YA MAISHA kama unania ya kujifunza?






NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA na NIMELIACHA!


Hebu basi mshairi LINTON KWESI JOHNSON arudie kishairi kuzungumzia- New world ORDER


Mshairi Linton Kwesi Johnson arudie pia shairi-Sonny 's Letter


Au tu Linton Kwesi amwage na shairi-Want FI go Rave?

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mija Shija Sayi 12:37 am  

Ni kweli kabisa.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 2:53 pm  

ndio

Markus Mpangala. 5:11 pm  

hakika

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! 12:04 pm  

Mh! Heri aliyekunya akanawa kuliko aliyejamba :-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP