UTUMWA wa MTU wa: `` Ni nini watu wengine WANAMTEGEMEA awe.´´:-(
>> Tuesday, December 15, 2009
Kirahisi,...
.... hata kabla MTOTO hajazaliwa KUNA AMBAVYO kuna  WATU  wanategemea AWE.
Kirahisi,....
.... baada ya MTOTO kuzaliwa  KUNA  AMBAVYO vinaendelea ambavyo  KUNA WATU wanamtegemea mtoto aendelee KUWA au tu hapo baadaye AWE.
Na kirahisi,...
.... MTOTO HUYO akishakuwa MTU MZIMA  atajikuta  mwenyewe anaendelea KUFUNGWA katika UTUMWA  wa ambayo KAFUNZWA kuwa ndio tegemeo hasa ,.....
... hasa kama kajikuta  kajifunza kuhitaji  hata ikiwa ni KUHESHIMIWA  TU na  kwa HILO  kujifunga katika taratibu za walimwengu  AMBAZO inabidi MTUMWA awe.:-(Chakusikitisha kirahisi,....
.... Hata HUYO mtu  akifunzwa kujiandaa kufa BADO mafunzo hayo yanaweza kumfanya afe MTUMWA kwa kuwa hata AKIFA kuna wamtegemeao baada ya kufa ni wapi aende au tu AWE.:-(
Swali:
- Unauhakika NDUGU, MARAFIKI au hata MALAYA wako hawakufanyi MTUMWA kwa kutegemea uwe MHESHIMIWA?
- Unafikiri wewe sio MTUMWA wa tu WATU WENGINE wa jinsi uhisivyo wanategemea UWE?
NI WAZO tu HILI MKUU!
Hebu Lord Kitchener abadili kwa kudai-If you're not White, you're Black
Au tu Lord Kitchener azungumzie tena matibabu katika -Dr Kitch
Lord Kitchener arudie- Sugar BUMBUM
Samahani nimenogewa namuachia tena LOrd Kitchener arudie-Pillow Fight na Kaka Roach
NIMEACHA nadhani ukijua tayari leo back ground manyanga a.k.a MUZIKI kwangu kunyumba ni Soca na Calypso!:-(
 
  
 Posts
Posts
 
 




7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Wazo hilo lilikuwa halijanijia akilini mwangu. I salute you!!
@Mkuu Chib: Asante! Na asante nyingine lukuki kwa kutochoka kunitembelea hapa Kijiweni.
wazo zuri ambalo wengi hatuwazi hivi hongera kwa kuwaza hivi!!!
hili nalo neno....lol
na unadhani wazazi wako hawakutegemea uwe mtumwa wa kichwa bila nywele kama Flaviana Matata ilihali ukaamua kuwa mtumwa wa nywele kama za Yasinta?...lol
Utegemezi na utumwa....duh!
utumwa, vifungo tunavyovingi. wengi wanapongeza lakini inahitaji kujikagua nakushika mienendo mipya.
hata mimi nimtumwa wa kufunga ndoa. unadhani nashindwa nini mpaka nifunge ndoa?
@KL: hicho ulichoshindwa ndicho kilichokulazimisha uingie katika utumwa wa kufunga ndoa....lol
yawezekana ikawa ni kwamba umekuwa ntumwa tayari wa 'pendo lililomdondokea nkeo'....lol
@Dada Yasinta: :-)
@Kadinali Ng'wanambiti: :-)
@Komandoo Kamala: Mmmh!
Post a Comment