Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Labda ZOEZESHA WATU mara kwa mara kwa KUJAMBA KIDOGO kama unauhakika mbeleni UTAKUNYA!:-(

>> Friday, December 04, 2009

[Tahadhari: Tararila hii INA dalili za tisha toto!]


Binadamu kama ujuavyo wanatabia MBAYA,...
..... na kwa hilo pamoja na yote WAJUAYO cha AJABU BADo wanahitaji jambo moja tu ambalo hawakuhusianishi nalo likutokee ili WASAHAU MENGINE YOTE YAKO na kukumbuka WEYE kwa hilo.



Kwa hiyo kama wewe sifa zako ni BONGE la MLOKOLE/Mswahilina na ni kweli hauna tabia MBAYA,.....

.....kumbuka JINSI BINADAMU a.k.a MTUZ zilivyo NA TABIA MBAYA,.....

... inahitajika unadakwe KWA KITU KIMOJA TU au mara moja TU, - kwa mfano ukitokea gesti hata ya SHANGAZI YAKO WATU WASIOMJUA waishio machangudoa- WAKATI WEWE ni kweli SIO CHANGUDOA ,- au tu UDAKWE kwenye picha na KIDEO mara moja tu ILE uliyoingia majaribuni ,- ILE SIKU AMBAYO kwa jitihada zako za kutaka uolewe ikabidi UAMUE KUKUBALI uonjwe kidogo na lijamaa mara moja TU kwa kudhani KWA HILO utaharakisha ndoa kwa KUMUONJESHA shemeji yetu mtarajiwa( akilini mwako) huku ukijipa moyo utatubu baadaye akichukua jumlajumla ........

.....na kwa bahati mbaya NI HILO TU laweza HITAJIKA na kutosha - ili MTAA MZIMA ubadili mtazamo na kukuona mwanakwetu ni BONGE la MALAYA wakati UKWELI WENYEWE WALA SIO HUO na ni kweli weye bi BONGE LA MCHOYO na kwa UNYIMI jamii isiyothamini MCHANGO WA KUJENGA TAIFA wa WAGAWAJI ingebidi hata IKUPE MEDALI kwa hilo.:-(

Swali:

  • Au?
Lakini,....

...kumbuka kuna watu wenye roho mbaya waliofanya jambo moja tu kwako jema uwakumbukao kuwa ni wenye ROHO NJEMA halafu KIBONGE.
Lakini ,....

....kumbuka kuna watu wengi wema na kwa bahati mbaya ulipokuwa na hitaji kubwa KWAKO ndio siku walikuwa hawana ingawa wanajulikana kwa kuwa nalo TIBABU LA HAJA YAKO HATA YA UPUPU - na hilo moja mara moja ndilo likufanyalo uwaoanishe na ROHO MBAYA halafu KIBONGE.:-(


Sasaaaaaaa!
Swali:
  • Unafikiri labda kama unajulikana KWA KUTOKOSEA , -Hivi si vizuri kuwazoesha watu kwa kukosea kidogokidogo mara kwa mara iliwasishitushwe ukifanya bonge la kosa?

  • Kwa hiyo umenielewa sasa namaanisha nini nisemavyo kama unajua KIBINADAMU ipo siku utakunya ni vizuri kuzoeza watu kwa kujamba kidogo KWA ADOADO mara kwa mara?
  • Unafikiri stori ya Tiger WOODS kuonja nje ya ndoa ingekuwa kubwa sana kama angejulikana kuwa pamoja na sifa zote ZA APATIAYO bado anakasoro tu kama andunje wowote wengine?



NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA!



Hebu Fela Kuti aendelee kwa-Army Arrangement



Au tu Fela Kuti alete na -Fear not For Man

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP