Chakula cha mawazo: Wanawake VS Wanaume!
>> Wednesday, March 09, 2011
Jana ilikuwa ni siku maalumu ya WANAWAKE ,...
... na katika pitapita zangu nilikutana na MTUZ zijadilizo nani zaidi kati ya WANAWAKE na WANAUME kitu kilichozua mjadala mwingine ulioanzishwa na swaliz:- Hivi ni kweli USAWA unawezekana kupiganiwa na BINADAMU ambaye inajulikana ki asili yake ni mshindani?
- Na hivi kuna kitu usawa kati ya WANAWAKE na WANAUME au hata kati ya BINADAMU mmoja na Mwingine?
Baadhi ya yaliyokuwa yanatekenya watu katika porojo jana ni haya hapa kwenye video clips zifuatazo:
Women are better than Men
Men are better than Women
NI mtekenyo tu wa MAWAZO Mkuu!
Swali:
- Umetekenyeka kidongoloso?
6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Ha ha ha ha! labda ningesema tu wanawake na wanaume wanatofauti kidogo sana ni kwamba wanawake wana huruma ambayo mwanaume hana. Sijapenda hiyo ya dr phil kulinganisha wanawake na mbwa:-(
@Yasinta "kulinganisha wanawake na mbwa"?
Basi atakuwa anaumwa kichwani! Na kusema ukweli sinamuda hata wa kuangalia video yake.
Ninachojua mimi ni kwamba misingi ya mtoto yoyote yule tumboni mwa mama yake ni ya kike: tunakuwa wote wasichana kabla hatujawa wavulana!
Pili, unachokikandamiza ni kile unachokiogopa kwani ukikiachilia kitakuja kukutawala. Hiyo ndio sababu sisi wanaume tunawakandamizeni dada zetu!
Bin-Adamu wote ni sawa bila kujali jinsia, rangi,sura, dini, kabila,uwezo n.k. Hawa watu wanaopenda kushindana kuwa mwanamke ni bora kuliko mwanaume au kinyume chake wana matatizo binafsi yanayowasibu. Aidha wanasumbuliwa na inferiority complex au superiority complex!
BINADAMU wote ni sawa bila kuangalia jinsia ila tunatofautiana kibaiolojia yaani ya mwanamke yuko tofauti na mwanamuke mwenzake pia mwanaume yuko tofauti na mwanaume mwenzake
Pamoja na kwamba tunazo tofauti za kibayolojia, mifumo na imani za kijamii hasa ndizo zimeendeleza kubaguana na kudharauliana huku tunakokuona leo katika jamii mbalimbali.
Mfano mzuri ni hapa Marekani. Hata kama mna kiwango sawa cha elimu na mnafanya kazi sawa, bado mwanamke analipwa mshahara mdogo kuliko ule wa mwanaume. Kwa nini? Kuna sababu yo yote ya msingi ya kuhalalisha unyonyaji huu?
Binadamu (aka Homo Sapiens!)
Inasemekana `` BINADAMU ni sawa ila sio SAWASAWA!´´
Post a Comment