Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ukichunguza wasikilizao maneno yaliyo kwenye NYIMBO ZA DINI na MAHUBIRI au tu hata MANENO yaliyotumika kutongozea waliokubali utagundua,...

>> Thursday, March 24, 2011

.....SIO kila asikilizaye NENO anatafakari ayasikiayo MANENO,...
..... na ndio maana unaweza kukuta MZINZI yuko bize anasikiliza nyimbo zikatazazo UZINZI bila hata kustukia zinamsuta ,...
... MWIZI fisadi kakaa kanisani mbele kabisa huku akimsikiliza ASKOFU akikemea ufisadi na wizi bila kuguswa,...
... na MSWALIHINA ajuaye maneno yakatazayo  nyama ya NGURUWE kwa kuiita  ni haramu akiagizia KITIMOTO bila kustukia maneno KITIMOTO na NYAMA YA NGURUWE yanamaanisha kitu kilekile kinamna ambacho ni haramu ,...
.... na bila kusahau UWEZAVYO KUSTUKIA mpaka  adanganywaye wakati anatongozwa kwa MANENO ayaliyowazi ni UONGO hakutafakari MANENO ayasikiayo  ya  kuwa KIDUME  asiye na BESENI  anadai kila  akioga anamuona KIGOLI kwenye BESENI ,...
....au akidai  kila wakati ANAMUWAZA YEYE TU  wakati yeye atongozwaye na mtaa mzima  inajulikana kauli hiyo anamuambia kila KIGOLI na wamwisho kuambiwa hivyo ni shoga ya atongozwaye ,...
..... kitu ambacho kuna wakati humshangaza mpaka mtongozaji mwenyewe   AKISHAKUBALIWA.:-(

Swali:
  • Si unajua MANENO YAKUTISHAYO kwa mtu bila kuyatafakari labda wala hayasemi kitu na nisawa tu na MLIO wa NGOMA kwa asiyejua MLIO wa ngoma waaina hiyo UNAASHIRIA nini hata katika enzi zile ambazo ngoma aka Talking Drums ndio zilipeleka mawasiliano mbali kuwa kwa jirani kuna MSIBA?
  • Huwa unatafakari MANENO uyasikiayo lakini -au yameshageuka kuwa ni maneno tu kama WATANZANIA wapendao nyimbo za KIKONGO  za KOFFI OLOMIDE walivyoridhika  kwa kutokuelewa KOFI Olomide katika nyimbo zake MANENO  ayasemayo yanamaana gani? 
  • Na si nasikia mpaka WASAINIO mikataba ya TANZANIA huwa hawatafakari maneno ya MIKATABA yanasema na yanamaana gani na ndio maana VITA ya Tanzania na IDI AMIN  mikataba ya silaha karibia ifilisi nchi chini ya Nyerere na  baada ya Nyerere  labda sio siri  KUANZIA RADA mpaka mikataba ya MADINI kinachoendelea  chamoto twakiona ?

Ndio,...
.... wengi hatutafakari MANENO yana maana gani,.....
... ndio maana labda usishangae ukikuta waimba kwaya , wenye  N.G.O za kueneza jinsi ya KUJIKINGA na UKIMWI na WAHUBIRI wakatazao waumini kitu kwa maneno ya nyimbo na MAHUBIRI yao ,...
....wakiongoza KUFANYA yaleyale WAKATAZAYO katika yaliyopo katika MANENO yao wayatumiayo KUKATAZA na kufunza wengine!:-(Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na wala usikonde!:-(
SHIKAMOO basi,...

...Sasa nini kama hata SHIKAMOO hailainishi  kitu ili angalau utabasamu? 

Lione lile!:-(


Hebu Gelly na AT wabadili tu ili tusikonde zaidi kwa -Binti YenuAu tu USWAZI na Shirko wapige-Mwizi


Sijui kwanini lakini hebu tu tena NINA SIMONE arudishe usiriasi katika-I wish I knew how

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP