Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

LADHA!

>> Tuesday, December 29, 2009



Kuwa na LADHA,...
... ni uwezo wa kustukia kitu BORA, kwa kuwa unajua ni nini UBORA.


Lakini LADHA,....
....ni UTAMU hata wa ile CHACHU isiyo BORA.:-(


Ladha,...
... ndio IUAYO watu KWA HIARI kwa kuwa tu wamejizoesha ladha ,...
....ya UTAMU wa visivyo BORA.:-(


Kizuri na kibaya katika LADHA,....
... kwa bahati mbaya HUFUNDISHIKA kama tu afundishikavyo MTU kujua ni viatu gani BORA.


CHAKUSIKITISHA kuhusu LADHA,...
...ni kwamba mengi ambayo WATU huangaikia kufudhu KATIKA ujuaji wa LADHA ,....
.... ili waipende LADHA,...

.... mara karibu zote kwao hayo si BORA.:-(








Swali:

  • Unafikiri una LADHA?

  • Si unajua adhaniaye ladha ya CHAI YA SUKARI ni tamu anafundishika kupenda ladha ya CHAI BILA SUKARI hasa akistukia chai isiyo na sukari ndio BORA?

  • SI unajua apendaye LADHA ya ASALI anafundishika kupenda ladha ya BIA?


  • Si unajua MUME au MKE apendaye ladha ya jamii kuhusu NDOA aliye kwenye NDOA anafundishika kupenda ladha ya MAPENZI YA KULIPIA ya MALAYA?


NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA na Usikonde!:-(



Hebu katika kubadili somo tusikilize Chef akiulizwa swali -Chef what's a prostitute?




Au tu TONY TUFF alete ustaarabu kijiweni kwa kitu- Mix ME Down

7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Said Michael 7:26 am  

Duh! Kamanda kweli unaona mbali, mada zako ni rahisi kusoma na unaeleweka vizuzi. Ladha ya uandishi unayotumia kufikisha ujumbe imetulia sana Mkuu.

Simon Kitururu 11:53 am  

@Mkuu Said Michael: Asante Mkuu!

Lakini kuna watu kibao pia huwa hawaelewi naongelea nini .:-(

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! 11:58 am  

@Mt. Simon: yawezekana nkawa mmoja wao hasa ninapofikiria UTAMU wa pilipili. Hivi huwa ni upi hasa mpaka unapostukia kuwa nyamachoma haina ladha bila pilipili? ;-)

ni vijimambo tu mkubwa....lol!

Yasinta Ngonyani 11:09 pm  

nanukuu "Unafikiri una LADHA?" mwisho wa kunukuu. Sijui ka najua nina ladha gani:-) Na nafikiri sijua kama kuna anayejua hili.

chib 12:38 am  

Kila kitu kina ladha yake. Ukienda kwa wakorea wakikuadithia utamu na ladha ya konokono unaweza kuachia ugali uliomaliza kula muda mchache uliopita, ilhali ukikutana na mama mjamzito aanze kukuelezea utamu wa udongo wa kichuguu.....

Faith S Hilary 2:47 am  

kilichokuwa akilini mwangu ni kama alichosema kaka chib. Na mmh...nina ladha kweli...sijui!!

Chef, what's prostitute?
Chef, its a nice day isn't it?
Chef, what's a prostitute? HAHAHAHA!

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! 10:24 am  

@Yasinta: mwenye kujua ladha ni mwenye kuonja..je hujamuuliza mwenye kukuonja?...lol

Una uhakika hujui ladha ya dawa hata kama weye si mgonjwa....? lol

Angalizo: kuonja si lazima iwe vile ufikiriavo ama vipi mkubwa SK?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP