Tuangalie safari MOJA ya MHESHIMIWA MSAFI ya kuelekea kwenye CHOO kichafu!
>> Friday, March 18, 2011
Tahadhari MHESHIMIWA : Wazo Limepinda!:-(
STORI ya kiaina TAIMU:
------------------------------___________-----------------------------__________-------------
Kikao kilianza salama tu ofisini kwa bosi,...
.... ingawa kila mmoja alihisi bosi hayuko kama kawaida yake hasa kwa kuwa safari hii bosi alikuwa anaonyesha dhahiri kutojiamini kitu ambacho wafanyakazi wote hawajawahi kukiona,...
... kutoka na ukweli kuwa bosi huyu ni aina ya wale MABOSI ambao hata kama hawajui KITU hujifanya wanajua na wanaamini kwa kujifanya wanajiamini mbele ya wafanyakazi ndio moja ya kitu kifanyacho walete picha ya wao kuwa ni viongozi bora mbele ya wawaongozao.HALIMA alimfinya pajani AGNESS ambaye ni mfanyakazi mwenzie waliokaa naye karibu kwenye meza ya mkutano huku wote wawili wakijizuia kucheka na kuendelea kujikausha kama vile hawajastukia tofauti ya hali ya hewa ofisini hapo,...
.... kwa kuwa ukweli ofisi nzima ghafla ilianza kunuka kama KINYESI aka MAVI ingawa kama kawaida ya watu wazima hasa wajiheshimuo na wasiotaka kudhalilisha mtu wote ofisini ilibidi wajifanye hawajui kinachoendelea na kujitahidi sana kutofikiria ni nani katika mkutano ule hapo ofisini ndiye mhusika aliyechafua hali ya hewa kwa silaha ya nyuklia aina ya ``USHUZI tepwetepwe ule usiotoa sauti´´.:-(
Na baada ya uvumilivu wa mabomu kadhaa yenye harufu zisizo kifani , kila mtu aliyehudhuria alifarijika kwa kuwa mkutano uliahirishwa. Na wakati wafanyakazi wamepozi koridoni kidogo kujadiliana maswala yaliyoongelewa ofisini kwa bosi wakati wanaelekea makazini kwao ,...
... ghafla ndio wakashuhudia bosi akitoka kule ofisini na kuwapita kwa mwendo wa ajabu kidogo kihatua za kunyata hata USITAJI wa kutingisha tako ,...
...hasa kwa kuwa walijua mwendo wake wa kawaida ni upi kwa kuwa waliozoea kumkodolea macho akitembea hata tu wakati walichokuwa wakifanya ilikuwa ni kutathmini tu ughali wa nguo zake mwanana.
Ila SAFARI hii bosi alichofanya ndicho kiliongezea watu kumuangalia kwa kuwa ALIWACHEKEA PIA wakati anawapita,....
... hasa ukizingatia huyu MHESHIMIWA ni aina ya mabosi ambao wako siriasi sana na huwa hawachekicheki hovyo hasa mbele za wafanyakazi,...
... ingawa baadhi ya wafanyakazi waliowahi kugongana naye BAA akiwa na marafiki zakewakipata MA-COCKTAILS aka KILAJI SHORORO wanadai alionekana yeye ndiye mchekeshaji wa mashoga zake na wakati wote ni fulu kukenua menu hasa kwa staili ile maarufu ya KUTABASAMU.``Vipi tena mbona bosi anaelekea kwenye choo cha wafanyakazi wa kawaida na hivi kuna maji kule kweli?´´- sauti nyingine ilisikika ikinong'ona.
Halafu karibu wafanyakazi wote hata bila kutamka neno walionekana kuunganisha safari hiyo ya bosi, MWENDO WAKE WA KUSUASUA na makombora ya kemikali ya aina ya USHUZI walioyahimili kwa muda mrefu MKUTANONI kwa kujibaraguza hawayastukii kule ofisini kwa bosi,..
...ingawa ilionyesha dhahiri karibu kila mmoja wao hakuwa kastukia kuwa yale makombora aliyekuwa anayatungua kimya kimya kwa staili ya KUYAPOROMOSHA KIMYAKIMYA alikuwa ni bosi yule ambaye ni mwanamama mwanana ambaye kwa wengi pale kazini hata kwa mvuto wake tu ilikuwa tosha kufuta hisia za kumuhusisha yeye KIBOSI mzuri kama MALAIKA na matumizi ya choo kwa staili ya KUSHUSHA kilo za timba aka kunya au tu hata katika lile swala laini lijulikanalo kwa lugha ya kitaalamu kama KUKOJOA.
------------------------------_________________________------------------------------
Safari ya MHESHIMIWA ya kwenda chooni ilianzia ofisini.
Siku hiyo ilikuwa ni ya pili katika ukarabati wa choo chake cha ofisi ambacho alitaka kiwe cha kukaa na sio cha kihindi kwa kuwa alidai maswala ya kuchuchumaa hapendelei na yanamchezo wa kufanya baadhi ya sketi zake kukunjika kunjika asivyotaka hasa ukizingatia yeye anamaindi sana muonekano wa nguo zake ambazo huziagizia Ufaransa tu ambako ndiko alisomea na kuishi miaka mingi kabla ya kuamua kurudi Tanzania.
Na siku hizi mbili za ukarabati wa choo chake binafsi alipanga asiwe kazini ingawa kutokana na dharura akajikuta analazimika kuwepo na pia kuitisha mkutano wa dharura ofisini mwake ili kuhakikisha mambo yanaenda mswano katika KAMPUNI.
Wakati bado anajiuliza maswali yaliyoegemea kwenye kujilaumu ni kwanini itokee siku ambayo ofisi yake yenye kila kitu mpaka bafu ndani iwe na choo kisichotumika siku ile -ndio itokee ana matatizo ya tumbo lenye gesi na sasa anahisi linapiga hatua ya pili na kuashiria uwezekano wa mharo pia,...
.... alijitahidi kutembea kwa madoido AWEZAVYO katika kujaribu kutoweka wazi kuwa kabanwa bonge la haja.Na katika hatua hizo za kujibaraguza alijikuta anachekeachekea wafanyakazi njiani kitu ambacho kilizidi kumstua alipostukia kuchekea kwake watu kunafanya watu wanapigwa na butwaa.
Na baada ya kufika CHOONI pamoja kuwa kabanwa sana na labda hata chupi yake ya mauamaua imeshapigwa kamstari kidogo KANJANONJANO KIUJIUJI ambako hakakuwepo hapo mwanzonin wakati anavalishwa mwili wake MWANANA kificha nyeti hicho cha bei ya GHALI -alihakikisha ana fungua maji mpaka mwisho yajae kwenye ndoo itumikayo kukusanyia maji ya kuchambia na ya kuflashi bidhaa zikisha fanikiwa. Ingawa nia ilikuwa ni maji YAPIGE KELELE TU ili kuua sauti mbalimbali ambazo anajua tayari ndizo atakazo tengeneza wakati anajisaidia haja zote MBILI kuu kwa msukumo na juhudi zote ,...
... ili kama kuna mtu atakaye kuwa nje ya mlango wa choo asiwe na uhakika MHESHIMIWA anaenda choo namba ngapi na kwa staili ipi kwa kuwa alikuwa anaombea makelele ya maji yameze sauti mbalimbali za kitarumbeta mbovu zitakazo tokana na Mheshimiwa kupumua kwa juhudi au tu katika ushushaji tu wa kilo kadhaa TEPWETEPWE huku akijizuia kustukia ni jinsi gani kalazimika kwenda kwenye choo kichafu ,...
... ingawa pia akijisikia UAHUENI a.ka FARAJA kuwa angalau choo cha kujisitiri kakipata kabla ya mambo kuharibika kabisa ,...
....ingawa bado kitu kimtishacho ni fikira zilizomjia ghafla KWA MUDA MFUPI na kumfanya ajiulize kimoyomoyo kama bado anaweza kuchambia maji kwa kuwa yeye ni mtu wa TISHU na kuchambia maji anakuhusianisha na kuchezea mavi kwa kuyashikashika ,.....
....ingawa bado kitu kimtishacho ni fikira zilizomjia ghafla KWA MUDA MFUPI na kumfanya ajiulize kimoyomoyo kama bado anaweza kuchambia maji kwa kuwa yeye ni mtu wa TISHU na kuchambia maji anakuhusianisha na kuchezea mavi kwa kuyashikashika ,.....
....ingawa WAZO hilo lilimpotea tena haraka sana KWA FARAJA ALIYOIPATA baada ya raundi moja na nusu aliyoitekeleza kwa uhuru kabisa yenye mchanganyiko wa vijambo na shehena tepwetepwe ya aina ya uharisho huku bado kidogo AKIRI kwa SAUTI ``Leo ningejinyea kama choo hiki hakikuwepo hapa karibu kwa jinsi nilivyobanwa.:-(´´
Na hiyo ndio ilikuwa moja ya safari ya mheshimiwa mmoja ya kwenda kwenye choo kichafu akidharaucho kwa kuwa hakimuhusu na kwa kawaida hata hakifikirii uchafu au UBORA wake kwa kuwa ni cha mahohehahe wafanyakazi tu ambao kwake hawako sawa naye !:-(
Ndio stori hii imeruka jinsi MHESHIMIWA baada ya kuingia chooni alivyovua chupi ya MAUAMAUA na kufungulia maji yameze kelele za shughuli kwa spidi na nguvu ambazo hata MENDE waliokuwepo hapo chooni walionekana kupigwa butwaa kwa kuwa katika chabo zao hii ya SHUGHULIKO la MHESHIMIWA ilivunja rekodi.
Na ni kweli iliruka PIA hata kipengele cha kuwa MHESHIMIWA kibosile wakati anatoka chooni na huku katika kuwaza anafikia uamuzi wa kurudi NYUMBANI ili kuepuka kujidhalilisha zaidi HAPO kazini - kwa bahati mbaya alijamba kidogo tena safari hii kwa SAUTI mbele za wafanyakazi aliowapita akielekea ofisini ambao nao walimezea tena na kujifanya hawajastukia hata safari hii bomu lile la kemikali!:-(
------------------_____________________________------------------------------------------
Katika kurudisha taralila upande wa BUSARA zaidi na kuliondoa kwenye Ujinga katika UjingaBUSARA
huu:Ndio,...
..... MTU ukidharaucho kama BOSI alivyokuwa anadharau choo ambacho alifikiri hakihitaji ,...
.... kuna siku hicho ukidharaucho huweza geuka MWOKOZI!:-(
Ndio,...
.....kunauwezekano hata mtu ajifanyeje kazoea kutumia UMA, KISU na VIJIKO katika kudadavua NGUNA na kula kwa mkono hawezi,...... ikibidi chakula kwa mkono kinalika tu kwa YEYOTE YULE kama BOSI alivyogundua kuwa KUCHAMBIA maji kunakuja automatiki tu hata kwa ajifanyaye sio mtaalamu kisa kazoea MAKOKONEO ya aina ya TISHU ,...
...na hata bosi mwenye anaweza kukiri kama chooni kulikuwa hakuna maji angebunia TU kitu katika kushughulikia kuchamba na katika ubunifu hata chupi yake ya ghali ya mauamaua ingeweza kufaa tu katika shughuli ingawa ingesaidia pia kuziba choo kama angeiacha kwenye tundu la choo katika staili ya kujaribu kuziba shehena aliyoitengeneza isionekane na watu kirahisi atakaye kuja baada yake CHOONI ingawa bado haitazuia vizuri shughuli za INZI.:-(
Swali:
- Si unajua karibu kila mtu kuna safari fulani hata kama ni mara moja moja humpeleka ajifanyako hakumuhusu kwa kuwa ukweli bado uko palepale hata mtu ajifikirie ni spesho vipi ila kama ni MTU basi kama MTU yawakumbayo watu yatamkuta tu siku moja?
- Na si unajua hakuna la KIBINADAMU lenye uhakika na hata upange vipi kama tu FUKUSHIMA JAPANI kuna kiwezacho kutokea ukagundua ni zaidi ya mipango ujiandaayo nayo na kwa hilo ukahitaji msaada hata wa udhaniacho sio msaada kwako?
Uliotakiwa kuwa ni utangulizi wa Taralila hii:
IKIBIDI na kama nin lazima ,....
... haki ya nani utalazimika KUFANYA mbele za watu uwafichao kitu !
- ni moja ya hoja ya msafiri kafiri aliyeonekana akitokea vichakani kujisaidia.
Njaa ikiuma vizuri UHARAMU wa nyama ya NGURUWE huisha -ni hoja ya MUUMINI mmoja
Choo kichafu hutembelewa na yeyote ahitajiye USITIRI wa choo,...
... na ni pale tu kama MAHITAJI ya choo sio ya lazima sana ndio SISTA DUU au BRAZA MENI Mheshimiwa anaweza kukwepa choo kisa anahisi choo KICHAFU!
-ni hoja ya Mheshimiwa kibogoyo Wakufikirika.
Kwa hiyo,...
.....kama unachagua CHOO MKUU,...
.... wewe hujabanwa vizuri bado!:-(
Ni wazo tu hili KAMANDA Mheshimiwa hata kama limepinda!:-(
Na hebu Phil Colins abadili kwa-Drums na Take Me Home
Phil Collins adungunyue-True Colors
Phil Collins apapasepapase maeneo kwa - In the air tonight
Au tu Phil ajaribu kuzima tu manyanga kwa -Do U remember?
Ingawa sijui kwanini Bryan Adams ngojea aingilie kati tu na kudai- The Only Thing That Looks Good On Me Is You
3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Mkuu wewe bwana mtaalamu wa kutunga hivi vitu, maana kila hatua nivumilia kucheka, kwani nasoma kwa kujiiba, siunajua tena ofisi za watu, uvumilivu ulinifanya nitoe kicheko cha ghafla na kila mtu aliniangalia kwa kushangaa!
TUPO PAMOJA MKUU, SAFI SANA, HATA UWE BOSI NAMNA GANI HIYO KITU HAINA CHA NANI AU NANI KIKIKUPATA UJUE AIBU HAIPO!
Umenikumbusha mbali sana na Phili Collins namkubali sana.
@M3: :-)
@Edna: Jamaa mtundu yani!
Post a Comment