MFANYAKAZI na MFANYIWAKAZI wakati inasadikiwa KWA WOTE KAZI ni tamu!
>> Wednesday, December 16, 2009
Kila mtu hata kabla hajazaliwa HUANZA kwanza kufanyisha watu KAZI.:-(
Na akizaliwa tu  MTU  huendeleza kufanyisha watu kazi  ,....
... na miongoni mwa moja ya KAZI ZA KWANZAKWANZA aitoayo MTU kwa watu ni ile ya KUCHAMBWA a.k.a KUBADILISHWA NEPI yenye choo laini na ujazo fulani wa mkojo , na kumbuka kazi hiyo ya KUCHEZA na KINYESI mhusika TOTO huitoa bila kujali kuwa apewaye hiyo shughuli kwake ni KAZI.:-(
Swali:
- Sasa umegundua ni wapi akupaye kazi bila KUJALI unajisikiaje alitoa wapi hiyo hulka ?
Na ni baada ya miaka MICHACHE tu baadaye MTOTO aliyeingia duniani huanza naye kufanyishwa KAZI,.....
..... ingawa kazi za MWANZOMWANZO ni kama tu zile za kusakiziwa kwenda mlangoni MTU AKIGONGA HODI  ili kudanganya `` MAMA KANIAMBIA KUWA  niseme WENYE NYUMBA HAWAPO!´´ yote ikiwa ni moja tu ya shughuli  na mafunzo ya mwazomwazo HATA YAKO  ya KUDANGANYA KAZINI  hata kabla hujafikiria ya kulipwa mshahara KAZI.:-(
NDIO , ni muhimu KAZI,...
..... lakini kwenye kazi kuna WATENDEWAO kazi.:-(
Na katika KAZI,....
.... tukumbuke kuna MFANYAKAZI ambaye kuridhika kwake kuko katika kufanyia WENGINE KAZI. :-)
Lakini pia katika KAZI,....
.... kuna WAAJIRIWA ambao ingekuwa BOMBA a.k.a BORA sana wangekuwa wao ndio WAAJIRI wa watu katika AJIRA a.k.a hizo KAZI.
Na  KWA BAHATI MBAYA mara kibao katika tuzifanyazo kazi ,.....
....tunazifanya tu kwa kuwa hatufikirii tunamfanyia nani kazi.:-(
 Swali: ....tunazifanya tu kwa kuwa hatufikirii tunamfanyia nani kazi.:-(
- Unauhakika humfanyiii adui yako au  tu MHESHIMIWA SHETANI ufanyayo hiyo KAZI?
- Si unajua wengi wawaajirio watu ni NYOKO?
Na haki ya nani inazingua yoyote uifanyayo KAZI,...
.... hasa kama wewe ni miongoni mwa ambao  hunogewa zaidi KUAJIRI watu wengine a.k.a KUFANYISHA WENGINE KAZI  kwa kuwa unajijua ni mbunifu zaidi  wa kazi na kwa sababu MOJA MBILi huwezi hata mwenyewe kuanza kwa KUJIAJIRI MWENYEWE kazi.:-(
Na nikiongea kama MTANZANIA  kuhusu kazi,...
.... naweza kukuambia kuwa elimu ya TANZANIA mara karibu zote hulenga tu kumjenga MTANZANIA asijiajiri  kwa kuwa inalenga kumuandaa kujisikia inabidi AAJIRIWE MAENEO siku akihitaji KAZI.:-(Na ukichunguzaTanzania utastukia wengi wajiajirio kuanzia kwenye KILIMO vijijini mpaka mijini KIKAZI,...
.... wengi wao ni wale wenye sifa  AMBAZO KWAKO  NI za kuwa hawakwenda sana SHULE KAMA WEWE ULIYEAJIRIWA NA UNAMSHAHARA BONGE LA MSHIKAKI , na kwa HILO unaamini ilibidi  walazimike KUJIBUNIA KAZI.
Swali:
- Unabisha?
- Lakini si unakumbuka ajibuniaye kazi leo akifanikiwa kesho anaweza kuwa muajiri WAKO?
MFANYAKAZI na MFANYIWAKAZI,....
,..... ni kweli wote labda KWAO ni tamu KAZI.
,..... ni kweli wote labda KWAO ni tamu KAZI.
Lakini kama unafanyishwa KAZI,.....
.... ingawa nia  YAKO IFANYAYO UFANYISHWE KAZI labda ni MSHAHARA au hata STATASI a.k.a MSHEBEDUO ukuwezeshao KUJISHEBEDUA kuwa wewe ni kiboko kwa kuwa UMEAJIRIWA na UNAKAZi,....
...... LABDA fikiria pia hivi kikweli unafanyanini katika hiyo kazi na kikweli unamfanyia nani hiyo KAZI.:-(
TUNAJUA,...
.....katika kazi za unyumba chumbani   WATOTO WAKILALA ni rahisi kujua unamfanyia nani kazi,....
.... au ni nani mvivu katika kukufanyia kazi KAMA NI YA ufundi wa  tendo la ndoa ndio KAZi.
Lakini  ulimwenguni  KIKAZI,......
... unaweza kujikuta wakati unafikiri unafanyiwa kazi IKAWA UKWELI wenyewe ni wewe UFANYISHWAYE KAZI.:-(Na ina weza PIA ikawa UNAFIKIRI ni kwa ajili tu ya mshahara ndio maana UNAFANYA KAZI!
KWA BAHATI MBAYA  ,....
.....ukweli wenyewe unaweza kuwa hata kwa utulivu wa UBONGO WAKO tu bila hata kuhitaji mshahara WEYE unahitaji KAZI.:-(Swali:
- Unafikiri ni kweli unaweza kuishi bila kazi ?
NAKATIZA WAZO KIDUCHU!:-(
Hebu KEM alete tena-WHEN LOVE CALLS[REMIX - Ft FLOETRY]
Floetry walete- Fantasize
Floetry walete -Floetic
Au tu Faith Evans amalizie kwa -Mesmerized
 
  
 Posts
Posts
 
 




2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
inafikirisha hii kazi
@Komandoo Kamala: Si utani!
Post a Comment