Kuna MAMBO labda YAFANYE matusi au YASEME tu SASA hivi wakati UMRI unaruhusu!:-(
>> Saturday, March 19, 2011
Ndio,...
... kwa kuwa UKINGOJEA ili uyafanye BAADAYE ,...
... au UYASEME baadaye,....
... hasa katika JAMII HII ambayo kwa kawaida ina MAMBO ambayo imeshajiwekea kuwa hata kitendo cha kumvumilia MTOTO ALAMBAYE kamasi hutegemea MTOTO alambaye malighafi HIZO za pua ana UMRI GANI,.......inaweza kukuona hufai KUHESHIMIKA ukingojangoja kufanya mengine baadaye ambayo labda inatakiwa UYAFANYE SASA HIVI.:-(
Swali:
- SI unajua kuna uwezekano hata UVAAVYO baadaye ukikuwa kidogo KIMINI chako SKETI au KIBWAYA - kitakuwa hakifai kuonwa katika JAMII ya siku hizi ambayo paja kidogo tu kuonekana ASHKI KIBAO hupanda WATU WAZIMA na VIJANA -hata kama bado unamapaja mazuri kwa kuwa ushakuwa LIMAMA na jamii inaamini LIMAMA ni nishai kuvaa kama kigoli wa miaka kumi na tano?
- Au?
- SI inasemekana MICHAEL JACKSON kwa kuanza ukubwani kuchezea midoli amabyo labda angetakiwa kuichezea UTOTONI wakati anafanya ya KIKUBWA ile JAMII HIIHII ilishindwa kumuelewa?
Ndio,...
....labda KUNA MAMBO ni ruksa kwa mtoto au KIGOLI ambaye jamii inaamini bado hajajua kustukia maswala ya kiutu UZIMA,........ na kuna ambayo usipofanya SASA hivi au kusema sasa hivi KIDUME aka NJEMBA,...
Ndio,..
...hili ni WAZO TU Nguli!:-(
Hebu Hypnotic Brass Ensemble katika kubadili wazo waingizie-WAR
Bassekou Kouyate na Ngoni Ba wabadili mchezo kidogo ingawa aimbaye ni Amy Sacko mke wa Bassekou ambaye kwa KIAFRIKA zaidi alawalawishe kwa-Jonkoloni
Bassekou Kouyate aendeleze zaidi mdindo kwa - Ngoni Fola
Bassekou Kouyate na Ngoni Ba waguseguse chini kidogo zaidi karibu na nanihii kwa- Segu Blue
Au tu Hypnotic Brass Ensemble wazime ndude kwa-Brass in AFRICA
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment