Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

NITAKUSHANGILIA kwa lolote! - ''Si unajua wewe ni MTU wa KWETU halafu NI ukoo mmoja?''

>> Wednesday, December 02, 2009

''WAKWETU lazima tumshangilie kwa lolote lisifiwalo''
- ni moja ya busara za watu.


Lakini lolote lisifiwalo,..
... na WAKWETU TUMSIFIAYE kwa kuwa ni WAKWETU saa nyingine afanyacho ingawa wajanja wanakishangilia, hakistahili SIFA wala kushangiliwa ingawa kina umaarufu na KUSHANGILIWA na WEWE ujipendekezao KWAO.:-(


NDIO sikatai,...
..KUNA WASTAHILIO SIFA!

Swali:
  • Unauhakika hakuna uwashangiliao wakati hata wafanyacho hukielewi kifanyacho washangiliwe na unashangilia kwa kuwa tu MNATOKA kabila moja, NCHI MOJA, nyumba moja, au yeye kama wewe wote mafanikio yenu yalianzia kwenye umalaya?

  • Hivi weye kama MTANZANIA hujawahi kuionea aibu TV au redio kisa kiongelewacho ukiwa na wenye choo kisafi ni jinsi asilimia 95% ya vyoo vyote vya umma TANZANIA ni vichafu?
Na habari yenyewe ni :
WATANZANIA ndio wanaongoza kwa KUUA MAALIBINO.:-(
Kama weye ni MBONGO mshangiliaji Wabongo kwa kuwa ni WABONGO ,SHANGILIA na hilo SASA tukuone!:-(
[Nyoooo a.k.a bonge la msonyo!]


Kumbuka hili ni wazo tu MHESHIMIWA.


Hebu twende Sudan Emmanuel Jal alete-War CHild



Au twende Somali K'naan alete-The DUSTY FOOT PHILOSOPHER

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP