Wakati inadhaniwa na BINADAMU kuwa NYANI haoni KUNDULE,......
>> Sunday, March 27, 2011
.......labda kiendeleacho hasahasa kama asemaye hilo/HUO MSEMO ni BINADAMU ni kuwa,....
.... hivyo ni ADHANIAVYO tu na idhaniwavyo tu na BINADAMU,...
....... kwa kuwa KIHALIHALISI labda NYANI hatafsiri KUNDU la MWENZIYE kama KUNDU hata kama aonalo tu ni KUNDU LA mwenzie kwa mtazamo wa BINADAMU wawaangaliao nyani kwa pembeni,...
... kwa kuwa labda kimawazo ya NYANI labda KUNDULE ni KIKALIO au tu sio KITU KIFIKIRIWACHO kama idhaniwao na BINADAMU wenye akili mpaka wanatumia akili kutafiti mikundu hiyo mpaka KUJIPATIA mpaka MSEMO huo ``Nyani haoni KUNDULE´´ .:-(
Swali:
- Si labda ni kweli kuwa kuna uwezekano lakini tetesi ya kuwa ``NYANI HAONI KUNDULE´´ ni tafsiri tu ya BINADAMU aliyewahi tu kuwa pembeni ya NYANI akaona MKUNDU wa NYANI afikiriaye anaelewa NYANI WANATAFAKARI NINI kuhusu MIKUNDU - kitu ambacho labda sio kitu BINADAMU awezacho kuelewa -na kutumia afikiriacho NYANI WANAFIKIRIA katika kujaribu tu kuelewesha MTU yale ya KIBINADAMU?:-(
Hebu Al Green abadili mkao kwa -I'm Glad You're Mine
D'Angelo achokoze kwa kurudia - So Glad You're Mine (Al Green cover)
D'angelo asogeze chupi pembeni kidogo kwa - How does it feel
Hebu D'Angelo, Spanky, Saadiq, Ali Shaheed na ?uestlove wadinye -Lady
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment