Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UTUMWA wa MTU wa: `` Ni nini watu wengine WANAMTEGEMEA awe.´´:-(

>> Tuesday, December 15, 2009

Kirahisi,...

.... hata kabla MTOTO hajazaliwa KUNA AMBAVYO kuna WATU wanategemea AWE.


Kirahisi,....
.... baada ya MTOTO kuzaliwa KUNA AMBAVYO vinaendelea ambavyo KUNA WATU wanamtegemea mtoto aendelee KUWA au tu hapo baadaye AWE.

Na kirahisi,...
.... MTOTO HUYO akishakuwa MTU MZIMA atajikuta mwenyewe anaendelea KUFUNGWA katika UTUMWA wa ambayo KAFUNZWA kuwa ndio tegemeo hasa ,.....
... hasa kama kajikuta kajifunza kuhitaji hata ikiwa ni KUHESHIMIWA TU na kwa HILO kujifunga katika taratibu za walimwengu AMBAZO inabidi MTUMWA awe.:-(



Chakusikitisha kirahisi,....
.... Hata HUYO mtu akifunzwa kujiandaa kufa BADO mafunzo hayo yanaweza kumfanya afe MTUMWA kwa kuwa hata AKIFA kuna wamtegemeao baada ya kufa ni wapi aende au tu AWE.:-(


Swali:

  • Unauhakika NDUGU, MARAFIKI au hata MALAYA wako hawakufanyi MTUMWA kwa kutegemea uwe MHESHIMIWA?

  • Unafikiri wewe sio MTUMWA wa tu WATU WENGINE wa jinsi uhisivyo wanategemea UWE?


NI WAZO tu HILI MKUU!


Hebu Lord Kitchener abadili kwa kudai-If you're not White, you're Black


Au tu Lord Kitchener azungumzie tena matibabu katika -Dr Kitch


Lord Kitchener arudie- Sugar BUMBUM


Samahani nimenogewa namuachia tena LOrd Kitchener arudie-Pillow Fight na Kaka Roach






NIMEACHA nadhani ukijua tayari leo back ground manyanga a.k.a MUZIKI kwangu kunyumba ni Soca na Calypso!:-(

7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

chib 5:39 pm  

Wazo hilo lilikuwa halijanijia akilini mwangu. I salute you!!

Simon Kitururu 5:58 pm  

@Mkuu Chib: Asante! Na asante nyingine lukuki kwa kutochoka kunitembelea hapa Kijiweni.

Yasinta Ngonyani 7:48 pm  

wazo zuri ambalo wengi hatuwazi hivi hongera kwa kuwaza hivi!!!

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! 8:54 am  

hili nalo neno....lol

na unadhani wazazi wako hawakutegemea uwe mtumwa wa kichwa bila nywele kama Flaviana Matata ilihali ukaamua kuwa mtumwa wa nywele kama za Yasinta?...lol

Utegemezi na utumwa....duh!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 11:19 am  

utumwa, vifungo tunavyovingi. wengi wanapongeza lakini inahitaji kujikagua nakushika mienendo mipya.

hata mimi nimtumwa wa kufunga ndoa. unadhani nashindwa nini mpaka nifunge ndoa?

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! 12:34 pm  

@KL: hicho ulichoshindwa ndicho kilichokulazimisha uingie katika utumwa wa kufunga ndoa....lol

yawezekana ikawa ni kwamba umekuwa ntumwa tayari wa 'pendo lililomdondokea nkeo'....lol

Simon Kitururu 3:18 pm  

@Dada Yasinta: :-)
@Kadinali Ng'wanambiti: :-)
@Komandoo Kamala: Mmmh!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP