Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MNONG'ONEZO kwa APOKEAYE au afanikiwaye kutarajia ZAWADI!

>> Thursday, December 24, 2009

NI KWELI,....


.....WAUNGWANA hudai ZAWADI ni kitu chochote,...


.....INGAWA waungwana WASICHOSEMA ni kwamba,...


...hata VISIVYO KIUNGWANA wakipewa MAVI hawaiti au hawataita MAVI zawadi,.....:-(





Swali la KIUNGWANA:
  • Unauhakika aliyepewa zawadi huwa mara zote hustukia hiyo sio ZAWADI?

  • Si unakumbuka kuna WENZETU kule TANZANIA watokao katika MAENEO YA MADINI kama ALMASI walitoa ALMASI kwa zawadi ya PIPI?

  • SI kuna machifu waliosaidia maeneo yao yachukulliwe na WAKOLONI kwa zawadi ya ZE WHISKEY?

  • Si unakumbuka katika awezavyopewa mtu vingine ni LAANA hata kama sio MAVI?

  • Unafikiri zawadi yako sio kujidhalilisha UTU wakati ufikiriacho ni kwamba unamzawadia tu mtu UCHI?



NDIO,...
......Haki ya nani sikubishii kama wewe ni miongoni wa waaminio kuwa ZAWADI ni ZAWADI,...
.....na KUTOONA kuwa,....

..... mara kibao SIO ZAWADI ndio ZAWADI!:-(




NI wazo TU hili MHESHIMIWA na NIMELIACHA,....

...... ingawa NI MATUMAINI YANGU waweza kulikumbuka wakati UNACHEKELEA UDHANIACHO upewacho ni ZAWADI!:-(




MWISHO wa TARARILA .


Au ngojea Tantra ZAWADI atupe zawadi ya -``GIRL´´

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MARKUS MPANGALA 5:33 pm  

tatizo zawadi zinaumwa...na kila zawadi kumkbe ni Lifti tu kama baiskeli,bajaj, au pikipiki. lakini mtu akinyimwa zawadi si ananung'unika? ipo kazi hapa mtakatifu...ni maisha na falsafa ndani ya neno

Yasinta Ngonyani 10:36 pm  

DUH! hapa ipo kazi!! heri ya krismas Mtaka-tifu:-)

Simon Kitururu 4:03 am  

@Mkuu Markus: Kunungunika wakati unapokea zawadi inasemekana ni kipimo tu cha jinsigani zawadi ni tamu.

@Dada YAsinta: Asante Dada Mpenzi!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP