Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MITAZAMO ya nani ni rahisi bila utafiti wa asemayo KUSIKILIZWA !:-(

>> Thursday, March 03, 2011

Wafananao na WEWE ,...

.... yasemekana ni rahisi WEWE kuwasikiliza na KUAMINI wasemayo,...
.... na ndio maana inasemekana  kuna asilimia kubwa ya WALIOOA ukichunguza utastukia wanafanana na WALIOWAOA kiaina.:-(





Samahani naanza TARALILA hii  upya!:-(


Tokea mtu azaliwe,....
......alipozaliwa kuna tabia za kujua nini , WALIOMZAA wanaamini nini, MPAKA mazingira aliyokulia wanamchezo wa kuamini nini kilaliwacho na nini haramu kama moja ya kimchango tukiruka mengine,....
......VINAMCHANGO kwenye MITAZAMO yake  ya NI NANI ZAIDI anaweza   bila kufanya utafiti  kuamini  tu kwa KUMSIKILIZA!:-(



Na  labda NI KWELI,....
.....BINADAMU anamchezo  wa KUJIFUNZA YA KUAMINI NI KWELI hata  ya kijinga KIJINGA kwa kuwa ni kawaida kwa MTU kutofikiria kila  kitu kwa MAKINI hasa kutokana na wingi wa anayombananayo MAISHANI YALIVYO MENGI ukifuatilia  kila kitu tokea azaliwe,....

..... kitu  kifanyacho kuna BAADHI ya mambo mengi tu ambayo MTU huyachukulia ni kweli kutokana tu  na ukweli kazaliwa katika MAZINGIRA FULANI ambayo ni kawaida hayo mambo  kuchukuliwa kama ni UKWELI hata bila utafiti BINAFSI,....

..... kwa kuwa tu WAZAZI awaheshimuo, AWATAMBUAO kama wasomi MAHIRI na kuamini tu labda ni wajuzi wa SWALA, na yote ambayo yanachangia ``COMMON SENSE ZAKE´´ kufanya aamini  ni kweli hata kama ni  UKWELI tu kwa kuwa ni MTAZAMO ausikiao UKIRUDIWARUDIWA nakutamkwa kama ndio kweli,...
...... na kwa kitu KURUDIWARUDIWA kinamchezo wakuchukuliwa tu ni sahihi na WATU  hata kama usahihi wake HAUJAHAKIKISHWA na mtu binafsi ,...
.... na MTU  anapata TU  faraja kujioanisha nao MTAZAMO  kwa kuwa ndio yaliyozoeleka na ndiyo yaaminiwayo na  anao WASIKILIZA!:-(

SWALI:
  • Si kuna sababu unaona matangazo ya COCA COLA , PEPSI na Colgate yanavyorudiwarudia mpaka  watumiao hivyo vitu  wanasahau kuwa labda hawajavitafiti  na wakiviona huvinunua kwa kuwa ndivyo WAVISIKIAVYO na labda yote ni kwasababu tu  ya WALIYOSIKILIZA?

  • SI inajulikana  ni rahisi  kwa mtu kuamini  hata UKRISTO na UISLAMU kuwa ni DINI ZA KWELI bila utafiti binafsi KIRAHISI TU kama kwenye familia atokayo, MAZINGIRA  watokayo, na kwa WANAOWAHESHIMU ndio kinachoaminika hata kama ni bila utafiti maalumu BINAFSI kwa kuwa tu ndio kirudiwachorudiwacho  wanacho SIKILIZA?


Ndio,....
.... kwa kuwa MAISHANI  tuna mengi,....
.... kuna ambayo HATUFANYII UTAFITI  ilituyaamini,.....
.... na tunayaamini ni KWELI kutokana tu na kuwaamini  wanaotuzunguka TUNAO WASIKILIZA.:-(


Na kwa kuwa BINADAMU anamchezo wa kusahau kuwa  kwa kuwa tu tumejifunza kuheshimu mtu kutokana na kuheshimu kipaji chake cha KUCHEZA FUTIBOLI a.k.a KABUMBU,...
.... labda bado ukweli uko palepale DAVID BECKHAM  labda MTAZAMO wake KIIMANI , SIASA , anafikiriaje mademu WASAGAJI au hata katika swala zima la MISOSI na KUJIPIKILISHA hauna nguvu na wala haustahili KUHESHIMIKA hata kama akisema tunasikiliza.:-(

Swali:
  • Si umeshawahi kusikia washabiki wa KABUMBU wakisikiliza kwa makini David BECKHAM anawaza nini  kuhusu maswala ambayo labda ayajuaye kiusahihi ni Rais Mheshimiwa GADDAFI wa Libya  hata kama kuna wenye nia ya kujua kitu ambao kutokana tu na WALIYOSIKILIZA kutoka kwa wanaowaamini -GADDAFI hastahili KUHESHIMIKA na kusikilizwa?




