IKITOKEA KUWA kwa bahati mbaya UMEANZA KUAMINI UONGO WAKO uwadanganyao WATU WENGINE!:-(
>> Friday, December 18, 2009
GHAFLA,......
.... unaweza KUANZA kuamini una bonge la TAKO,.....
....wakati wengine wanatafuta MAKALIO YAKO BILA MAFANIKIO  yako wapi kwa kuwa hawazioni NUNDU ZA TAKO katika lako KALIO.:-(
GHAFLA,....
.... zile stori zako za kubuni za KIJANJA  zinaweza kukufanya uanze kuamini WEWE ni  kweli ni MJANJA.
Na taratibu,.....
.... ULEVI WAKO WA KILA SIKU   waweza KUKUFANYA  ujiaminishe KUWA  sio ulevi ILA  ni BURUDANI  tu kidogo YA KILA SIKU ya  kutuliza KICHWA baada ya KAZI NGUMU  kwa kunywa tu pombe sana kidogo kuliko wengine  na hilo ni KWA KUWA WEWE UMEIZOEA POMBE na wala  HILO sio tatizo wala ULEVI.
Ghafla ,....
.. na kugawa kwako  kidude ovyo waweza amini si UMALAYA ila ni ROHO NZURI TU YAKO ya kugawia kila wenye HITAJI mgao.
Na taratibu,...
.. kwa kuwa uliwahi kusifiwa MZURI SANA UKAAMINI, waweza anza kuamini wote wasioona UZURI WAKO ni ma-HATER a.k.a WAKUONEAO DONGE TU kwa kuwa wewe MZURI.
KABLA SIJAKATIZA WAZO, kwa kifupi nachojaribu kusema NI:....
Kama umezoea KUDANGANYA watu ni hekima kuchunguza ni lipi urudialo mara kwa mara katika KUDANGANYA WATU  ili kuhakikisha huanzi KULIAMINI kuwa HILO  ni KWELI WEWE MWENYEWE.
 Tatizo ni;..... ......si rahisi kustukia ni dakika na SAA GANI ATAKAYORUDI BWANA YESU,... [samahani!]..
nilitaka kusema si rahisi kustukia ni sekunde gani ianzishayo kugeuza udanganyacho, wewe mwenyewe kuanza kukiamini.:-(
 Na UKISHAAMINI udanganyacho  unaweza usiustukie UONGO wake kama tu SIMON KITURURU alivyoanza kuamini ni kweli yeye ni; Mtakatifu SIMON KITURURU.:-(nilitaka kusema si rahisi kustukia ni sekunde gani ianzishayo kugeuza udanganyacho, wewe mwenyewe kuanza kukiamini.:-(
Swali:
- Unafikiri kuna asiyejidanganya?
- Unauhakika hujidanganyi kuwa akuambiaye anakupenda ni kweli anakupenda?
- Unauhakika unajua ni lipi katika urudialo kudanganya watu ndilo upatialo vizuri KUDANGANYA?
NIMEACHA!
Na moja kwa moja turudi HAITI Wyclef JEAN alete -M.V.P. Kompa
Au tu tubaki hapa hapa HAITI Wyclef Jean aje na T VICE pamoja na BUJU BANTON warudie-Party by THE SEA
 
  
 Posts
Posts
 
 




0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment