Wakati MWENZIO Mpenzi MAULANA ana HAMU,....
>> Saturday, December 26, 2009
...... wote TWAJUA sio lazima na WEWE wakati huo uwe na HAMU.:-(
Ila HAMU yako ikistukiwa na  MTU  yawezapandisha mtu HAMU!
Ila HAMU yako ikistukiwa na MTU yawezapandisha PIA kinyume cha HAMU YAKO mtu!:-(
Ila HAMU yako ikistukiwa na MTU yawezapandisha PIA kinyume cha HAMU YAKO mtu!:-(
Na IKIWA tatizo NI huruma YAKO kwa MWENYE HAMU,...
.....ndiyo ikufanyayo UFIKIRIE ili umtibu HAMU ZAKE  mwenye hamu ,....
...inabidi UJIANZISHIE au  KUJIPANDISHA yako hamu ili uwe kama MWENYE HAMU,...
.... huyo MWENZIO utakaye KUMTIBU au TU kumuigilizia kuwa na HAMU,....
...waweza kumtesa MWENZIO kwa kumpa matumaini  UTAPANDWA HAMU  kwa kuonyesha dalili unajitahidi kupandisha HAMU ,....
... HASA kwa kuonyesha JUHUDI zako  za KUJIPANDISHA HAMU,...
.....halafu  UKASHINDWA kufanikisha KUJIPANDISHA hamu,......IKADHIHIRIKA , hasa kama ULIMUONYESHA kuwa nia yako ilikuwa NAWE UPANDWE NA HAMU ili KWA PAMOJA msaidiane KUZITIBU KWA PAMOJA zenu HAMU.:-(
NDIO,...
....hamu kibao za watu HASA ZA ``KUNA - NIKUKUNE a.k.a TUKUNANE´´ siri ya TIBABU inaaminika ni ushirikiano wa PAMOJA wa WENYE HAMU katika kuzitibu HAMU.
NDIO,...
....sio wote HUPANDWA na HAMU kwa kustukia tu MWANAKWETU una HAMU.:-(
NDIO,....
... Kuna wachukizwao na hata KUONDOKWA na HAMU wakistukia tu Mwanakwetu UNA HAMU.:-(
Na YASEMEKANA moja ya KOSA tufanyalo  SIYE watu ni kutia moyo watu kuwa katika tibabu lao la HAMU nasi kwanza tutapandwa  HAMU kabla ya kuwatibu yao HAMU.:-(
Na kwa bahati mbaya INASEMEKANA katika KUMTIBU MWENZIO hamu zake wakati wewe mwenyewe huna hamu ,....
....mchezo MZURI hata wa matusi HUWA HAUNOGI na waweza hata kumuumiza asiye na HAMU.:-(
Tukiachana na kucheza na maneno:....
....Siriasli a.k.a Swali KIDUCHU:
- Ushawahi kupandishwa hamu ya kitu hata kama ni hamu ya kucheza netiboli kisa umeshuhudia umzimiaye apandwavyo HAMU a.k.a mzuka wa Netiboli?
- Kwani HUJUI MAFANIKIO YA WENGINE kuna YAWAFANYAO waingiwe na HAMU ya KUFANIKIWA lakini pia kuna YAWAFANYAO watake KULOGA MTUHUYO ALIYEFANIKIWA kwa kuwa tu AMEFANIKIWA?
- Ukistukia MWENZIO anahamu kwani kila mwenzio au kila wakati ushuhudiao hicho weye hupandwa hamu?
- Kwani ukistukia hamu ya mwenzio ya MCHICHA huwezi pandwa hamu ya MISHIKAKI?
NI wazo tu MHESHIMIWA HILI na RUKSA KUTOLIELEWA ingawa  SHUKRANI ZA DHATI kama   likikufanya ufikirie KITU.:-(
Ngojea St Germain wabadili hali ya hewa kwa kurudisha KITU CHA UHAKIKA au tu - SURE THING
 
  
 Posts
Posts
 
 




0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment