Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kabla hujafungua mtu UBONGO nakustukia anakutamani kama unavyomtamani!

>> Thursday, March 10, 2011

 Ndio,...
.... TAMAA zipo,
........CHUKI ipo,
...........AMANI ipo,
..............UMBEA upo,
................na MATUMAINI yapo,....

.......pale BINADAMU walipo!:-(


 Kitishacho ni  ukweli ,...
.......TAMAA zipo
...........CHUKI ipo,
...............AMANI ipo,
...................UMBEA upo,
..................... na KILA KITU kilichopo,....
....... kipo kuanzia NDANI yetu wenyewe,...
........ hasa kwa kuwa yote huishi katika BINADAMU ambao ni MIMI na WEWE hapahapa tulipo hata kama ni UBONGONI  MWETU tu,...
... na kwa bahati mbaya sio tu kwa wengine KULE  ambako ni rahisi kuwanyoshea vidole kule WALIPO!:-(


Swali:
  • Au?
  • Hujawahi  kujishangaa mwenyewe hata kwa jinsi uwezavyo kukasirika siku nyingine mpaka ukastuka kwa kustukia kwa mara ya kwanza jinsi gani unavyoweza kugeuka mpaka UKAJISHANGAA kwa KUGEUKA mazingira na ishu vikiruhusu ?

Ndio,..
... labda mengi tuyaonayo wengine wafanyayo hapa  DUNIANI hata yatushangazayo,...
..... yamo tu kwenye DNA na hulka  za binadamu mpaka sisi,...
... na labda mazingira  yakijipanga vizuri  karibu kila mmoja wetu anaweza kula na kuokota makopo MAJALALANI!:-(



Swali:
  • Si unakumbuka kunibishia nni RUKSA?


Mengi tuyalalamikiayo WENGINE ,...
... LABDA yamo tu ndani yetu,...
... na ukifungua mtu  KICHWA na kuusoma UBONGO wake unawaza nini labda unaweza kukuta awazacho BI KIDUDE na alichokuwa anawaza Mama THERESA  kama tu Mama Maria ,...
...LABDA kiubinadamu wake  ni sawa!:-(


Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(






Jill Scott abadili wazo kwa -A Long Walk




Jill Scott aendelee kwa -Gettin' In The Way




Au tu Jill Scott amalizie kwa-Golden

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP