Ila bado kuna ambayo huwazika zaidi CHOONI kwa kuwa,...
... ni rahisi kuyakumbuka ukiwa MSALANI.:-(
Swali:
Si unakumbuka kuna mambo unayakumbuka tu kirahisi ukiwa na NJAA?
Ndio,...
...kuna MAMBO ni labda ni mpaka UKIONA MGONGO ndio unakumbuka mfereji wa mwanzo wa TAKO au tu ni UKIONA kitanda ndio kikumbushayo hata ya MASHUKA bado MACHAFU ,...
....ingawa LABDA ni ukweli PIA kimawazo ya kitandani labda yanafanyika hata CHOONI kiwazo na wala tu sio kweli WAZO hilo lawazika tu huko MSALANI!:-(
NI hilo tu na NI WAZO tu hili MHESHIMIWA!:-(
Tutulize maswala na manyanga yasiyo na fujo kwa WATU wasiotaka FUJO kwa kubakia Brazil ili Gilberto Gil alainishe kwa - Estrela
Twende UFARANSA ili Henri Salvador arudie - Jardin d'hiver
Henri Salvador arudie-Jazz Méditerranée
Alainishe zaidi kwa - Chambre Avec Vue
Au turudi tu Brazil ili Elis Regina arudie- Madalena
... pamoja na kuwa KUNA wajifunzao KUDOKOA MBOGA WENYEWE bila kufundishwa na MTU,...
....au tu KUNA wale warekebishao mpaka JINSI YA KUSALI au tu STAILI ya kufanya MATUSI ili iwe sio MPAPASO kwa mafanikio kwa kuhangaikia hilo WAO WENYEWE,...
.... na kwa kurekebisha STAILI kwa KUJIFUNZA wao wenyewe kwa hata kwa KURUDIARUDIA mpaka kitendo HICHO kwa BINADAMU WENGINE washuhudiao kuwa lijamaa mpaka kwa kuuza MAAANDAZI linafanikiwa na kwa hilo lina cha KUADIMAYWA kama wale jinsi idaiwavyo WAMEJIFUNZA WENYEWE,....
.... labda BADO ukweli uko palepale kuwa MENGI ,...
..... watu hujifunza kutoka kwa WENGINE,...
.... na mengi wafundishayo WALIMU wa KITU ,...
... hayo walijifunza kutoka kwa MWALIMU wao hata wasio muita au kustukia ni MWALIMU.:-(
Swali:
Unabisha?
Kwani unafikiri WALIMU wengi hata tukiruka wale waliofundisha MTU kuvaa chupi huwa wanaitwa WALIMU?
Na siinasemekana asilimia kubwa ya MAISHA ya MTU - mtu huitumia kujifunza kitu hata kama hastukii anavyojifunza ?
Ndio,...
... labda MWALIMU ana MWALIMU.:-(
NI HILO TUna ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
Hebu WAZIRI wa UTAMADUNI wa zamani wa BRAZIL yule Gilberto Gil aanzishe upya kwa -Toda menina baiana
Au tu Gilberto Gil adinye tu na -Aquele Abraço Read more...
.... na kama ni wajinga utachelewa kujua kwa kuwa UREMBO ndio uustukiao.:-(
Kuna wajifichao nyuma ya HARAKATI,...
..... na wanachofanya ni kufanya uoanishe UTU wao na HARAKATI zao wakati wao kama WATU kuwa ni ambalo hawataki liwe ni jambo listukiwalo.
Na kuna wajifichao katika DINI,...
....na wanaweza kuwa wafanyalo ni kutumia DINI na hata MUNGU ili kukurusha kustukia yao BINAFSi ambayo yanatisha kama yakiwa ndiyo moja ya ambalo USTUKIALO
Kuna wajifichao nyuma ya KAZI,...
..... na ukitaka kuwaudhi ruka kutamka ni MAMENEJA wa kitu fulani kwa kuwa ukiondoa UMENEJA WAO na UONGOZI wao wa CHAMA labda hakuna lao BINAFSI kama WATU BINAFSi wajivunialo.:-(
Kuna wajifichao nyuma ya SHULE zao,...
.... na ni tusi kwao kutowaita MADAKTARI hata kama NI UDAKTARI WA KUPEWA kwa kuwa hicho ndio kithibitisho tu kuwa pamoja na yao yakijinga angalau waliwahi kwenda SHULE au wanaheshimiwa KISHULESHULE ingawa labda ni vigumu kwenye hilo kama ni BUSARA za USOMI wao ndilo kustukia ulengalo .:-(
Kuna wajifichao nyuma ya WATOTO , mme au WAUME zao,...
.... kwa kuwa yao ili wajisikie MAISHA yana maaana ni WAUME, watoto, WAZAZI au WAUME zao waaminikao kuna kitu wamefanikiwa ndio watakalo liwe listukiwalo.:-(
Swali:
Umeshawahi kukutana na mtu ambaye hatumii kitu KUJIFICHA nyuma yake ili angalau kukujengea jinsi UMTAFSIRIVYO?
Ndio,...
.... labda kila mtu kajificha nyuma ya kitu fulani ,....
... na ukijua ukweli juu ya MTU ,...
.....kiutu labda MALAYA ndiye MLOKOLE na MLOKOLE ndiye MALAYA !:-(
NI wazo tu hili MHESHIMIWA!
Hebu ghafla Loketo waingilie shughuli kwa -Extra Ball
...watu wengi wapendao kula nyama hawakuzaliwa na TESTI ya NYAMA bomba ILIYOIVA ,....
....kama tu ilivyokuwa ni kweli LADHA ya SUKARI kwenye chai ni yakujifunza tu kwa kuwa kuna SUKARI!:-(
Swali:
SI unajua CHAI inanyweka bila sukari na kama unatumia SUKARI kurembesha chai yako hilo ni jambo la kujifunza tu kama iwezekanavyo TU kwa aliyezoea chai ya sukari kujifunza kuinywa bila sukari?
Ndio,...
.... labda BINADAMU ni MWANAFUNZI by nature na hata tukiacha maswala ya LADHA,...
... ila labda pia hata mapenzi ya MATAKO na vyote vilivyomo kwenye TAKO ya BINADAMU mpenda MATAKO ni ya kujifunza tu pia ,...
..... na cha kutisha ni kwamba LABDA uwezo huo wa kupenda MATAKO anao hata BINADAMU ambaye kwa sasa sio MPENDA matako!:-(
Swali:
SI inasemekana karibu wengi wapenda BIA ilibidi wajifunze kupenda ladha ya BIA?
Ndio,... ....labda kuna SUKARI ,....
... ndio hasa kisababishacho ULIPATA NAFASI YA KUJIFUNZA LADHA na unajua ladha ya SUKARI ,...
....na kama kungekuwa hakuna SUKARI kama CHUMVI tu vile,...
... MSOSI unalika bila CHUMVI wala SUKARI!:-(
Swali:
AU?
SI inasemekana aliyezaliwa maeneo ya walao MBWA na PAKA ndiye rahisi kujua nyama ya paka ni tamu vipi?
Ndio,...
.... labda ukichunguza ,...
....utastukia mengi uyapendayo ,...
... umejifunzia tu kuyapenda UKUBWANI,...
...na kama usingejifunza ladha LABDA wala HAYANOGI!:-(
...... wengi TANZANIA kama wanamgao nanihii , na wanaaamini serikali yao inawatekelezea wayahitajio hasa KATIKA WAHISICHO NCHI YAO ndio itoacho na yenye UWEZO NACHO ufanyao maisha yao wakitaka kitumbua wanatumbua,..
...LABDA hawatajali GADDAFI anaibaje,...
-SAMAHANI! -
... namaanisha HAWATAJALI SANA viongozi wa TANZANIA wanaibaje ,...
... na LABDA kama tu CCM ingeweza kutoa KITUMBUA,... ....labda CHADEMA na CUF visingekuwa vyama visumbufu kwa kutoa tu stori za MAANDAZI -maandazi ambayo haVIjagawa bado.:-(
Na haki ya nani INASEMEKANA kwa aliyetibiwa HAMU vizuri si rahisi KURUBUNIWA na MTU kwa kutumia STORI TU za KITIBU HAMU kilichobenjuka tayari KIDUDE kama kionekanavyo KITAMU KATIKA STORI ZA WENGINE wadaio KINATIBU HAMU kuwafanya WARUBUNIWE na wawe na MUNKARI au tu hamu yaVITU ambavyo UWEPO wake bado ni STORI tu!
Swali:
SI inasemekana aliyeridhika na yake aliyo na UHAKIKA NAYO si rahisi kukubali kuhatarisha maisha yake yenye uhakika kwa kukimbilia ambavyo havina UHAKIKA na vyenye tetesi za hatari?
SI aliyeridhika kuwa MOTO unaunguza hahitaji kugusa MOTO ili kuhakikisha UNAUNGUZA?
Ndio nawaza tu ,...
... nafasi ya vyama vya UPINZANI kwenye siasa ya TANZANIA kama CCM ingekuwa inatimiza KWELI porojo za kwenye harakati za UCHAGUZI,...
...NA ni wazo tu HILI!:-(
....SAMAHANI ,...
...nabadili ndude,...
Hebu Main Street Singers wanipe msaaada kwa KUDINYA kitu.......-MUNGU NI PENDO
Ngojea ghafla Black Ice abadili mdinyo na KATIKA KUBADILI aongelee The music industry's exploitation of artists kwa kugusia ndude katika-Or DIE
Amir Sulaiman adunge nanihii - Spiting Truth
Au tu Notorious BIG aje tu na R.KELLY walainishe ZAIDI kwa kuongelea kula ngoma AMBACHO HAKI YA NANI NI KITU RAHISI yasemekana kwa wasioogopa dhambi au UKIMWI kwa ndude-Fuck U Tonight
Nahusudu SHAIRI hili la TAYLOR MALI ,...
.... ambalo nafikiri linadaka maswala ya fanyayoProf. Mbele, Mwalimu Nyerere,Mwalimu Kheri Kitururu,Prof. Matondo na Mtakatifu N.N. MHANGO ...
....bila kumsahau akaribiaye kufikia uprofesa MALKIORY .W. MATIYA enzi zake za KUTICHI na,...
...na WALIMU WENGINE wote WENGI niwaheshimuo ,...
...ni walimu na pia kuendelea kufanya kazi muhimu HII ya kufunndisha ya UALIMU ,...
....HEBU tudake tu mpekecho wake ki MADUNGURUDU .....
... na siamini PIA kuwa UN aka UMOJA wa MATAIFA ambao ni wenyepesa WAAMUZI ,...
....na WOTE wampigao GADDAFI wafanyavyo ni kwa ajili ya kulinda RAIA wa LIBYA wasiuawe na GADDAFIwakati tunaona wakaavyo kimya mahali pengine RAIA wakiuawa na kufanya mchezo wa Ze KUFA!.:-(
Just SAYIN'!:-(
Hebu tubadili WAZO ......
...kwa kupata mashairi zaidi,....
....na hebu ngojeaBLACK ICE aanzishe kwa ......
Black ICE asisitizie kitu kwa -Truth is
GEMINI asawazishe kitu kwa-What are you fighting for
Au tu Julian Curry azime manyanga kwa - Niggers , Niggas and Niggaz
MGUNO ni kiashirio kwa umpendaye kuwa afanyavyo vinakusikilizisha UTAMU.
MGUNO ni sauti katika kustuka.:-(
MGUNO ni TAARIFA hata KINYAMA kuwa inauma,...
.....kwa hiyo MGUNO ni MAUMIVU.:-(
KUGUNA ni kukataa!
MGUNO ni SENTENSI katika TAARIFA hata kama kimaandishi yawezachukuliwa KAMA sio sentensi.:-(!
Swali:
Unafikiri mara ya MWISHO ulivyoguna ulikuwa unamaanisha nini?
Kwani unafikiri ulistukia mara ya mwisho ulivyoguna au ni wengine LABDA ndio walisikia na kustukia uliguna kwa kuwa labda ni wengine ndio ambao wanajua nakusikia yako?
Ndio,...
...inasemekana kunakuguna bila sauti,...
......na hili ni WAZO tu MHESHIMIWA!:-(
Hebu Raphael Saadiq aanzishe tena upya- Good Man
Brick warudie - Fun
Ndio India Arie na AKINYELE wali sampo BRICKS katika biti hili ingawa AKINYELE anamatusi kama hivi kwenye BITI HILIHILI kikidude-Put It in Your Mouth
Wakati eti India Arie biti HILIHILI aliliweka mdomo safi katika-VIDEO
....hata MTU ajisahaulisheje kuwa HANA MATATIZO,...
... hakuondoi UKWELI kuwa ana hayo MATATIZO na haki ya nani tena MATATIZO kama YAPO ,...
....kujisahaulisha hakuondoi UKWELI matatizo HAYO utakayo kuyasahau BADO yako PALEPALE.:-(
Swali:
Si nasikia hata ulisifieje TOTO lenye sura kama MATAKO ya bata kuwa lina sura kama MALAIKA bado HAKUGEUZI UKWELI kuwa toto lenye sura kama matako ya BATA hilo lina sura kama MATAKO ya BATA na haki yanani tena kimuonekano halionekani kama MALAIKA?
Ndio,...
...labda hata ujisahaulishe vipi hata KAMA NI kwa hata KULEWA POMBE , elimu au hata kulewa tu DINI kama wafanyavyo WENYE DINI , wapagani, walokole na waswahilina katika kujaribu kujisahaulisha machungu ya DUNIA,...
.... labda BADO HUKO hakuondoi TATIZO aisee!:-(
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
Hebu King Sunny Ade abadili ghafla kwa -Oluwa No'o Jeun Kan / Sijuade
Notorious BIG abadili kabisa kwa-Suicidal Thoughts
Notorious BIG akumbushe-Niggas Bleed
Biggie Smalls aanze kulainisha kwa-Sky's The Limit
.......labda kiendeleacho hasahasa kama asemaye hilo/HUO MSEMO ni BINADAMU ni kuwa,....
.... hivyo ni ADHANIAVYO tu na idhaniwavyo tu na BINADAMU,...
....... kwa kuwa KIHALIHALISI labda NYANI hatafsiri KUNDU la MWENZIYE kama KUNDU hata kama aonalo tu ni KUNDU LA mwenzie kwa mtazamo wa BINADAMU wawaangaliao nyani kwa pembeni,...
... kwa kuwa labda kimawazo ya NYANI labda KUNDULE ni KIKALIO au tu sio KITU KIFIKIRIWACHO kama idhaniwao na BINADAMU wenye akili mpaka wanatumia akili kutafiti mikundu hiyo mpaka KUJIPATIA mpaka MSEMO huo ``Nyani haoni KUNDULE´´ .:-(
Swali:
Si labda ni kweli kuwa kuna uwezekano lakini tetesi ya kuwa ``NYANI HAONI KUNDULE´´ ni tafsiri tu ya BINADAMU aliyewahi tu kuwa pembeni ya NYANI akaona MKUNDU wa NYANI afikiriaye anaelewa NYANI WANATAFAKARI NINI kuhusu MIKUNDU - kitu ambacho labda sio kitu BINADAMU awezacho kuelewa -na kutumia afikiriacho NYANI WANAFIKIRIA katika kujaribu tu kuelewesha MTU yale ya KIBINADAMU?:-(
Ni wazo tu hili dhaifuMHESHIMIWA na wala usikonde!:-(
Hebu Al Green abadili mkao kwa -I'm Glad You're Mine
D'Angelo achokoze kwa kurudia- So Glad You're Mine (Al Green cover)
D'angelo asogeze chupi pembeni kidogo kwa - How does it feel
Hebu D'Angelo, Spanky, Saadiq, Ali Shaheed na ?uestlove wadinye -Lady
1.Mganga mwingine wa tiba za magonjwa Sugu aliyefahamika kwa jina la Jafar Welino(17) mkazi wa mtaa wa Mianzini Kitongoji cha Mabatini jijini Mbeya ameibuka na kutoa tiba kwa mamia ya wakazi wa jiji la Mbeya na viotongoji vyake.
2. Umati wa watu ulionekana katika nyumba anayoishi kijana huyo wakisubiri kupatiwa tiba hiyo huku wakiwa na vikombe vyao mikononi. Baadhi ya wananchi waliofika eneo hilo walidai kuwa wamefika hapo kutokana na taarifa za kuwa kijana huyo anatibu magonjwa Sugu bure kama vile ambavyo anatibu Mchungaji mstaafu wa Loliondo Mzee Ambilikile Mwasapila.
3. Akizungumza kwa niaba ya kijana huyo mama mkubwa wa mganga huyo aliyejitambulisha kwa jina la Edina Sanga alisema kuwa kijana huyo alianza tiba hiyo wiki mbili zilizopita ambapo kabla ya kuanza kutibu alimueleza mama yake huyo kuwa alitokewa na mama yake mzazi a,mbaye kwa sasa ni marehemu akimuelekeza kurithi mikoba yake.
4. Bi.Sanga alisema kuwa mama yake kijana huyo ambaye kwa sasa ni marehemu alikuwa ni mtu mwenye maruhani ambapo kwa kutumia maruhani hayo alikuwa akitoa tiba kwa wakazi mbalimbali mjini Mbeya.Alisema kijana huyo ambaye wamezaliwa mapacha na dada yake aliyemtambulisha kwa jina la Hadija Welino kwamba yeye anasoma kidato cha Nne katika shule ya sekondari Itende.
5. Hata hivyo Bi.Sanga alisema kuwa kijana huyo aliitwa katika ofisi ya Ofisa Mtendaji ili kutoa maelezo ya namna ambavyo anaendesha tiba hiyo na kuwa hata hivyo anaendelea kutoa tiba kwa watu kwa kunywa vikombe viwili kwa muda wa siku mbili. Alisema kuwa dawa hiyo aliifuata katika kijiji cha Iyula kilichopo wilayani Mbozi na kuwa mara alipofika alianza kuichemsha na kuwagawia wananchi wanaosumbuliwa na maradhi sugu. Aidha umati wa watu walikuwa wamejipanga katika mistari kusubiri tiba hiyo ambapo
6. Mwenyekiti wa mtaa wa Mianzini Bi.Elizabethy Mwakabungu aliweka utaratibu wa wananchi kupata tiba ikiwa ni pamoja na kuchangia fedha kidogo kwa ajili ya kununulia kuni za kuchemshia dawa hiyo.Akizungumza na umati wa watu waliokuja kujipatia tiba hiyo Mwenyekiti huyo wa mtaa alisema kuwa kila ambaye atapata kikombe kimoja cha dawa anatakiwa kupata kikombe cha pili siku inayofuata.
7. ‘’Mganga katuagiza kuwa kila anayekunywa kikombe kimoja anatakiwa kunywa kikombe cha pili siku inayofuata…yeyote atakayekunywa hatakiwi kunywa pombe kwa muda wa siku saba,’’alisema Bi. Mwakabungu
....mkabili hata kwa angalau hata kwa KUMSABAHI basi umpendaye ambaye kumtongoza bado UNAHOFIA,...
....fanya mazoezi hata kwenye blogu yake na sio uso kwa uso KUMTUKANA utakaye kumtukana TOKEA SIKU NYINGI kwa kutumia jina lako halisi NA KAMILI ikiwa bado kufanya hivyo uso kwa USO unahofia,.... .....au tu jifunze kumkabili MUNGU hata kwa maombi kama ndiye UNAYEMHOFIA,...
...isije kufanya UMUOGOPE TU ingawa inasemekana ni MUNGU wa upendo na apenda watu kwa hiyo labda sio wa KUHOFIA.:-(
Swali:
Si hata MAJAMBAZI na MAFISADI labda huanza kuua hofu ya kuiba kwa KUPATA PAKUANZIA KUONDOA HOFU -pale kwenye wizi mdogomdogo kabla hawajafikia kukosa hofu katika WIZI mkubwa uhitajio watu wafe kwa kupigwa risasi au tu kwa kuwa dawa za hospitali YA SERIKALI ambazo zingewaponya BOSI kazitumia kumjengea kimada nyumba ya pili?
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
SAMAHANI!
Hebu SAMY DIKO aingilie shughuli ghafla kwa- Je Vous Aime
Au tu Samy Diko aendeleze tu mpekecho kwa -EYAE'E EYA
Ndio ,...
... kwa kawaida siku hizi tunahesabu MIAKA kwa kuhesabu siku ambazo hugeuka MIAKA ,...
.....lakini kuna umri wa KIBAOLOJIA ambao hutokana na ni jinsi gani tumejitunza KIAFYA na ndio uwezao kufanya saa nyingine kuna MIMTU ufikiriayo ni MIZEE na uipayo BONGE ZA shikamoo kumbe ni MIDOGO kwako ,.....
....na UMRI ambao ni mtu anavyojisikia ambao unamisingi yake KISAIKOLOJIA zaidi ambayo huweza kusababisha kufanya LIMAMA au LIBABA zima kuonekana linamitabia au linavaa kitoto.:-(
Lakini,...
Swali liko pale pale kuwa:
Unafikiri USINGEJUA tarehe uliyozaliwa WEYE ungedhania una umri gani?
SI labda UMRI na MIAKA ya mtu ni vitu tofauti?
Nawaza NAKUJIULIZA tu kwa sauti MHESHIMIWA na wala usibanwe chupi!:-(
....katika KUFANYA yawezekanayo ambayo HATUYAFANYI ,... ......labda wengi wetu tutafutacho ni VIZINGITI na VIPINGAMIZI!:-(
Na wakati ili tupate NGUVU ya kuchukua HATUA na kuanza KUTEKELEZA,....
.....tufikiriacho KUFANYA,....
......tutakacho KUFANYA,....
......labda kihitajikacho ni MTAZAMO chanya na MATUMAINI katika ya dalili za WEZEKANO na yawezekanayo na kuanza kufanya kwa kuwa LABDA hakuna chochote ambacho kitakosa VIZINGITI na kitakosa VIKATISHAVYO TAMAA kuanza kama ukivisaka hivyo,....
.... hasa kwa kuwa kwa kuwaza tu sana KIMTAZAMO HASI na woga wa nini ni pungufu katika HALIHALISI YA MTU kabla YA KUFANYA ,...
....yaweza kuwa ndio kitengenezacho KIZUIZI kikubwa cha kutatua matatizo ya mtu na ambacho ndicho hasa BREKI ya cha kufanya kitu ili kujikomboa- KIPINGAMIZI!:-(
Swali:
Au?
Kuna mangapi unafikiri HUFANYI kwa kuwa umejitafutia tu mwenyewe VIZINGITI na vipingamizi na labda hata UDHAIFU ili kuhalalisha HAVIWEZEKANI hata kujaribu KUANZA pambano la kujikomboa?
Ndio,...
... labda kitu KIZURI ,....
... wengi wetu tunakitafuta KASORO na udhaifu ili kujizuia kitu,....
.... na kwa bahati mbaya labda hakuna kitu ambacho ukikichambua ili kusaka KASORO na ,....
..... utakosa udhaifu na KASORO!:-(
Swali:
Si unajua hata MREMBO usiyemuona kasoro kwa kuwa ananukia vizuri bado ukimsachi mpaka utumboni bado utamkuta anatembea na mavi kwenye utumbo?
Ndio,....
.... kama unataka KUFANYA kitu ,...
... ukitaka kupata vizingiti na vipingamizi vya kufanya hivyo vitu ,...
.... utavipata tu MHESHIMIWA!:-(
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA lilengalo WOTE wenye MAAIDIA ya kufanya MAVITU babu kubwa ila WANASITA kuchukua hatua ya KUANZA KUFANYA MAVITU hayo MAKUBWA!:-(
.....SIO kila asikilizaye NENO anatafakari ayasikiayo MANENO,...
..... na ndio maana unaweza kukuta MZINZI yuko bize anasikiliza nyimbo zikatazazo UZINZI bila hata kustukia zinamsuta ,...
... MWIZI fisadi kakaa kanisani mbele kabisa huku akimsikiliza ASKOFU akikemea ufisadi na wizi bila kuguswa,...
... na MSWALIHINA ajuaye maneno yakatazayo nyama ya NGURUWE kwa kuiita ni haramu akiagizia KITIMOTO bila kustukia maneno KITIMOTO na NYAMA YA NGURUWE yanamaanisha kitu kilekile kinamna ambacho ni haramu ,...
.... na bila kusahau UWEZAVYO KUSTUKIA mpaka adanganywaye wakati anatongozwa kwa MANENO ayaliyowazi ni UONGO hakutafakari MANENO ayasikiayo ya kuwa KIDUME asiye na BESENI anadai kila akioga anamuona KIGOLI kwenye BESENI ,...
....au akidai kila wakati ANAMUWAZA YEYE TU wakati yeye atongozwaye na mtaa mzima inajulikana kauli hiyo anamuambia kila KIGOLI na wamwisho kuambiwa hivyo ni shoga ya atongozwaye ,...
..... kitu ambacho kuna wakati humshangaza mpaka mtongozaji mwenyewe AKISHAKUBALIWA.:-(
Swali:
Si unajua MANENO YAKUTISHAYO kwa mtu bila kuyatafakari labda wala hayasemi kitu na nisawa tu na MLIO wa NGOMA kwa asiyejua MLIO wa ngoma waaina hiyo UNAASHIRIA nini hata katika enzi zile ambazo ngoma aka Talking Drums ndio zilipeleka mawasiliano mbali kuwa kwa jirani kuna MSIBA?
Huwa unatafakari MANENO uyasikiayo lakini -au yameshageuka kuwa ni maneno tu kama WATANZANIA wapendao nyimbo za KIKONGO za KOFFI OLOMIDE walivyoridhika kwa kutokuelewa KOFI Olomide katika nyimbo zake MANENO ayasemayo yanamaana gani?
Na si nasikia mpaka WASAINIO mikataba ya TANZANIA huwa hawatafakari maneno ya MIKATABA yanasema na yanamaana gani na ndio maana VITA ya Tanzania na IDI AMIN mikataba ya silaha karibia ifilisi nchi chini ya Nyerere na baada ya Nyerere labda sio siri KUANZIA RADA mpaka mikataba ya MADINI kinachoendelea chamoto twakiona ?
Ndio,...
.... wengi hatutafakari MANENO yana maana gani,.....
... ndio maana labda usishangae ukikuta waimba kwaya , wenye N.G.O za kueneza jinsi ya KUJIKINGA na UKIMWI na WAHUBIRI wakatazao waumini kitu kwa maneno ya nyimbo na MAHUBIRI yao ,...
....wakiongoza KUFANYA yaleyale WAKATAZAYO katika yaliyopo katika MANENO yao wayatumiayo KUKATAZA na kufunza wengine!:-(
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na wala usikonde!:-(
SHIKAMOO basi,...
...Sasa nini kama hata SHIKAMOO hailainishi kitu ili angalau utabasamu?
Lione lile!:-(
Hebu Gelly na AT wabadili tu ili tusikonde zaidi kwa -Binti Yenu
Au tu USWAZI na Shirko wapige-Mwizi
Sijui kwanini lakini hebu tu tena NINA SIMONE arudishe usiriasi katika-I wish I knew how
Aah jamani nawasabahi JAMANI mbona mmenuna namna hiyo?
Naomba TABASAMU kidogo basi!
AKSANTEEEE Dada zangu,.... ... na moja kwa moja ngojea tuongelee mapumbu.!:-(
Ndio,...
...najua kati yenu kuna watundu ambao TAYARI mshawahi kuona hii kitu wakati toto la KIUME linaogeshwa au hata kupapasa hiki KIFAA ,...
....tukiachilia mbali na hata kujua kuwa HII NDUDE ikigongwa inauma kweli kwa hiyo tayari ni wastaarabu na hamjaribu kubinya au hata wakati wa ugomvi kupiga teke hiki kifaa MAKENDE kwa kuhurumia mchango wake kwa vizazi vijavyo.
Na nashukuru kwa hilo yani!
Ila bado ,...
...wanawake WENGI ni miongoni mwa watu wengi wasiostukia kwanini WANAUME wanajihadhari kubinywa KORODANI ,...
...na pia wasiostukia hiki kifaa hakiko kwa ajili ya UZALISHAJI TU wa malighafi shahawa aka MBEGU za KIUME ambazo ni maarufu sana kwa kuchafua mashuka kama tu kusababisha mimba zikilengwa kwenye tundu lenye yai lihitajilo rutuba.:-(
Hiki kifaa kina kazi zaidi ya UZAZI aisee,...
..... kwa kuwa ni chombo kitengenezacho pia HORMONES aka HOMONI ambazo hutumika kurekebisha mwili wa BINADAMU kutokana pia na kuwa na mfumo ujulikanao kama endocrine system au System of Glands ambazo hutengeneza hizi Hormones na kuzimwaga kwenye damu ya mtu ambazo hurekebisha kuanzia UKUAJI wa MTU, anavyojisikia mtu (MOODS) , mpaka jinsi ni kwa spidi gani unasikia njaa kutokana na hizi HORMONES kucheza na ndude METABOLISM ya mwili,...
....ingawa NDIO ,...
...kifaa HIKI hujulikana zaidi labda kwa mchango wake wa sperms au kwa lugha ya kitaalamu SHAHAWA na kwa homoni moja zaidi ya aina ya TESTOSTERONE ambayo inafanya DUME akae kidume ,...
.... yani fulu MIDEVU na minywelenywele bwelele mwilini isababishayo hata gizani kama mjanja ukipapasa ustukie ulipapasalo ni dume RIJALI , misuli mikubwa na mpaka bonge za mifupa kiujazo pia,..
....kitu isababishayo BODE la njemba liwe tofauti kidogo na BODE la kimwana mrembo mwenye kiuno kama nyigu,...
...ikiwa na maana inasaidia DUME lisikae KIJIKE - ki fulu bonge za titi.
Na ukitaka kuijua zaidi hii ndude ninliyopapasa mpaka hapa ,...
....Testicle,....
.....Testosterone ,....
.......kitu kizima ENDOCRINE SYSTEM,.....
.......hormones ,....
.....au hata kitu Sperm aka Shahawa ,...
.....gugo aka GOOGLE tu hizo MSAMIATIZ,...
....ambazo ndizo nimechezanazo katika somo mpaka hapa MKUU kwa shule zaidi isiyo ya juujuu kama ya vidokezo tu niistuayo hapa KIADOADO.:-(
Lakini kwa kifupi ,....
... nafikiri tutakubaliana kuwa MAPUMBU ni muhimu aisee mdada!:-(
Hebu tupate kwanza kielelezo cha hiki kifaa :
Hiki kifaa hutunzwa katika kifuko kilichoumbwa kwa mchanganyiko wa ngozi na misuli ``SCROTUM´´ ambacho kazi yake kubwa ijulikanayo ni kuweka KORODANI kijoto chini ya joto la mwili kwa kuwa KENDEZ zikiwa na joto kama la mwili mbegu za kiume zitengenezwazo huingia udhaifu na kufanya kidume sio kila goli lake lina afya na nguvu kwa kutokana na joto kuathiri kitu kiitwacho na wabongao ung'eng'e - Sperm Count.
Na kutokana na hilo mpaka kuna wadaio bila USHAHIDI WA KITAALAMU kuwa labda MIDUME ijihadhari na chupi aka VIFICHA NYETI vibadavyo sana na kuzuia kazi ya kifuko ya kusogeza makende mbali na mwili joto likizidi na kuyarudisha karibu na mwili kama kipupwe kimezidi kushusha joto za pumbuz .
Hebu tukideku kipicha kifaa:
Hapa ni kitu kikivutwa juu ikiwa kinabaridi iathiriyo joto litakiwalo katika kiwanda cha shahawa na na kikishushwa chini kidogo kimnig'inio ikiwa joto la mwili ni kubwa zaidi kidogo kuliko lihitajiwalo kiwandani.
Na nadhani unakiona wakati kimesogeza BALLS karibu na mwili hapo kulia .
Na kikiachanisha KORODANI na mwili huteremka kama ionekanavyo hapo kushoto.
Kazi hii ya kupandisha na kushusha GOLOLI hufanywa zaidi na Misuli ya cremester aka Cremaster muscle ambayo huvuta pia makende juu kama MHESHIMIWA KIDUME ananyege na kitu kimesimama ,...
... kazi ifanywayo PIA ili kulinda shehena za aina ya KORODANI zisiathiriwe KATIKA KURUPUSHANI hasa wakati mheshimiwa anakula ngoma aka ANANGONOKA.
Mpaka hapa nimepapasa,...
....Cremaster muscle,...
.....Scrotum,....
....na Sperm Count ,...
,....ambazo kwa shule zaidi wewe ZIGUGO tu ukizingati katika taralila hii nazigusia kwa juujuu.:-(
Na kifuko aka KITUNZA MAKENDE HIKI kinasemekana kuwa na undugu sana na Labia Majora kwa wanawake.
Asanteni WADADA,....
... na nimatumaini kuna angalau jambo MOJA ili taralila hii ifanikiwe labda mtalifanya na hilo ni angalau kujiuliza kitu kimoja ambacho kitazalisha angalau MGUGO aka M-Google kitu kimoja zaidi KUTOKANA na TARALILA HIII na kujua angalau kitu kimoja zaidi kuhusu hizi KENDEZI ambazo historia yake kwa UZALISHAJI na hata yakufanya MIDUME iote NDEVU na kuwa na TITI ndogo ukilinganisha na NYONYO za WANAWAKE ,... .... ni tokea enzi za ADAMU na HAWA.
SASA TARALILA inaegemea kwa WANAUME zaidi ,...
..... na hii,...
.... ni KITU siriasi zaidi hasa kwa kuwa inagusa zaidi SARATANI ya Ze PUMBUZ!:-(
Hebu tuanze upya na twende shule kuhusu MAPUMBU,...
...kwa msaada wa MWANADADA,...
..... Dr. Susan Jewell kwa .....
Mdada SUSAN aendelee..
Somo zaidi kwa wanaume kuhusu kucheki hiki kifaa hasa kutokana na saratani ya kiaina ichezayo maeneo kwa kumdeku huyu MDADA akizidi kufunza katika hii-Testicle exam
Kabla sijaacha labda tucheki SHULE MCHANGANYIKO,...
...hasa kwa wazazi ambao wamepata mtoto wa KIUME ambao labda inabidi wajue tu pia kuna kitu kiitwacho-Undescended Testicle kwa kumsikiliza Dr Steven Friedman
Mpaka hapa kwa shule zaidi unaweza KUGUGO,....
....Undescended testicle,....
...Testicular cancer,..
... ambavyo nimevigusa kwa juujuu .:-(
NIMEACHA!
Samahani tunakumbushana tu SWALA na madhumuni ilikuwa nikuchokoza udadisi wako ili udadisi zaidi kujua zaidi kuhusu hii kitu MHESHIMIWA,...
.....na kama umekwazika au hukujifunza kitu KATIKA PROSESI ya KUDAKA USHUSHAJI wangu wa HII ishu KI-UjingaBUSARA maana yake mlengwa wa TARALILA HII haikuwa wewe,...
Lakini UKINONG'ONA ikasikika na utakaye UNONG'ONAYO asisikie,...
... kunakasheshe zake aiseee!:-(
Swali:
Si unajua ukinong'ona ukasikika kuna NOMA aka NISHAI zake hasa kama unong'onacho ni UMBEYA?
Lakini,..
.... kwa kuwa DUNIANI bado kuna MENGI TU labda sio busara KUYAPAYUKA ingawa inajulikana DUNIANI hakuna siri,...
NONG'ONA tu AISEE!
Ila labda
.... ni muhimu kuzingatia ukishapayuka UKASIKIKA labda ndio inaweza kuwa IMETOKA HIYO kama tu maji yaliyomwagika mchangani yasivyozoleka,...
... na itakuwa ni JUHUDI zisizo za msingi kujaribu kuyameza yaliyopayukwa na kusikiwa nakujifanya huyajui kwa UMMA uliokusikia,...
...na kama unakumbuka hilo,...
..... basi ukinistua mie ntasogea UNINONG'ONEZE ,...
...na kwa wengine labda kwa UHURU,...
NONG'ONA TU AISEEE!
Swali :
Si unajua asilimia kubwa ya YANONG'ONEZWAYO ili watu wengine wasisikie huwa KWA KAWAIDA ni ya kawaida sana na labda wala hayastaili KUNONG'ONWA?
Ndio,...
... kama huna uhakika na harufu ya mdomo wako,...
... kumbuka WAKATI UNAMSOGEZEA MTU LIMDOMO LAKO inaweza kuwa unanuka mdomo aisee ,...
...na wakati unamnong'oneza mtu HARUFU YA kitu DOMO ikafanya ANONG'ONEZWAYE aweze kukumbuka UNANUKA DOMO kuliko bonge la UDAKU kuwa Rais MWINYI unadhani aliwahi KUKUKONYEZA ambacho ndicho ULICHOBUNI na ndicho unachonong'ona aisee!:-(
NI wazo tu hili lililokaa kushoto zaidi ya kulia MHESHIMIWA!:-(
DUH labda tubadili kabisaaa ili tuondoke kwenye hili WAZO nishai
NA ,...
....hebu Burning Spear aanzishe upya kwa -Driver
Burning Spear aje NAIROBI kudai-Jah no DEAD
Joseph Hill aje naye hapa hapa NAIROBI na kuongelea tatizo la kuwa-She want Money
..... kuna BAADHI ya MASWALI labda hayana jibu la UHAKIKA KIBINADAMU hata kama kuna watakao jibu na majibu yao kuchukuliwa kama ndio jibu lakusadikika,....
... ndio maana hata kama SASA HIVI kuna wajaribuo kufikiria kuwa wana JIBU la labda YESU angekuwepo KARNE hii angekuwa na BLOGU na angekuwa anafuatiliwa na MTUZ kadhaa wa kadhaa ambao kwenye KIBOXI cha MAONI aka COMMENT wangekuwa wanatoa maoni BWELELE hata ya kumtusi na WAKAAMINIKA kwa kuwa wamedai wameoteshwa kama BABU wa LOLIONDO,...
..... bado wafanyacho sasa hivi KWA MAJIBU YAO HAYO kirahisi LABDA itakuwa ni KUBUNIA TU .:-(
Swali:
SI unajua kuna MAMBO labda yana JIBU ila JIBU lake sio lazima awe nalo MTU?
Si unajuwa jibu la tatizo la KUBUNIA na KUOTESHWA kama la BABU wa LOLIONDO linaweza kuwa ni sawa kama HUNA IMANI na maswala ya KUOTESHWA?
Ndio,... ... labda bado ni kweli kila kitu hata kisichomuhusu MWALIMU NYERERE kina JIBU,...
... ila haki ya nani HAKUNA mtu ajuaye kwa usahihi NA UHAKIKA hilo JIBU .:-(
Swali:
AU?
Na kukosa jibu na kukiri ``HAKUNA JIBU´´- si labda ndio aina moja wapo ya JIBU aka ndio jibu LENYEWE?
Na najua ,...
.... ni silika ya BINADAMU kutafuta MAJIBU,....
..... lakini labda kuna mambo KUTOYAJUA ndio chanzo cha FURAHA maishani ,...
.... kwa kuwa labda KUJUA kila kitu sio UBINADAMU na wala hakuboreshi UBINADAMU,...
.... ukizingatia kuwa hata tukijua kama NYERERE angeanzisha BLOGU angekuwa anafuatiliwa na watu wangapi isingesaidia kuweka tonge mezani mwetu na wala isingetusaidia sana kupata hata kificha nyeti kwa wengi wetu!:-(
NI wazo tu hili MHESHIMIWA!
Hebu tumfuate tena hko Kameruni mdada SANDRA NKAKÉ arudie -I miss my LAND
SI unajua kuna aangaliaye mdada KIBONGE kama njemba tu yenye bonge ya KITAMBI na kuwaza uzuri na ULIMBWENDE wa huyo TIPWATIPWA wakati kuna mwingine wakati huohuo akimuangalia huyohuyo BWANYENYE bonyebonye na afikiriacho kwa UNENE WAKE ni magonjwa na sio ULIMBWENDE wala uzuri wa huyo AJUZA -kitu kimfanyacho afikirie jinsi ya kumshauri apunguze UNENE ili awe na afya njema?
Ndio,...
.....wapigao chabo mchezo huohuo wa unyumba hawafikirii SAWA,....
..... na ndio maana ajali ikitokea BONGO sio wote wakimbiliao palipotokea ajali wanakwenda kuokoa watu ukizingatia wengine wafikiriacho ni DILI LA kusachi maiti mawaleti tayari wakiwa na mipango ya kutanua baadaye BAA kama ikitokea waliofariki ni wengi na walikuwa wanasafiri na NGAWIRA pesa za kutosha kwenda kwao huko uswekeni .:-(
NI wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
Hebu tubadili wazo hili nishai kwa kuangalia mazoezi ya mchezo wa GOLF kiduchu.....
Kuna dogodogo wa engo za BONGO FLEVA na hata za SINDIMBA wasahauo kuna MTUZ kimiziki kama JOHN KITIME ,...
... ndio waliowahi mpaka kupata GRAMMY katika wanamuziki wa TANZANIA,....
GRAMMY kwa MFAFANUO kiduchu ambayo JOHN KITIME kashawahi kupata kwa kutambublika KIMATAIFA kwa UMAHIRI -kwa kibena ni:
A Grammy Award (originally called Gramophone Award) — or Grammy — is an accolade by the National Academy of Recording Arts and Sciences of the United States to recognize outstanding achievement in the music industry. The annual awards ceremony features performances by prominent artists, and some of the awards of more popular interest are presented in a widely viewed televised ceremony. It is the music equivalent to the Emmy Awards for television, and the Academy Awards for film.
The first Grammy Awards ceremony was held on May 4, 1959, to honor musical accomplishments by performers for the year 1958. The most recent ceremony, the 53rd Grammy Awards, was held on February 13, 2011, at the Staples Center in Los Angeles.
Hebu Anania Ngoliga ambaye ni NGULI MWINGINE mwenye kidude Grammy kutoka TZ aka BONGO NYOSO atekenye NENO na kifaa,....
ANANIA adinye zaidi nanihii chini kidogo karibu kabisa na nanihii kwa....
Au tu John KITIME aturudishe kwenye NJENJE ambako anatekenya maswala kwa GITAA na SAUTI katika bendi ya THE KILIMANJARO BAND kama kawa ashambulie jukwaa kwa-Masafa MAREFU
Sijui kwanini ila ngojea tu King Kiki arudie tu naye-MASANTULA
Tahadhari: Taralila hii si nzuri kwa MFANYAKAZI BORA!:-(
Ndio,....
... pamoja nakuwa KUJITAHIDI, kuhangaikia vitu na KUJITUMA kwa wenye busara FARAJA ZAKE ndio huzisifia hata kuzitukuza kwa kubobea katika wadaivyo ni malipo manono mtu upatayo BAADA YA KUJITAHIDI na kuhangaikia,...
.... lakini labda tusisahau kuwa labda kuna FARAJA pia za UVIVU na kuzembea ,...
.... na ndio maana labda kuna MIJITU kibao inazembea na ni fulu KULA kulala.:-(
Swali:
Na si inasemekana kwa hata kwa WAFANYA KAZI kwa BIDII wakishapata wanachohangaikia FARAJA waipatayo kwa hilo haidumu na kwa hiyo itabidi waanze tena upya kuhangaikia kitu kingine ili kufukuzia FARAJA kama hiyo tena?:-(
Ndio,...
....Labda UZEMBE na UVIVU vinafaraja zake pia aisee,...
.... na ndio maana si kila mtu anafuata busara za hata mpaka vifichwavyo na chupi za malaya kuvihangaikia.:-(
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Jumatatu NJEMA na KUJISHUGHULISHA kwenye faraja kwema MKUU!
Hebu twende Kameruni ili Sandra Nkaké arudie kuomba mtu awe-Sex Friend
The Hypnotic Brass Ensemble warudie-Planet Gibbous
Au tu Hypnotic Brass Ensemble wamalizie tu kwa - Balicky Bon
... unastukia kwa UWAZI zaidi kuwa kuna KUANDIKA VIZURI pia kuhitajikako katika UANDISHI haki ya nani tena ,...
... ambako kwa WENGI WETU kunahitaji mazoezi kwa kuwa kwa bahati mbaya hakuji tu HIVIHIVI !:-(
Swali:
SI umestukia kuna waandikao na KUNA WAANDIKAO vizuri hapa DUNIANI?
MAANDISHI ni muhimu,....
.....ingawa labda kuna umuhimu pia waujuao WAANDIKAO vizuri wakaeleweka niwaoneao WIVU!:-(
Nawaza tu kwa sauti MHESHIMIWA,...
.....wakati naendelea kufanyia mazoezi UANDISHI wa kiaina fulani!:-(
Hebu Mos Def arudie mahesabu kwa-Mathematics
Busta Rhymes ajaribu kulainisha zaidi kwa-I Love My Chick
Au hebu NYAMA YA BATA isimuliwe vizuri kinyamunyamu iifanyayo NYAMA HI kuwa NYAMUNYAMU katika ndude ya Off Side Trick akiwa na Mzee Yusuf na Sella wakimuongelea-BATA...