Na labda KLOROKWINI  ni dawa tu ya MALARIA yenye sumu tu kama nyingine,....
.... na dawa nyingine ni bora katika kutibu MALARIA mpaka wabadilishapo mtazamo tuwaaminio na KUWASIKILIZA!:-(

Na labda kila siku tutaendelea kusikia MATANGAZO ya Coca Cola na Colgate  kama wengine tu walivyoyasikia kutokea UTOTONI mpaka UZEENI hata kama yanaletwa kwa ladha nyingine,...
....ili tusiache kuamini watakayo tuamini WENYE KAMPUNI  hata kama ni MAILUMINATI  kuhusu vitu hivyo kwa kuwa kuna wahusika wanajua TUNASIKILIZA!:-(



Na sio MAKAMPUNI na DINI tu zipendazo kurudiarudia maneno  ili wasikilizao waamini hata bila kufanya utafiti wa kuwa LABDA katika hayo wasikiayo kuna wenye mitazamo mingine,...
.... kwa kuwa ni kweli  kitu kikirudiwarudiwa kuna hata MWANZO ambao HAWAKUAMINI  ila mwishowe hufikia kufanya kama walivyopingananavyo mwanzoni wakati wanatumia akili kufikiri kwa kuwa tu LABDA vya kutosha WAMESIKILIZA!:-(

Swali:
  • Si inasemekan kwa kusikiliza MARA KWA MARA sana kuhusu jinsi AFRIKA kulivyokuwa na UKIMWI  kutoka na wenye DATA aka STATISTIKI a.ka NAMBA BUNIFU za IDADI -kuna watu wanaamini karibu kila mtu ugonganaye mitaani AFRIKA ya CHINI ya jangwa la SAHARA labda ana vijimdudu kama waaminivyo kila mtu ni MASIKINI na anaishi juu ya miti Afrika kwa kuwa habari wasikiazo ni za umasikini na MAGONJWA tu kutoka  AFRIKA ?
NDIO,....
.... labda ni mengi UAMINIYO kama MIMI TU NIAMINIVYO ambayo ni zao tu  la TUNAYOYASIKILIZA,...
.... na utafiti hatufanyi kwa kuwa tuna kisingizio,....
......tuko BIZE kwa hiyo kama tumuaminiye kisa anasura ya UPOLE asemacho kuhusu somo la SAYANSI ambalo hakulisomea  TUTAAMINI  kwa kuwa ndiye tunaye MSIKILIZA!:-(



Na LABDA ,...
...kuna uwaaminio kisa WAMEFANANA na wewe tu kinamna na hakuna lingine,...
....na hapa naongelea kufanana kuwezako kuwa ni kwa LIPUA LAKO  mpaka kufanana tu KIIMANI kisa wote sio wachawi mkubalianako ingawa yeye kavaa KIBWAYA cha MAJANI YA MIGOMBA - ingawa hata kwa HILO  unasahau labda maswala ya vitambaa vya kushonea magauni ya saresare za KITCHEN PATI zisizo fanana na VIBWAYA - huyo LABDA  sio wa kumsikiliza !:-(

Naendelea kuwaza na NI RUKSA kunibishia......:-(
NA  NI WAZO tu hili MHESHIMIWA wala usikonde!:-(


Tubadili kidogo WAZO na kujiliwaza kwa kuangalia tena MDADA akijivunia makalio---




Au tuendelee tu kidogo wakati najaribu kufikiria wanawazanini hawa wakati wanaselebuka...



Au tu pumzike TOFAUTI kwa kucheki mara ya kwanza MBUNGE mwanaume kuvaa hereni Bungeni hapo Kenya .....

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 3:11 pm  

Duh, mkuu umenigusa nami nikawa nawaza ...`HIVI KWANINI WATU TUWE BENDERA KUFUATA UPEPO, TUKASUKUMWA HATA BILA KUJUA WAPI TUNAPOKWENDA, LABDA NI KWASABABU YA KAWAIDA, KUWA KILA MSUKUMO KUTOKA matawi ya JUU UNA NGUVU ZAIDI, na huo mvumo unaweza ukawa `ALAMA ZA NYAKATI'?
Tutapata muda kweli wa kutafiti, wakati kuna mvumo wa kutisha? tena wa kutoka kwa mkuu wa dola kubwa! Labda ndio `nyakati hizo'. Wasiwasi wangu mkuu, ni je twaweza kutafiti kile kilichowekwa lebo ya `FROM TAIFA KUBWA'
Nimewaza tu mkuu!

Simon Kitururu 8:53 am  

@Mkuu M3:Yani umenizidishia mawazo yani!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP