Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Labda NIKIKUA sitaki kuwa kama MIMI!

>> Wednesday, December 02, 2009

Na nikikua labda sitaki kuwa kama WEWE,...
......Wewe uninyosheaye kidole kwa kuwa unaona kasoro yangu ya kuwa MIMI.


Lakini nikikua labda pia nataka kuwa kama WEWE,...
.....Wewe ambaye kwa usifiwayo natamani asifiwaye hayo ingekuwa MIMI.:-(


Lakini nimekua na MIMI si WEWE,...
...Kwa hiyo wakati unanikosoa kumbuka kuwa WEWE sio MIMI.

Swali:
  • Lakini si unakumbuka ndani ya mtu umjuaye asifiwaye asifiwalo linaweza likawa ni moja tu ambalo linastahili sifa?
  • Si unajua ukizaliwa na kuishi ufukweni kuna uwezekano kirahisi utajua kuogelea na labda kujua kwako kuogelea na kumzidi yule malaya wako wa dodoma kusiko kuwa na bahari hakustahili sifa?

  • Unafikiri katika BINADAMU walio hai wangekuwa na chaguo kabla ya kuzaliwa, kuna ambaye angechagua kuzaliwa kama yeye huyuhuyu aliyehai?
NI WAZO TU HILI MKUU!


Hebu CHICCO TWALA abadili kwa kitu kisababishacho baadhi ya watu wasifiwe ambacho ni-Money

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP