Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Heshima za MAMA WATOTO kwa MUME WAKE ikifikia zinafanana sana na za BINTI ya MAMA WATOTO HUYO katika kumheshimu BABA WATOTO!:-(

>> Friday, December 18, 2009






Swali:

Heshima za BINTI na MKE si zinatakiwa zitofautianE?





Katika UNYUMBA,....

... heshima za MAMA WATOTO zikizidi HASA zile zifananazo au kucheza karibu na za :
`` SHIKAMOO BABA WATOTO´´,...

..zaweza kumfanya BABA WATOTO atafute huduma ya heshima za MAENEO au tumizi la ENEO zifananazo na zile za MALAYA katika tu kujaribu kujazia ladha ya afikiriao ni utamu ahitajio kuupata kutoka kwa MAMA WATOTO .:-(


Swali:
  • Ushawahi kuchunguza ni nini kitofautishacho utamu wa kimada KWA MWENYE MKE ukiufananisha na utamu wa MKE WAKE?
  • Unafikiri katika kukidhi KUHESHIMIWA unapatia HITAJI LA KUHESHIWA kwa utakavyo KUHESHIMIWA?

Kumbuka:
Katika heshima hata kama INZI na MBU wote wanastaili heshima,...
... heshima ya INZI si lazima ndio ahemiwavyo MBU.:-(



Na kwa kuwa watu wanalazimisha HESHIMA iwe ya aina moja ndio maana kuna waheshimuo MBWA kama tu wawaheshimuvyo WATU ,....
......na hapa siongelei WAZUNGU.:-(



Nikirudi katika KISIMI cha HOJA;....

HESHIMA za MAMA WATOTO zikifanana sana na za BINTI ya MAMA WATOTO,.....

.... utamu wa CHIPSI MAYAI ya KIKUBWA apewayo BABA WATOTO na MAMA WATOTO katika ladha ni kawaida kwa mwenye mapenzi ya chumvi , ....
......HIZO CHIPSI hazina CHUMVI.:-(


Na HESHIMA adaizo BABA WATOTO zikizidi kumfanya MAMA WATOTO amfananishe BABA WATOTO na MWALIMU MKUU AOGOPWAYE yule wa SHULE YA MSINGI alikosomea MAMA WATOTO,...


... utamu wa CHIPSI MAYAI wa KIKUBWA atakazozipata MAMA WATOTO kirahisi kwa MAMA WATOTO hizo chipsi hazitakuja na KACHUMBARI na katika ladha yake kwa MAMA WATOTO apendaye ya chumvi,.....

......kirahisi kikosekanacho kwenye ladha itakuwa ni CHUMVI.:-(

Swali:

  • Ukiwa huna chumvi nyumbani ushawahi kutamani kwenda kuomba ugawiwe dawa ya jiko a.k.a CHUMVI nyumba ya jirani?
  • Kwa kuwa unathamini sana HESHIMA kwa hilo hudhani hukosei na KUANZA KUCHANGANYA HESHIMA ndio maana labda umuheshimuvyo MTU ni vile ulivyohitajika kumuheshimu JOGOO mchumba wa KUKU au tu MBWA?

NIMEACHA wazo na MHESHIMIWA kumbuka hili ni WAZO TU na ni ruksa KUTOELEWA kwa hiyo usikonde MKUU!

Nakutakia IJUMAA na WIKIENDI KIBONGE Mheshimiwa!



Basi kabla sijaanza kivyangu labda tutulize wazo kwa kutingishiwa tena kidogo tako kama...

Au tu baadhi wacheke katika ...



BAADAYE BASI mungu akipenda MHESHIMIWA Othrong'ong'o!:-(

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 10:49 am  

Darasa la leo ni ngumu kidogo kwangu:-)

Simon Kitururu 10:58 am  

@Dada Yasinta:

Kuna uwezekano mkubwa SIELEWEKI katika hili.:-(


Kwa kifupi darasa linaangalia swala la :

Pamoja na kuwa na Heshima , je unatofautisha heshima uumpayo Baba watoto wako na Heshima imfaayo Baba yako Mzazi?

Na hudhani achanganyaye heshima imfaayo BABA MZAZI na kumpa hiyo Baba watoto kuna jambo litachanganya chumvi na sukari katika ladha ya apendaye sukari?

Mija Shija Sayi 2:14 pm  

Hata mimi nitarudi baadaye nisome kwa nafasi filosofia hii ya leo.

Ila video za leo zimenichana mbavu duh!

Koero Mkundi 6:31 am  

Kama hujua mambo ya matusi itakuwa ngumu kumuelewa Kitururu

Simon Kitururu 11:18 pm  

@Da Mija: :-)


@ Dada Koero: Sasa nini jamani unanitolea siri yangu hadharani? Ntakushika kibindo weye , WEYE SHAURI YAKO ! :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP