Unafikiri MWALIMU NYERERE angekuwa hai na kaanzisha BLOGU angekuwa na wamfuatiliao WANGAPI?
>> Tuesday, March 22, 2011
Ndio,...
..... kuna BAADHI ya MASWALI labda hayana jibu la UHAKIKA KIBINADAMU hata kama kuna watakao jibu na majibu yao kuchukuliwa kama ndio jibu lakusadikika,....
... ndio maana hata kama SASA HIVI kuna wajaribuo kufikiria kuwa wana JIBU la labda YESU angekuwepo KARNE hii angekuwa na BLOGU na angekuwa anafuatiliwa na MTUZ kadhaa wa kadhaa ambao kwenye KIBOXI cha MAONI aka COMMENT wangekuwa wanatoa maoni BWELELE hata ya kumtusi na WAKAAMINIKA kwa kuwa wamedai wameoteshwa kama BABU wa LOLIONDO,........ bado wafanyacho sasa hivi KWA MAJIBU YAO HAYO kirahisi LABDA itakuwa ni KUBUNIA TU .:-(
Swali:
- SI unajua kuna MAMBO labda yana JIBU ila JIBU lake sio lazima awe nalo MTU?
- Si unajuwa jibu la tatizo la KUBUNIA na KUOTESHWA kama la BABU wa LOLIONDO linaweza kuwa ni sawa kama HUNA IMANI na maswala ya KUOTESHWA?
Ndio,...
... labda bado ni kweli kila kitu hata kisichomuhusu MWALIMU NYERERE kina JIBU,...
... ila haki ya nani HAKUNA mtu ajuaye kwa usahihi NA UHAKIKA hilo JIBU .:-(
Swali:
- AU?
- Na kukosa jibu na kukiri ``HAKUNA JIBU´´- si labda ndio aina moja wapo ya JIBU aka ndio jibu LENYEWE?
Na najua ,...
.... ni silika ya BINADAMU kutafuta MAJIBU,....
..... lakini labda kuna mambo KUTOYAJUA ndio chanzo cha FURAHA maishani ,...
.... kwa kuwa labda KUJUA kila kitu sio UBINADAMU na wala hakuboreshi UBINADAMU,...
.... ukizingatia kuwa hata tukijua kama NYERERE angeanzisha BLOGU angekuwa anafuatiliwa na watu wangapi isingesaidia kuweka tonge mezani mwetu na wala isingetusaidia sana kupata hata kificha nyeti kwa wengi wetu!:-(NI wazo tu hili MHESHIMIWA!
Hebu tumfuate tena hko Kameruni mdada SANDRA NKAKÉ arudie -I miss my LAND
Sandra amwage kitu kiushauri kuwa -Stay True
Au anikune tu tena kwa sindimba-Higher
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
..... lakini labda kuna mambo KUTOYAJUA ndio chanzo cha FURAHA maishani ,..
Na mimi nadhani hapa ndipo binadamu tulipoenda kombo. Tunajitahidi kujua kila kitu na badala yake tunaishia kuishi kwa wasiwasi na hata kugonjweka.
Ni kweli ninahitaji kujua kwamba moyo wangu unapiga sijui mara elfu ngapi kwa siku, unasukuma sijui galoni ngapi za damu kwa siku, na kwamba ukisimama hata kwa sekunde chache tu basi mimi marehemu?
Umegonga pointi mkuu!
Tusichoke kuuliza,kujifunza na kudadisi! japo si kila jibu ni sahihi.
@kaka Matondo nakuunga mkono!
@kaka Kitururu asante kwa maneno machache yenye maana na kujifunza.
Post a Comment