Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Sababu CHACHE zinyambulishazo: `` KWANINI wakati WENGINE wanatukana kwa SAUTI wewe ULIMUMUNYA TUSI!´´:-(

>> Sunday, December 13, 2009

Kila MTU HUBANWA haja ya KUTUKANA ingawa LABDA SI kwa mfululizo NA UNGANGARI WA HAJA kama ule wa kubanwa HAJA ya kwenda MSALANI.:-(


Kikubwa kisababishacho mara nyingi hutukani tukasikia,...
... au huandiki TUSI tukalisoma na kujua ni WEWE ulioliandika,...
... ingawa WOTE tunajua unajua MATUSI na unatukana hata kimoyomoyo NI:


  • Kwanza : HUJAZOEA kutukana HADHARANI.
  • Pili: HUJACHUKIA VIZURI mpaka ukafikia kutojali ukitukana WATU WENGINE watafikiria WEWE NI MTU WA AINA GANI.

  • Tatu: labda bado unatukana ila WANAOTUKANWA hawajastukia usemacho ni TUSI.

  • Nne: HAUKO HURU TU.

  • Tano: weye HUPATII tu tusi UKITUKANA.
  • Sita: Wakati unafundishwa SWALA ZIMA la kujiheshimu ULIELEWA SANA SOMO.


NAKATIZA wazo!

Swali:

  • Si unajua ukubwa wa TUSI unategemea na uelewaji wa ATUKANWAYE TUSI?

  • Si unakumbuka akutukanaye tusi la nguoni na anaye kutusi KICHWA kama KOPO wote wanaweza wakawa katika UJAZO WA TUSI ngoma sare ingawa wewe kwa kuwa unajihisi unabonge la chogo waweza kuchukia zaidi ukitukaniwa kichwa kuliko SEHEMU ZA SIRI ZA WAKO MZAZI?

NI wazo tu hili MHESHIMIWA na NIMEACHA.

Hebu twende kidogo MSUMBIJI , GRUPO NYERERE wasawazishe kama hivi..



Au tu ABETI MASIKINI alete -SUMIKE

6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mija Shija Sayi 2:33 am  

Samahani Kitururu, wewe katika maisha ya kawaida unapenda kusoma vitabu gani?

Simon Kitururu 7:47 am  

@Da Mija: Napenda kusoma vitabu sana. Kuanzia Biblia , Korani mpaka vitabu vizungumziavyo watu niwazimiao.

Sasa hivi namsoma Barrack Obama katika kitabu Dreams from My Father na sijui kwanini nimechelewa hivi kukisoma ingawa nilikinunua muda mrefu sasa.:-(

Wewe unapendelea vitabu vya aina gani?

Mija Shija Sayi 11:26 pm  

Kwa kweli mimi si msomaji sana wa vitabu, ila na mimi sasa hivi nasoma kitabu hicho hicho cha Dreams from My Father, nikikimaliza naingia REPOSITION YOURSELF cha T.D JAKES. Natamani niwe msomaji mzuri wa vitabu lakini inaniwia ngumu, hivi kuna siri yoyote mnisaidie?

Simon Kitururu 5:39 pm  

@ Da Mija: DUh kumbe tunasoma kitabu kimoja!:-)



Mimi nimegawa usomaji wangu kwa aina mbili.

Wakati najisikia uvivu kusoma kitabu natafuta vitabu ambavyo vinazungumzia kitu nachokipenda.

Wakati na nguvu kisawasawa bila uchovu nasoma vitabu ambavyo vyaweza kuwa vigumu ila vyenye vitu navyotaka kujua.


Na siri ya Kusoma kwangu au hata kuandika ambayo naamini inanisaidi kuliko vyote ni kuanza tu kufanya hilo[Kusoma kama na cha kusoma au kuandika kama na chakuandika] bila kufikiria sana kitu kiwezacho kunitia uvivu .

Mija Shija Sayi 4:01 pm  

Umenipa nguvu, naomba nikuige ili nami niwe msomaji mzuri.

Stay blessed.

Simon Kitururu 3:41 am  

@Da Mija: Nashukuru kama imesaidia swala kiduchu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP